Moja ya matukio ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Libya, Tripoli. |
Duru za kiusalama nchini Libya zinasema kuwa shambulizi la bomu limekiharibu vibaya kituo kimoja cha polisi katika mji wa mashariki mwa nchi hiyo wa Benghazi.
“Kifaa chenye mripuko kilitupwa kwenye kituo cha polisi cha Al-Baraka mjini Benghazi, na kuharibu mabaki ya jengo hilo ambalo lilikuwa limeshambuliwa pia wiki moja iliyopita. Lakini hapakutokea maafa," kilisema chanzo hicho.
Mnamo Aprili 27, askari mmoja wa Libya aliuawa baada ya watu wenye silaha kukishambulia kituo cha ukaguzi cha Uqba bin Nafae katika mji wa bandari wa Derna, ulioko kilometa 800 (maili 548) kusini mwa mji mkuu, Tripoli.
Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuidhibiti mipaka yake na kuzirejesha silaha zilizoibiwa baada ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Kanali Muammar Qaddafi kuuawa mwaka 2011.
Serikali kuu ina udhibiti mdogo nje ya mji mkuu, na nchi hiyo imegawanyika sana kuathiriwa na makundi yenye silaha, makabila na koo mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment