Rasimu ya Katiba Mpya imechukua sura mpya, ikidaiwa kuwa muundo wa serikali tatu, unakamilisha hitaji la kundi la wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) maarufu kama G55, likihusishwa na Jaji Joseph Warioba.
G55 ni kikundi kilichowajumuisha wabunge 55 wakiwamo Njelu Kasaka (Lupa) na Philipo Marmo (Mbulu), ambacho mwaka 1994, waliibua hoja ya kuwepo serikali ya Tanganyika na kudaiwa kuungwa na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Mpya, Jaji Warioba.
Katibu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, Luteni mstaafu Hamis Chifupa, ameiambia NIPASHE Jumamosi, kuwa serikali tatu ni hatua ya kuuvunja Muungano na kuiweka nchi katika hali tete.
Chifupa ambaye ni baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge machachari kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Amina Chifupa, alisema muundo huo ulitegemewa kwa vile Jaji Warioba, aliiunga mkono G55 katika suala la Tanganyika.
“Rasimu ni nzuri, lakini kuhusu suala la kuwepo kwa serikali tatu, limenishtua sana kwa sababu katika sera ya CCM, haizungumzii kuwapo kwake bali serikali mbili,” alisema.
Chifupa alisema hata Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, alitahadharisha kuhusu uwepo wa serikali tatu, hasa kuibuliwa kwa ile ya Tanganyika.
Hata hivyo, Chifupa alisema ‘mtego’ wa mapendekezo ya serikali tatu, umefanywa na Tume ya Katiba Mpya inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Kwa mujibu wa Chifupa, Jaji Warioba alikuwa miongoni mwa wabunge waliokuwa upande wa kundi maarufu lililojulikana kama G55 ambalo mwaka 1994, liliunga mkono hoja ya aliyekuwa Mbunge wa Lupa, Njelu Kasaka, kutaka iwepo kwa Tanganyika.
Alisema kitendo cha wabunge hao kuidai Tanganyika, kilimkera Mwalimu Nyerere, aliyeonyesha kutokubaliana na muundo wa serikali tatu kwa madai ingesababisha kuvunjika kwa Muungano na kulisambaratisha taifa hili.
“Sikushangazwa sana na mapendekezo ya Tume ya Warioba kuhusu kuwepo kwa serikali tatu, kwani yeye alikuwa miongoni mwa kundi la G55 ‘kulilia’ taifa hilo, hata Mwalimu Nyerere alimuonya tulipokutana uwanja wa ndege wa Dar wakati akienda Msumbiji mwaka 1994,” alisema.
Katibu huyo mstaafu alisema, akiwa pamoja na Warioba siku hiyo, Mwalimu Nyerere, alimfokea (Warioba) kwa kumuita Sinde ni Mtanganyika nay eye (Mwalimu) ni Mtanzania.
“Ushahidi wa maneno hayo ninayo, kwani tulikuwa tumekaa pale uwanja wa ndege katika makochi mekundu tukiwa watatu…sasa kwa mapendekezo ya Tume ya Warioba kupendekeza serikali tatu, sikushangazwa,” alisema Chifupa.
Hata hivyo, alisema pamoja na Nyerere kumkemea Warioba, lakini alimgusa Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, wakati huo akiwa Spika.
Kwa mujibu wa Chifupa, Msekwa, hakumridhisha Mwalimu Nyerere kwa kuruhusu suala hilo kujadiliwa na wabunge.
“Nyerere alihofia matukio mawili iwapo kutakuwepo na serikali tatu, moja nchi kwenda mrama na pili kuwapa nafasi maadui kuweza kujipenyeza kupitia mianya ya kuvurugika kwa Muungano,” alisema.
Chifupa aliwataka Watanzania kusoma kitabu cha Mwalimu Nyerere kiitwacho ‘Tanzania na Hatma ya Uongozi Wetu’, kwani kuna sehemu kinaelezea iwapo Tanganyika itazaliwa tena, lazima Tanzania itakufa.
Aliwashauri viongozi wa chama hicho kutoshabikia rasimu hiyo katika kipengele cha mapendekezo ya serikali tatu, kwani kufanya hivyo ni kumgeuka muasisi wa taifa hili, Mwalimu Nyerere.
Alitoa mfano katika kura za maoni zilizofanywa mwaka 1994 na serikali ya CCM katika mkoa wa Mara, iwapo serikali ipi inafaa kati ya tatu, mbili na moja, alisema jumla ya wanachama 79,124 walipendekeza serikali mbili.
Pia Chifupa alisema katika tukio hilo, 70,646 walitaka serikali moja na 3,609 walitaka serikali tatu.
CHANZO: NIPASHE

About mahamoud
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:
Post a Comment