RIPOTI: MAAFISA WA RWANDA WANACHOCHEA GHASIA MASHARIKI MWA KONGO

M23 rebels (file photo)
Waasi wa M23





Maafisa wa kijeshi wa Rwanda wanachochea ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema.

Kwa mujibu wa ripoti ya “siri” yenye kurasa 43 ya Kundi la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa, Kikundi cha waasi wa M23 kinaendelea kutoa mafunzo kwa wapiganaji wake kutokea Rwanda na kwa msaada wa maofisa wa kijeshi wa Rwanda, shirika la habari la Reuters liliripoti jana Ijumaa. Reuters inasema kuwa imeiona ripoti hiyo.


"Wataalamu hao walituma barua kwenda kwa serikali ya Rwanda tarehe 14 Juni 2013 wakiitaka ufafanuzi juu ya hatua yake ya kuwasaidia waasi na kusubiri jawabu,” wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa walisema katika ripoti hiyo.

Wataalamu hao waliwasilisha ripoti hiyo mbele ya Kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia vikwazo vya Kongo.


Umoja wa Mataifa na Kongo wamekuwa wakizituhumu Rwanda na Uganda kuwa zinawasaidia waasi nchini Kongo.


Rwanda na Uganda zimekuwa zikikanusha tuhuma hizo za kuwaunga mkono waasi wa M23, lakini hazijawahi kuwalaani hadharani waasi hao, ambao wamekuwa wakiongeza nguvu zao katika majimbo ya Kivu ya Kaskazini na Kivu ya Kusini katika eneo la mashariki mwa Kongo.




Makundi kadhaa yenye silaha, ikiwemo M23, wanaendesha harakati zao za uasi mashariki mwa Kongo na wanapigania kuidhibiti nchi hiyo kubwa yenye maliasili za madini, kama vile dhahabu, urani, coltan, ambayo hutumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya elektroniki, ikiwemo simu za mkononi.

Waasi wa M23 waliuteka mji wa Goma Novemba 20, 2012 baada ya walinda amani kuondoka  katika mji huo wenye wakazi milioni moja. Wapiganaji wa M23 waliondoka katika mji huo Desemba 1,2013 baada ya makubaliano ya kusimamisha mapigano.

Waasi wa M23 walijiondoa katika jeshi la Kongo mwezi Aprili 2012 kupinga kile walichodai kuwa ni mwenendo mbaya ndani ya jeshi la Taifa (FARDC). Walikuwa wamejumuishwa katika jeshi chini ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2009.

Tangu mwezi Mei 2012, takriban watu milioni 3 wameyekimbia makazi yao katika eneo la mashariki mwa Kongo. Takriban watu milioni 2.5 ni wakimbizi wa ndani, huku zaidi ya watu 460,000 wamekimbilia katika nchi za Rwanda na Uganda.

Kongo imekuwa ikikabiliwa na matatizo matatizo kwa miongo kadhaa, kama vile umaskini uliokithiri, miondombinu mibovu, na vita katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambavyo viliibuka tangu mwaka 1998 na kugharimu maisha ya zaidi ya watu milioni 5.5.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment