Wanafunzi sekondari Mzumbe waandamana kumwona RC



WANAFUNZI zaidi ya 600 wa shule ya sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wameandamana kwenda ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kumuelezea kero zao. Kero hizo ni pamoja na ubovu wa miundombinu na lugha chafu kutoka kwa walimu. Wanafunzi hao ambao walitoka shuleni hapo saa 8.00 usiku walizuiliwa kufika ofisi za mkuu wa mkoa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia katika Kijiji cha Kasanga Maliasili.
Inaelezwa kuwa wanafunzi hao walifunga barabara kuu ya Morogoro -Iringa upande mmoja saa kadhaa huku magari yakiendelea kutumia njia moja.

Wanafunzi hao walikataa kuzungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Elia Ntandu ambaye alifika katika Kijiji cha Kasanga Maliasili ili kuzungumza nao. Kwa mujibu wa wanafunzi hao, walisisitiza kumuona Mkuu wa Mkoa, Joel Bendera ambaye kwa sasa yuko nje ya mkoa kikazi.

Hali hiyo ilisababisha mvutano uliodumu kwa zaidi ya saa mbili hadi hatimaye walipokubalu kuzungumza na katibu tawala huyo.

Katika kueleza kero zao wanafunzi hao, pamoja na mambo mengine walitaka Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Dismas Njawa ahamishwe na walimu wenzake.

Mmoja wa wanafunzi hao, Emil Mayani alisema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile miundombinu mibovu, ikiwamo choo bafu za kuogeza hazina milango, mabweni machakavu huku baadhi yakiwa hayana umeme.

Nyingine ni chakula kibaya, ubadhirifu wa fedha za shule, ukosefu wa mwalimu wa somo la fizikia kwa kidato cha tano, walimu wengi kutofundisha ipasavyo na lugha chafu ya baadhi ya walimu.

Alipoulizwa, Mkuu wa Shule hiyo, Dismas Njawa alidai masuala mengi waliyozungumza wanafunzi hao hayana ukweli wowote na ni uzishi wa wanafunzi wachache tu.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment