Wapiganaji wa PKK wakifanya mazoezi kaskazini mwa Iraq |
Kundi la waasi wa Kikurdi (PKK) nchini Uturuki limesema kuwa wapiganaji wake wameanza kuondoka Uturuki kuelekea katika ngome zao kaskazini mwa Iraq.
Gultan Kisinak, kiongozi wa chama chenye mrengo wa Kikurdi cha (BDP), alisema kuwa kundi la kwanza la wapiganaji hao limeanza kuondoka leo kuelekea mpakani mwa Iraq.
Ocalan, ambaye alikamatwa na vikosi vya Serikali ya Uturuki katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, mwaka 1999, anatumikia kifungo cha maisha katika gereza moja kwenye kisiwa cha Imrali kwa makosa ya kuongoza kikundi cha PKK na kuanzisha mapigano na Serikali ya Uturuki.
Katika taarifa iliyotolewa na kundi hilo mapema Jumanne ya jana, lilisema kuwa zoezi hilo "litaendelea katika utaratibu maalumu uliowekwa."
Kundi la PKK limekuwa likipigania kujitenga kwa eneo la kusini mashariki mwa Uturuki tangu miaka ya 1980. Mgogoro huo umegharimu maisha ya makumi kwa maelfu ya watu.
Wapigana kadhaa wa PKK wanaaminika kuwa wanaishi nchini Uturuki, huku tawi lake la kijeshi likiwa na ngome yake kaskazini mwa Iraq.
0 comments:
Post a Comment