Amani ya Zanzibar itavurugwa na Maalim Seif-CCM


Vuai Ali Vuai; Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema mihimili ya amani visiwani  Zanzibar imetetereka na kuyumba tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Novemba mwaka 2010.
Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai katika mkutano wake na waandishui wa habari uliofanyika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja jana kufuiatia kuibuka kwa vitendo vya hujuma dhidi ya viongozi wa serikali,dini pamoja na kuibuka kwa kundi linalofanya kampeni za kutaka kuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Vuai alisema wakati umefika kwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi kufanya tathmini ili kuangalia Zanxzibar ilikofikia tangu kuundwa kwa SUK kutokana na misingi ya amani na umoja wa kitaifa kuanza kutikisika.
“Amani ya Zanzibar imeanza kutetereka tangu kuundwa kwa SUK,BLM na BLW wanapaswa kufanyai tathmini mhali ilikofikia na hatma yake”Alisema Vuai ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Khamis  na Katibu wa NEC Zanibar Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Mhandisi  Hamad Masauini .
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo alisema katika kipindi cha miaka miwili tokea kuundwa kwa SUK viongozi wa ngazi za Serikali na madhehebu za diniwamekuwa wakimwagiwa tindikali na kupigwa risasi huku mamshambulizi hayo yakiwalenga zaidi watu wenye itikadi fulani ya kisiasa na mali  kuharibiwa.
Alisema makanisa na msaskani za CCCM yamechomwa moto pamoja na uharibifu wa  miundombinu ya Serikali  kinyume na malengo na madhumuni ya kuundwa kwa Serrikali iliopo ya kuondosha mivutano ya kisiasa ili kudumisha amani na mshikamano wa Kitaifa.
Alisema hali ya m,ani na umoja wa kitaifa inaendelea kuzorota baada ya kuibuka kikundi cha wanasiasa wanaoungwa mkono na wafuasi wa CUF ambao hufanya kampeni za kuvunja Mjuungano wa Tanganyika na Zanzibar kupitia mjadala wa mabadiliko ya katiba bila ya kuheshimu sheria na taratibu halali.
Akiizungumzia kauli iliotolewa na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seifa Sharif Hamad aliyoitoa katika mkutano wa hadhara na kumtaja Rais mstaafu Dk Amani Abeid Karume kwamba anashirikiana nae kuhakikisha  hadi Zanzibar ikipa dola  kamili,Vuai alisema tamko hilo linalenga kumkaangia mbuyo Dk Karume na kumuhasimisha na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shain.
“Kauli ya Maalim Seif imelenga kujenga fitna kati ya Rais Dk Shein na Dk Karume,ameonyesha wazi yeye ni muumini na mtiifu kwa Rais Dk Karume  si kwa Dk Shein ambaye ndiye aliyemteua na kumuapisha kuwa Makamo wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar”Alisema Vuai.
Akikinukuu kifungu cha 39(1)(5) alisema Makamo wa Kwnza ni mshauri mkuu wa Rais wa Zanziabr lakini kinyume chake amelitumia jukwaa la kisiasa ili kumfuja na kumdhalilisha mbele ya umma akimwita ni mtu anayeshindwa kutekeleza ahadi zake ikiwemo kuwapatia vitambulisho vya uzanzibari mkaazi wananchi wa Unguja na Pemba.
Akiielezea Kamati ya maridhiano inayopinga mfumo wa Muungano wa Zanzibar alisema haina Baraka za CCM na wanaojiita wajumbe kutoka CCM ni watu waliojiteua kwasababu hakuna kumbukumbu za CCM zinazoonyesha kuitea kamati hiyo.
Vuai alisema Kamati inayojiita ya maridhiano ni ya wanachama jina na kusaka pochi ambayo imeamua kujivikia joho la kuitetea Zanzibar huku ikijinasibisha kuwa ndiyo ilioleta serikali ya umoja wa kitaifa wakati jambo hilo lilitokana na maamuzi yaliofikia Butiama mwama 2008.
“Kampeni zinazofanywa na Maalim Seif na kikundi chake za kuingilia kazi za mabadiliko ya katiba lengo lake kubwa ni kuleta vurugu kabla ya rasimu ya katiba kutolewa na kujadiliwa kwenye mabaraza ,bunge la katiba na baadae kupigiwa kura ya maoni”Alisema Vuai.
Alisema kitendo cha Maalim Seif kumsaliti hadharani Rais Dk Shein si kipya machoni mwa wazanzibari kwani huko nyuma pia aliwahi kumzunguuka Rais Aboud Jumbe Mwinyi  na kunyanyasa kisiasa Rais Idris Abdul  Wakil hadi wote walipoondoka madarakani.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM Zanzibar alisema Maalim Seif hawezi kuwa msemaji wa wazanaibari wote kupinga muungano wakati hakuna vikao vya wananchi waliopitisha maazimio hayo hasa kwa kuzingatia kuna vyama vingi na kiloa chama kina sera na msimamo wake.
“Kuna taarifa za siri za kikundi hicho kumuendea Rais wa awamu ya tano Zanzibar  Dk Salmin Amour wakimtaka awaunge mkono harakati zao za kupinga muungano,tunashukuru kwa majibu aliyowapatia kuwa anaheshimu na kufuata msimamo wa chama chake”Alisema Vuai.
Alisema Kamati ya Moyo ni ya wachumia tumbo ambao alidai wamelenga kuleta vurugu na kuligawa Taifa kwa maslahi binafsi na kuwataka wananchi wa Zanzaibar na Bara kuwa makini na wanasiasa wanaotaka kuvunja muungano kupitia mchakato  wa mabadiliko ya katiba.
Akihutubia mkiutano wa hadhara juzi akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya maridhiano,Maalim Seif alisema wazanzibari hawatakuwa tayari kukubali rasimu ya katiba mpya ikiwa haijazingatia Zanzibar kupata dola yake kamili ikiwemo kuwa na kiti umoja wa mataifa na kujiamulia mambo ya ndani na nje.
Source: NIPASHE
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment