JESHI LA NIGERIA KATIKA OPERESHENI NZITO DHIDI YA BOKO HARAM


Nigeria’s army has launched a military campaign against militants in the northeast. The file photo shows Nigerian soldiers of a parachute regiment.


Jeshi la Nigeria limeanzisha kampeni kubwa ya kijeshi dhidi ya waasi katika maeneo ya mipakani kufuatia Rais wa nchi hiyo kutangaza hali ya hatari katika maeneo ya kaskazini mashariki.



Mamlaka zinasema kuwa jana alhamisi jeshi la nchi hiyo lilitumia ndege za kivita, helkopta na vikosi vya ardhini katika operesheni kubwa katika majimbo ya kaskazini mashariki ya Borno, Adamawa na Yobe.



Kampeni hiyo ya kijeshi inalenga kulidhibiti eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa Boko Haram ambao wameweka kambi mbalimbali huko.


Mnamo Mei 14, Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu, wiki moja baada ya waasi kufanya mashambulizi kwenye kambi za jeshi, vituo vya polisi na gereza moja mjini Bama katika Jimbo la Borno. Zaidi ya watu 50 waliuawa na waasi wakasababisha wafungwa 100 kutoroka.



Rais wa Nigeria alieleza kuwa nchi inakabiliwa na uasi ambao "unatishia vikali umoja wa kieneo." "Baadhi ya maeneo ya Borno yameshachukuliwa."


Aidha, hali ya hatari imetangazwa katika Jimbo la Adamawa, huku huduma za simu za kiganjani zikizimwa kabisa katika eneo hilo.


Boko Haram imedai kuhusika na mashambulizi na milipuko kadhaa nchini humo tangu mwaka 2009.


Kwa zaidi ya miaka minne, ghasia katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo zimegharimu maisha ya zaidi ya watu 3,500. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment