MILIPUKO YA MABOMU YAITIKISA PAKISTAN

13.05.2011 пакистан теракт пакистан жертвы пакистан взрыв пакистан





Milipuko miwili ya mabomu imeutikisa mji wa Karachi nchini Pakistani na kuuwa watu wasiopungua 8 na kuwajeruhi wengine 20 wakati huu ambao nchi hiyo inafanya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia. Mlipuko mmoja ulimlenga mmoja wa wagombea katika uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo, vimeripoti kuwa milipuko hiyo ilitokea mjini Karachi katika eneo la Landhi.

Bomu moja lililengwa kwenye ofisi za chama cha Awami National Party (ANP), ambacho ni miongoni mwa vyama vitatu vya kisekula na kilebirali ambavyo inasemekana kuwa vimekuwa vikilengwa na wapiganaji wa Taliban.

Mgombe wa chama cha ANP, Aman Ullah aliweza kukwepa bomu lililokuwa limemkusudia yeye.

Mlipuko mwingine unaripotiwa kutokea mjini Karachi katika eneo la Quaidabad jirani na kituo cha kupigia kura, likaharibu majengo kadhaa ikiwa ni pamoja na maeneo ya biashara.

Radio Pakistan imeripoti kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mir Hazar Khan Khoso alilaani mashambuli ya Karachi na kuagiza kupatiwa matibabu kwa majeruhi wote.

Mamilioni ya wapiga kura nchini Pakistan wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa kihistoria, ambao ndio uchaguzi wa kwanza wa kubadilishana madaraka kwa amani katika historia ya miaka 66 ya nchi hiyo. Lakini ghasia zimezuka kwa kuwa wapiganaji wa Kitaliban wanaiona demokrasia kuwa ni jambo lilo kinyume na Uislamu. Usalama katika maeneo ya kupiga kura umeimarishwa huku maelfu ya vikosi vya usalama vikiwekwa kwenye vituo vya kupiga kura ili kuwazuia wapiganaji hao wasiingilie mchakato huo.


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment