HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI 2013/14



 HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
MHE. PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
KWA MWAKA 2013/14

ORODHA YA VIFUPISHO

AFD - French Development Agency

AfDB - African Development Bank

BADEA - Bank of Arab for Economic Development in Africa

BGM - Bulyanhulu Gold Mine

BOT - Bank of Tanzania

BZGM - Buzwagi Gold Mine

CAMARTEC - Centre for Agricultural Mechanisation and Rural Technology

CBOs - Community Based Organizations

CCM - Chama Cha Mapinduzi

CFL - Compact Florescent Light

CIDA - Canadian International Development Agency

CNG - Compressed Natural Gas

DBSA - Development Bank of Southern Africa

DFID - Department for International Development

EU - European Union

EWURA - Energy and Water Utilities Regulatory Authority

FINIDA - Finland Department for International Development Agency

GEF - Global Environment Facility

GGM - Geita Gold Mine

GPM - Golden Pride Mine

GST - Geological Survey of Tanzania

GVEP - Global Village Energy Partnership Program

HFO - Heavy Fuel Oil

HSBC - Hong Kong and Shanghai Banking Corporation

ICEIDA - Icelandic International Development Agency

IDA - International Development Association

IFC - International Finance Corporation

ISO - International Organization for Standardization

JBIC - Japan Bank for International Corporation


ORODHA YA VIFUPISHO

JICA - Japan International Cooperation Agency

kV - Kilovolti

Mb. - Mbunge

MCC - Millenium Challenge Corporation

MCIMS - Mining Cadastral Information Management System

MKUKUTA - Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania

ML - Mining License

MoU - Memorandum of Understanding

MRI - Mineral Resources Institute

MVA - Megavolt Ampere

MW - MegaWatt

MWh - MegaWatt-hour

NACTE - National Council for Technical Education

NBS - National Bureau of Statistics

NDC - National Development Corporation

NEMC - National Environment Management Council

NGOs - Non-Governmental Organisations

NLGM - New Luika Gold Mine

NMGM - North Mara Gold Mine

NORAD - Norwegian Agency for Development Cooperation

NSSF - National Social Security Fund

OC - Other Charges

OFID - OPEC Fund for International Development

ORIO - Facility for Infrastructure Development (Netherlands)

PAYE - Pay As You Earn

PICL - Petroleum Importation Coordinator Limited

PL - Prospecting License

PLR - Prospecting License with Reconnaissance

PML - Primary Mining Licenseiii

ORODHA YA VIFUPISHO

PPA - Power Purchase Agreement

PPP - Public Private Partnership

PPRA - Public Procurement Regulatory Authority

PSAs - Production Sharing Agreements

PSPF - Public Service Pension Fund

QDS - Quarter Degree Sheet

REA - Rural Energy Agency

REMAs - Regional Miners Associations

RMO - Resident Mines Officer

SDL - Skills Development Levy

Sida - Swedish International Development Cooperation Agency

SIDO - Small Industries Development Organisation

SML - Special Mining Licence

SPM - Single Point Mooring

SPV - Special Purpose Vehicle

SSMP - Sustainable Solar Market Package

SSPA/T - Standardized Small Power Purchase Agreement/Tariff

STAMICO - State Mining Corporation

TANESCO - Tanzania Electric Supply Company

TANSORT - Tanzania Diamond Sorting Organisation

TAZAMA - Tanzania - Zambia Pipeline Limited

TBS - Tanzania Bureau of Standards

TEDAP - Tanzania Energy Development and Access Expansion Project

TEITI - Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative

TGM - Tulawaka Gold Mine

TIPER - Tanzania International Petroleum Reserve

TMAA - Tanzania Minerals Audit Agency

TPA - Tanzania Ports Authority

TPDC - Tanzania Petroleum Development Corporationiv

ORODHA YA VIFUPISHO

TRA - Tanzania Revenue Authority

TTM - TanzaniteOne Tanzanite Mine

TZS - Tanzanian Shilling

UDSM - University of Dar es Salaam

UNDP - United Nations Development Programme

UNEP - United Nations Environment Programme

UNICEF - United Nations Children’s Fund

UNIDO - United Nations Industrial Development Organization

USAID - United States Agency for International Development

USD - United States Dollar

VAT - Value Added Tax

VETA - Vocational Education Traininig Authority

WDL - Williamson Diamonds Limited

WHT - Withholding Tax

ZMO - Zonal Mines Officer

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2013/14





A. UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kutokana na Taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2012/13 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara na Taasisi zilizo chini yake kwa Mwaka 2013/14.
2. Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupata fursa hii ya kuwasilisha ndani ya Bunge lako Tukufu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2013/14. Awali ya yote, napenda kuwashukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.) kwa miongozo na ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, nawashukuru Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb.), Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Nishati, Mhe. Stephen Julius Masele (Mb.), Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Madini kwa  
                     ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kuongoza Wizara.
3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kukupongeza wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge na Wenyeviti wote wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa uongozi wenu mahiri katika kuliongoza Bunge hili na Kamati zake. Kwa namna ya pekee, natoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Victor Kilasile Mwambalaswa (Mb.), Makamu Mwenyekiti Mhe. Jerome Dismas Bwanausi (Mb.) na wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa mchango wao mkubwa katika kuchambua Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2013/14. Aidha, pamoja na upya wake, Kamati hiyo imekuwa ikitoa ushauri unaolenga kuboresha utendaji wa Wizara kwa maslahi ya Taifa, hasa katika kuhakikisha kwamba umeme wa uhakika unapatikana ili kuwezesha ukuaji wa uchumi wetu.
4. Mheshimiwa Spika, Mwezi Machi, 2013 Bunge lako Tukufu lilimpoteza Mhe. Salim Hemedi Khamis, Mbunge wa Chambani, Kisiwani Pemba. Naungana na wenzangu kutoa pole kwa Bunge lako, familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.
5. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2012/13.


B. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA WIZARA KWA MWAKA 2012/13
6. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wizara iliendelea kutekeleza mipango yake ili kuhakikisha kuwa Sekta za Nishati na Madini zinachangia ipasavyo katika ukuaji wa uchumi na Pato la Taifa. Kazi zilizopangwa kutekelezwa katika Sekta ya Nishati ni: kuongeza miundombinu ya gesi asilia; kuendeleza shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia; kusimamia biashara ya mafuta; kuongeza uwezo wa kufua umeme; kujenga njia za kusafirisha na kusambaza umeme; kuongeza kasi ya kupeleka umeme katika Makao Makuu ya Wilaya na maeneo ya Vijijini; kuhamasisha matumizi ya nishati jadidifu katika ufuaji wa umeme; kuhamasisha matumizi bora ya nishati; na kudurusu na kuandaa sera, sheria na mipango kwa ajili ya kusimamia Sekta ya Nishati.
7. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kufanyika katika Sekta ya Madini ni kuboresha utoaji na usimamizi wa leseni za madini; kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini; kuhamasisha uongezaji thamani madini; kuimarisha soko la madini ya vito; kuimarisha usalama, afya na utunzaji wa mazingira migodini; kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI); kuongeza fungamanisho la Sekta ya Madini na sekta nyingine za uchumi; ujenzi na uboreshaji
wa ofisi za madini; na kuziwezesha Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kwa manufaa ya Watanzania.
Ukusanyaji wa Mapato
8. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wizara yangu ilipangiwa kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 193.01. Hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2013 jumla ya Shilingi bilioni 157.29 zilikusanywa, sawa na asilimia 81.5 ya lengo. Juhudi za ukusanyaji zinaendelea ili kuhakikisha kuwa Wizara inafikia lengo hilo.
Matumizi
9. Mheshimiwa Spika, Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2012/13 ilikuwa Shilingi bilioni 641.27. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 110.08, sawa na asilimia 17.2 zilikuwa ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi bilioni 531.19, sawa na asilimia 82.8 zilikuwa ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Hata hivyo, Bajeti hiyo iliongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 826.27 kutokana na ongezeko la Shilingi bilioni 185.00 katika Bajeti ya Miradi ya Maendeleo kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mitambo ya kufua umeme.5
10. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2013 jumla ya fedha zilizopokelewa na Wizara kutoka Hazina zilikuwa Shilingi bilioni 740.91, sawa na asilimia 89.7 ya Bajeti yote ya Wizara kwa Mwaka 2012/13.


SEKTA YA NISHATI
Hali ya Uzalishaji Umeme
11. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wizara imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme nchini. Hadi kufikia Mwezi Aprili, 2013 uwezo wa mitambo ya kufua umeme (installed capacity) ulikuwa MW 1,438.24 (gesi asilia – asilimia 35, maji – asilimia 39 na mafuta – asilimia 26) ikilinganishwa na uwezo wa MW 1,375.75 uliokuwepo Mwezi Juni, 2012. Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2012 kiasi cha umeme kilichoingizwa kwenye Gridi ya Taifa kilikuwa MWh 5,759,756 ikilinganishwa na MWh 5,153,400 Mwaka 2011 sawa na ongezeko la asilimia 11.8. Aidha, mahitaji ya juu kabisa ya umeme kwa Mwaka 2012/13 yalifikia MW 851.35 Mwezi Oktoba, 2012 ikilinganishwa na wastani wa MW 820.35 kwa Mwaka 2011/12. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 3.8. Sababu ya ongezeko hili ni kutokana na kukamilika kwa miradi mingi ya umeme vijijini.


SEKTA NDOGO YA UMEME
Kuongeza Uwezo wa Kufua Umeme
12. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini, Serikali imechukua hatua mbalimbali ambazo ni pamoja na:
(i) Ujenzi wa Mtambo wa MW 60 Mwanza
13. Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kusimamia ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa MW 60 utakaotumia mafuta mazito (HFO) katika eneo la Nyakato, Mwanza. Ujenzi wa kituo hicho umekamilika Mwezi Mei, 2013 na unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Mwezi Juni, 2013. Kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kutaboresha upatikanaji wa umeme na kuimarisha Gridi ya Taifa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
(ii) Mradi wa Kinyerezi I - MW 150
14. Mheshimiwa Spika, ili kupunguza utegemezi wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia mafuta ambayo ni ghali, Serikali imeendelea kutekeleza mradi wa Kinyerezi - I (MW 150). Mradi huo utakaotumia gesi asilia na ujenzi wa njia za umeme za msongo wa kV 220 (Kinyerezi - Kimara) na kV 132 (Kinyerezi - Gongolamboto) utagharimu Dola za Marekani milioni 183.30, sawa na Shilingi bilioni 293.28. Mkandarasi wa
mradi huo ni M/S Jacobsen Electro AS kutoka Norway na Mshauri ni M/S Lahmeyer kutoka Ujerumani. Mkandarasi amelipwa malipo ya awali ya Dola za Marekani milioni 30, sawa na Shilingi bilioni 48 kutoka Hazina zikiwa ni fedha za Watanzania. Utekelezaji wa Mradi huo umeanza Mwezi Januari, 2013 na umepangwa kukamilika Mwaka 2014/15.
(iii) Mradi wa Kinyerezi II – MW 240
15. Mheshimiwa Spika, Japan Bank for International Corporation (JBIC) ya Japan ambayo itatoa mkopo wa asilimia 85 ya gharama za mradi wa Kinyerezi – II imewasilisha Serikalini Rasimu ya Mkataba wa Mkopo. Serikali itatoa asilimia 15 ya gharama za mradi. Gharama za mradi huo ni Dola za Marekani milioni 432, sawa na Shilingi bilioni 691.20.
(iv) Mradi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira MW 200
16. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Serikali imekamilisha taratibu za kisheria za kuurejesha Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira kutoka Kampuni ya “TanPower Resources Ltd”. Baada ya hatua hiyo, Serikali kupitia STAMICO ilifanya majadiliano na Kampuni ya “China National Plant Import and Export Corporation Ltd” (COMPLANT) ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huu. Gharama za mradi zinakadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 400, sawa  
na Shilingi bilioni 640. Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kufua umeme wa MW 200 kwa hatua ya awali.
(v) Mradi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka MW 400
17. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ngaka unaendelezwa na Kampuni ya TANCOAL Energy Limited ambayo ni Kampuni ya ubia kati ya Serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC (asilimia 30) na Kampuni ya Intra Energy Limited ya Australia (asilimia 70). Kampuni hiyo imeendelea na uchimbaji wa makaa ya mawe ambapo kwa kipindi cha kuanzia Agosti, 2011 hadi Aprili, 2013 jumla ya tani 166,775 za makaa ya mawe zilizalishwa, ambapo tani 121,685 ziliuzwa nchini na katika nchi za Kenya, Malawi, Mauritius na Uganda. Mauzo hayo yalikuwa na thamani ya Shilingi bilioni 14.66, sawa na Dola za Marekani milioni 9.16 ambapo Serikali imepata mrabaha wa Shilingi milioni 439.77, sawa na Dola za Marekani 274,856. Kampuni ya TANCOAL Energy Limited inapitia upya Taarifa ya upembuzi yakinifu (feasibility study) kwa ajili ya kujenga mitambo ya makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 400. Aidha, majadiliano kati TANESCO na TANCOAL Energy Limited kuhusu Mkataba wa Kuuziana Umeme (PPA) pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 220 kutoka Ngaka hadi Songea yatakamilika katika Mwaka 2013/14. Mradi huu utagharimu  
takriban Dola za Marekani milioni 400, sawa na Shilingi bilioni 640.
(vi) Mradi wa Kufua Umeme wa Mchuchuma MW 600
18. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Kampuni ya Sichuan Hongda ya China kwa kushirikiana na NDC imechoronga mashimo 40 ya utafiti yenye jumla ya kina cha mita 8,800. Mradi huo unaendelezwa kwa ubia kati ya NDC (asilimia 20) na Kampuni ya Sichuan Hongda (asilimia 80) unatarajiwa kufua umeme wa MW 300 katika awamu ya kwanza na unatarajiwa kukamilika Mwaka 2015/16. Mradi mzima utagharimu Dola za Marekani bilioni 1.2, sawa na Shilingi bilioni 1,920.
(vii) Mradi wa Somanga Fungu MW 320
19. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imekamilisha majadiliano ya mkataba wa kuuziana umeme (Power Purchase Agreement - PPA) na Kampuni ya “Kilwa Energy Ltd”. Baada ya Mkataba huo kuidhinishwa na EWURA, Kampuni hiyo itaanza utekelezaji wa mradi huu kwa awamu ambapo kwa kuanzia itafunga mitambo ya uwezo wa kufua umeme wa MW 230. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 365, sawa na Shilingi bilioni 584. Majadiliano kati ya Kampuni ya Kilwa Energy Ltd na TANESCO kuhusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Somanga Fungu hadi Kinyerezi, Dar es
Salaam katika msongo wa kV 220 yatakamilika mwishoni mwa Mwezi Juni, 2013.
(viii) Mradi wa Ufuaji na Usambazaji wa Umeme – Biharamulo, Mpanda na Ngara (ORIO)
20. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, uchambuzi wa zabuni ya ujenzi wa mradi wa ufuaji na usambazaji wa umeme katika miji ya Biharamulo, Mpanda na Ngara umekamilika na utekelezaji wake utaanza Mwaka 2013/14 na kukamilika Mwaka 2014/15. Mradi huu unahusisha ukarabati na upanuzi wa mfumo wa usambazaji umeme pamoja na ufungaji wa jenereta tatu zenye uwezo wa kufua umeme wa MW 2.5 kila moja katika maeneo hayo. Gharama za mradi huu ni Euro milioni 33, sawa na Shilingi bilioni 66.
(ix) Mradi wa Kufua Umeme Murongo – Kikagati
21. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, Serikali ilidhamiria kutekeleza mradi wa kufua umeme wa MW 16 kwa kushirikiana na Serikali ya Uganda (MW 8 kwa kila nchi). Hata hivyo, baada ya kupitia kwa kina rasimu ya Mkataba wa mradi huo, imebainika kuwepo kwa upungufu katika rasimu hiyo. Kutokana na hali hiyo, tumeamua kupitia upya vipengele vyote vya Mkataba kabla ya kuanza kwa utekelezaji kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi yetu. Gharama za mradi huo  
ni Dola za Marekani milioni 30.46, sawa na Shilingi bilioni 48.74.
(x) Ukarabati wa Mitambo katika Vituo vya Kufua Umeme
22. Mheshimiwa Spika, ukarabati wa vituo vya kufua umeme kwa kutumia maji vya Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Mtera na New Pangani Falls umeanza, baada ya kupata fedha kiasi cha Krona milioni 63 kutoka Serikali ya Norway, sawa na Shilingi bilioni 18.20. Kampuni ya “Verkis” kutoka nchini Iceland ambayo itasimamia utekelezaji wa mradi imepatikana. Aidha, uchambuzi wa zabuni za kupata Wakandarasi wa kukarabati vituo hivyo unaendelea.
(xi) Mradi wa Aggreko wa MW 100
23. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, Wizara kupitia TANESCO ilihuisha Mkataba wa kufua umeme kiasi cha MW 100 na Kampuni ya Aggreko kwa mwaka mmoja zaidi. Uhuishaji wa mkataba huo ulifikiwa baada ya makubaliano ya kupunguza bei za kuuziana umeme pamoja na urejeshaji mtaji (Energy and Capacity Charges) kwa takriban asilimia 34.  
Ruzuku kwa TANESCO
24. Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa Mwezi Agosti, 2011 Serikali iliamua kuidhamini TANESCO ili ipate mkopo wa Shilingi bilioni 408, sawa na Dola za Marekani milioni 255. Hata hivyo, kutokana na taratibu za mikopo za kibenki, TANESCO imeweza kupata Dola za Marekani milioni 65 tu, sawa na Shilingi bilioni 104. Hivyo, Serikali kulazimika kuingilia kati na kutoa Shilingi bilioni 402.23 kama ruzuku badala ya mkopo.
Kujenga Njia za Kusafirisha na Kusambaza Umeme
25. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa uimarishaji njia za kusafirisha na kusambaza umeme, Serikali iliendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo:
(i) Uboreshaji wa Huduma za Umeme Jijini Dar es Salaam
26. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imefunga jumla ya transfoma mpya 15 katika vituo vya Buguruni, City Centre, Kariakoo, Kipawa, Mbagala, Mbezi, Oysterbay na Ubungo. Vilevile, ufungaji wa transfoma mpya katika vituo vya Bahari Beach, Gongo la Mboto, Kigamboni na Kunduchi upo katika hatua za mwisho za utekelezaji. Mradi huu utakamilika Mwaka 2014/15 na utagharimu Dola za  
Marekani milioni 75, sawa na Shilingi bilioni 120. Ufungaji wa transfoma hizo utaimarisha upatikanaji wa umeme Jijini Dar es Salaam.
27. Mheshimiwa Spika, kazi ya kubadilisha nyaya zenye ukubwa wa milimita 150 na kuweka zenye ukubwa wa milimita 432 pamoja na kubadilisha nguzo zilizooza kwenye njia ya umeme ya kV 33 Ilala – Kurasini imekamilika kwa asilimia 99. Kazi iliyobaki ni kukarabati maungio yote tangu mwanzo wa njia hadi mwisho. Njia hii ya umeme ilikuwa inakatika mara kwa mara na kusababisha wateja wa maeneo ya Kigamboni, Kurasini, Mbagala na Mkuranga, kukosa umeme wa uhakika. Baada ya ukarabati kukamilika, wateja wa maeneo hayo sasa wanapata umeme wa uhakika.
28. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na kumpata Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya M/S ELTEL Group OY kutoka Finland kwa ajili ya kutekeleza mradi wa huduma za umeme Jijini Dar es Salaam. Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Finland kwa gharama ya Euro milioni 25, sawa na Shilingi bilioni 57.50 na Serikali itachangia Euro milioni 1.50, sawa na Shilingi bilioni 3.45. Uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo utafanyika tarehe 24 Mei, 2013, Dar es Salaam.
(ii) Mradi wa North - West Grid kV 400
29. Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kubadilisha msongo wa njia ya kusafirisha umeme kutoka kV 220 hadi kV 400 kwa mradi wa North - West Grid ambao utapitia maeneo ya Nyakanazi – Kigoma – Katavi – Rukwa hadi Mbeya ili kukidhi matarajio ya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika maeneo hayo. Maombi ya mkopo yamewasilishwa katika Benki ya Exim ya China kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Mradi huu utakapokamilika utaimarisha mfumo na upatikanaji wa umeme katika Mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Mbeya, Rukwa na Shinyanga. Gharama za awamu ya kwanza inakadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 136.25, sawa na Shilingi bilioni 218.
(iii) Mradi wa Makambako – Songea kV 220
30. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Serikali ilikamilisha durusu ya kuongeza uwezo wa njia ya umeme (upgrade) ya Makambako hadi Songea kutoka msongo wa kV 132 kwenda kV 220 (usafirishaji – kilomita 250 na usambazaji – kilomita 900). Mshauri wa mradi ni Kampuni ya SWECO International kutoka Sweden. Vilevile, zabuni ya kupata Mkandarasi wa kusambaza umeme katika maeneo ya mradi imetangazwa na itafunguliwa mwishoni mwa Mwezi Mei, 2013. Utekelezaji wa mradi umepangwa kuanza Mwezi Agosti, 2013. Mradi huu utakapokamilika utawezesha Mkoa wa Ruvuma kuunganishwa  
kwenye Gridi ya Taifa na kuimarisha juhudi za usambazaji wa umeme katika Miji ya Makambako, Njombe na Songea na katika Wilaya za Ludewa, Mbinga na Namtumbo.
(iv) Mradi wa Iringa – Shinyanga kV 400 (backbone)
31. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 670. Kwa sasa, zabuni za Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa njia kuu na vituo vya kupozea umeme zinachambuliwa. Serikali kupitia TANESCO imeanza kulipa fidia katika maeneo ya mradi. Mradi huu ambao gharama yake ni Dola za Marekani milioni 650, sawa na Shilingi bilioni 1,040 utakapokamilika utaimarisha Gridi ya Taifa, kupunguza upotevu wa umeme na kuongeza uwezo wa kusafirisha umeme wa kutosheleza mahitaji ya Kanda ya Kaskazini Magharibi. Mradi huu pia utahusisha usambazaji wa umeme vijijini katika maeneo ya mradi. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwaka 2015/16.
(v) Kuimarisha Njia za Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme
32. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imeendelea kubuni miradi ya kuboresha usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini. Katika kutekeleza miradi hiyo, vifaa vya kisasa vya kulinda mifumo ya Gridi yaani power system
protection relays vimenunuliwa na kufungwa katika vituo vya Iringa, Kidatu, Mufindi, Mwanza, Shinyanga na Singida. Aidha, vifaa maalum vya kugundua hitilafu kwenye njia za umeme (fault locators) vimenunuliwa na kufungwa katika vituo vya Chalinze, Hale, Kidatu, Msamvu na Ubungo. Gharama za mradi huo ni Dola za Marekani 503,862 sawa na Shilingi milioni 806.18.
33. Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara limekuwa kati ya kero kubwa kwa watumiaji wa umeme nchini. Sababu za kuwepo kwa tatizo hili ni pamoja na: uchakavu wa miundombinu ya usambazaji umeme na vifaa vyake; kuzidiwa uwezo kwa mifumo ya usambazaji umeme; na wizi wa nyaya za shaba na mafuta ya transfoma, hususan kwenye Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga. Katika kukabiliana na matatizo hayo, Serikali imechukua hatua zifuatazo: kubadilisha nguzo zilizoharibika katika njia za umeme wa msongo wa kV 0.4 na ule wa kV 11 na 33; kukata miti katika njia za umeme wa msongo wa kV 11 na 33; kubadilisha vikombe (insulators) vilivyovunjika; na kubadilisha nyaya chakavu.
34. Mheshimiwa Spika, wizi na uharibifu wa miundombinu ya umeme nchini, kwa muda mrefu umekuwa tatizo sugu kutokana na wahusika kubuni njia mbalimbali za kufanya uharibifu huo na kusababishia TANESCO na nchi kwa ujumla hasara kubwa. Mathalani, kwa kipindi cha Julai, 2012 hadi Aprili, 2013 Shirika limepata hasara
ya takriban Shilingi milioni 966.18, sawa na Dola za Marekani 603,862 kutokana na wizi na uharibifu wa miundombinu ya umeme katika Mikoa mbalimbali nchini. Ili kukabiliana na tatizo hili, Wizara kupitia TANESCO imefanya juhudi mbalimbali zikiwemo: kuweka transfoma karibu na maeneo ya makazi ili kuimarisha ulinzi; kutumia transfoma zisizohitaji mafuta; kutumia nyaya za aluminium badala ya shaba; na kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote wanaothibitika kujihusisha na wizi na uharibufu wa miundombinu ya umeme.
Miradi chini ya Ufadhili wa Millenium Challenge Corporation (MCC) ya Marekani
(i) Mradi wa Kujenga Njia za Kusambaza Umeme
35. Mheshimiwa Spika, mradi huu unahusu ujenzi wa njia za msongo wa kV 33, kV 11 na kV 0.4 kwa ajili ya kusambaza umeme katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Manyara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe na Tanga. Ujenzi wa njia za usambazaji za msongo wa kV 33 na kV 11 unaendelea na umefikia kiwango cha asilimia 80, ambapo kilomita 1,068 kati ya kilomita 1,335 zimekamilika. Aidha, ujenzi wa njia ndogo za usambazaji za msongo wa kV 0.4 unaendelea na umefikia kiwango cha asilimia 80, ambapo kilomita 1,094.4 kati ya kilomita 1,368 zimekamilika. Sehemu ya miradi iliyokamilika kwa Mkoa wa Dodoma ilihusisha jumla ya  
vijiji 46 na ilizunduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 11 Aprili, 2013 katika Kijiji cha Mkoka, Wilayani Kongwa. Gharama za mradi zilizotumika kwa Mkoa huo ni Dola za Marekani milioni 17.80, sawa na Shilingi bilioni 28.5. Sehemu iliyobaki ya mradi huo imepangwa kukamilika Mwezi Septemba, 2013. Aidha, ujenzi wa vituo 22 kati ya 24 vya kupozea umeme kV 33/0.4 na kV 11/0.4 unaendelea na utekelezaji wake umefikia asilimia 80. Mradi huu unahusu Mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe na Tanga.
(ii) Ujenzi wa Njia ya Pili ya Umeme kutoka Dar es Salaam kwenda Unguja
36. Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na ujenzi wa njia ya pili ya umeme ya kV 132 kutoka Ubungo hadi Ras-Kilomoni na utandazaji wa nyaya za umeme chini ya bahari kutoka Ras-Kilomoni hadi Mtoni – Unguja. Kazi ya kutandaza nyaya za umeme chini ya bahari ilianza Mwezi Julai, 2012 na ilikamilika na kuzinduliwa rasmi tarehe 10 Aprili, 2013 na Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar. Gharama za mradi huo ni Dola za Marekani milioni 50, sawa na Shilingi bilioni 80.
37. Mheshimiwa Spika, baada ya nchi yetu kukamilisha Awamu ya kwanza ya miradi ya MCC kwa ufanisi mkubwa, naomba kulitaarifu Bunge
lako Tukufu kuwa Tanzania imechaguliwa tena kuendelea kupata ufadhili kutoka MCC katika Awamu ya Pili ambayo itaanza Mwaka 2013/14. Kwa sasa, MCC inaendelea na uchambuzi wa kina wa miradi itakayofadhiliwa ili kujua kiasi halisi cha fedha kitakachotolewa. Maeneo ya kipaumbele katika awamu hiyo ni pamoja na upelekaji wa nishati jadidifu katika shule, zahanati, na vituo vya afya vijijini; ujenzi wa Kituo cha Malagarasi chenye uwezo wa kufua umeme wa MW 42; na ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa kV 132 kati ya Morogoro na Mtibwa.
Mradi wa kufua umeme Malagarasi MW 42
38. Mheshimiwa Spika, moja ya miradi ambayo Serikali iliamua kutekeleza kwa makusudi ili kuondoa kero ya umeme Mkoani Kigoma na Mikoa jirani ni Mradi wa kuzalisha umeme wa Malagarasi. Lengo lilikuwa ni kujenga Kituo cha kufua umeme kwa kutumia nguvu za maji chenye uwezo wa kufua MW 8 (Stage II) katika maporomoko ya Igamba kwenye Mto Malagarasi, Mkoani Kigoma na kujenga njia ya umeme ya msongo wa kV 33 kwenda Wilaya za Kasulu, Kigoma na Uvinza. Mradi huu ni mojawapo ya miradi mikubwa mitatu ya nishati inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC).
39. Mheshimiwa Spika, Maporomoko ya Mto Malagarasi yana maeneo makuu matatu (potential sites) ambayo yanaweza kutumika
kufua umeme. Maeneo hayo ni Malagarasi Stage I, Malagarasi Stage II (ambayo ndiyo yenye maporomoko ya Igamba) na Malagarasi Stage III. Hata hivyo, taarifa ya utafiti ya Mwaka 2004 ilionesha kuwa kuna konokono na samaki adimu (rare species) katika vidimbwi vya maporomoko ya Igamba (Stage II). Taarifa hiyo ilitumiwa katika taarifa ya utafiti wa mazingira ya awali (Preliminary EIA Study) ilifanywa na Kampuni ya Norplan ambayo ilipewa kazi hiyo na TANESCO Mwaka 2008. Taarifa hiyo iliwasilishwa MCC kama sehemu ya mahitaji ya MCC kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. Kutokana na taarifa hiyo, Mwezi Agosti, 2009 MCC ilituma jopo la Wataalam ili kuthibitisha taarifa za kuwepo viumbe hao adimu kabla ya kuanza kazi ya ujenzi wa mitambo ya kufua umeme. Taarifa ya jopo la Wataalam toka MCC ilithibitisha kuwepo kwa konokono na samaki adimu. Kutokana na taarifa hiyo na kwa kuzingatia kanuni za mazingira za kimataifa, Mwezi Novemba, 2009 MCC ilisitisha utekelezaji wa mradi huu.
40. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mradi huu ni kati ya miradi muhimu iliyokuwa imeainishwa katika utekelezaji wa Compact - I, MCC iliona umuhimu wa kuendelea kuufadhili mradi huu na hivyo kukubali kufanya upembuzi yakinifu mpya katika eneo jingine kwenye Mto Malagarasi Stage III. Mbali na kufadhili upembuzi yakinifu katika Malagarasi Stage III, miradi mingine ambayo ilikubaliwa na MCC kutekelezwa katika Mkoa wa Kigoma ni pamoja na mradi wa ukarabati  
na upanuzi wa miundombinu ya kusambazia umeme katika mji mzima wa Kigoma na maeneo yaliyoko jirani na mradi wa umeme utokanao na jua kwa vijiji vya Kasulu, Kigoma na Uvinza.
41. Mheshimiwa Spika, Kampuni ya ESB International ya Ireland ambayo ni Mshauri na msimamizi wa ujenzi wa miradi ya nishati inayofadhiliwa na MCC ilipewa jukumu pia la kufanya uchunguzi upya wa athari za mazingira na jamii na upembuzi yakinifu wa mradi katika Malagarasi Stage III. Katika kutekeleza mradi wa umeme wa Mto Malagarasi, Mshauri vilevile alipewa jukumu la kutayarisha nyaraka za zabuni (Technical Tender Documents). Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa kazi hizi zilikamilika Mwezi Desemba, 2012 na taarifa ya kazi hii inaonesha kuwa, maporomoko hayo yana uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 42.
42. Mheshimiwa Spika, kutokana na ukweli kwamba muda wa utekelezaji wa miradi ya awamu ya kwanza ya ufadhili wa MCC (Compact I) umekwisha na mradi huu hautaweza kutekelezwa, MCC imeridhia kuwa mradi wa ufuaji umeme wa MW 42 utekelezwe katika awamu ya pili ya ufadhili wa MCC (Compact - II).
Miradi chini ya Ufadhili wa JICA, Japan
43. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imekamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 66 kutoka Kiyungi hadi Makuyuni Mkoani
Kilimanjaro chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la JICA. Mradi huo umegharimu Dola za Marekani milioni 26.20, sawa na Shilingi bilioni 41.92 na umekamilika Mwezi Februari, 2013. Kazi nyingine zilizofanyika chini ya mradi huu ni ujenzi wa vituo vya kupozea umeme vyenye uwezo wa MVA 20 katika eneo la KCMC, Kiyungi, Lawate na YMCA Mkoani Kilimanjaro.
Upelekaji wa Umeme Makao Makuu ya Wilaya na Maeneo ya Vijijini
44. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA imeendelea kupeleka umeme katika Makao Makuu ya Wilaya na maeneo ya vijijini. Katika kipindi cha Mwaka 2012/13, upelekaji umeme Makao Makuu ya Wilaya za Namtumbo na Nkasi umekamilika. Mradi wa Namtumbo umegharimu Shilingi bilioni 3.87, sawa na Dola za Marekani milioni 2.42 na mradi wa Nkasi umegharimu Shilingi bilioni 5.58, sawa na Dola za Marekani milioni 3.49. Aidha, Serikali kupitia REA imeendelea kuwezesha utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Awamu ya Kwanza wa Kusambaza Umeme Vijijini katika mikoa 16 ya Tanzania Bara. Gharama za mradi huo ni jumla ya Shilingi bilioni 129, sawa na Dola za Marekani milioni 80.62. Kati ya fedha hizo, takriban Shilingi bilioni 30.0 ni mchango kutoka Serikali ya Sweden. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka 2013/14 badala ya Mwezi Desemba, 2012 kutokana na kuongezwa kwa maeneo mengine
kwenye awamu ya kwanza ya mradi.
45. Mheshimiwa Spika, upelekaji umeme Makao Makuu ya Wilaya ya Nyang’hwale umefikia asilimia 77. Mradi huo ambao unafadhiliwa na MCC utagharimu Shilingi bilioni 4.59, sawa na Dola za Marekani milioni 2.87. Aidha, Mkandarasi wa kupeleka umeme Makao Makuu ya Wilaya za Bukombe na Mbogwe ambaye ni Kampuni ya ELTEL Networks TE AB ya Sweden amepatikana. Kazi hiyo itaanza Mwezi Juni, 2013 na kukamilisha Mwezi Desemba, 2014. Kazi hii ni sehemu ya Mradi wa Electricity V.
46. Mheshimiwa Spika, tathmini ya zabuni za kuwapata wakandarasi wa kutekeleza Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini chini ya REA itakamilika mwishoni mwa Mwezi Mei, 2013. Gharama za utekelezaji wa mradi wa Awamu ya Pili ya Mpango huo zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 881, sawa na Dola za Marekani milioni 550. Aidha, Serikali ya Norway kupitia Shirika lake la Maendeleo (NORAD) itachangia Krona za Norway milioni 700, sawa na takriban Shilingi bilioni 192 katika Mfuko wa Nishati Vijijini. Chini ya mpango huo, umeme utapelekwa katika Makao Makuu ya Wilaya 13 ambazo hazina umeme kwa sasa na baadhi ya maeneo ya vijijini. Wilaya hizo ni Buhigwe, Busega, Chemba, Itilima, Kakonko, Kalambo, Kyerwa, Mkalama, Mlele, Momba, Nanyumbu, Nyasa na Uvinza. Gharama za upelekaji wa umeme katika Wilaya hizo
zinakadiriwa kugharimu Shilingi bilioni 70, sawa na Dola za Marekani milioni 43.75, na kiasi cha fedha kilichobaki cha Shilingi bilioni 122 kitatumika kupeleka umeme vijijini.
Usambazaji Umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara
47. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, mradi wa kusambaza umeme katika Mikoa ya Lindi na Mtwara ulitekelezwa katika maeneo ya Wilaya za Kilwa, Lindi, Masasi, Mtwara Mjini, Nachingwea, Newala, Ruangwa na Tandahimba. Mradi huo unafadhiliwa na Mfuko wa Nishati Vijijini kwa gharama ya Shilingi bilioni 5.0, sawa na Dola za Marekani milioni 3.13. Utekelezaji wa mradi upo katika hatua mbalimbali ambapo katika Mkoa wa Mtwara kilomita 24.78 kati ya 47.53 za njia za usambazaji umeme zimejengwa na transfoma 7 kati ya 24 zimefungwa. Jumla ya wateja 277 wameunganishiwa umeme.
48. Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Lindi, jumla ya kilomita 11.28 kati ya 28.20 za njia ya umeme ya msongo wa kV 33 na kV 11 zimejengwa. Aidha, ujenzi wa kilomita 59.5 kati ya 72.3 za njia ya umeme ya msongo wa kV 0.4 umekamilika na transfoma 5 kati ya 25 zimefungwa. Jumla ya wateja 132 wameunganishiwa umeme. Aidha, wateja katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wataendelea kunufaika kuunganishiwa umeme wa njia moja (single phase) kwa gharama ya Shilingi 99,000 tu ikilinganishwa na kiasi cha  
Shilingi 177,000 wanazotozwa wateja kwenye maeneo mengine ya vijijini nchini kupata huduma hiyo. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa, punguzo hili lilikuwa liishe Mwezi Juni, 2013. Kwa kuzingatia usikivu wa Serikali ya CCM na baada ya kupokea maombi kutoka kwa Viongozi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara, Serikali imekubali punguzo hilo liendelee hadi tarehe 30 Juni, 2014. Tunawaomba wananchi wa Mtwara na Lindi wajitahidi kutumia fursa hii kuhakikisha wanaunganishiwa umeme kwa bei hii nafuu.
Mipango ya Kupunguza Gharama za Kuunganisha Umeme
49. Mheshimiwa Spika, utakumbuka kuwa, katika Hotuba yangu ya Mwaka 2012/13, Serikali iliahidi kupunguza gharama za kuunganisha umeme katika maeneo ya vijijini na mijini ili kuweza kufikisha huduma hiyo kwa wananchi wengi zaidi. Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, ahadi hiyo imetekelezwa kuanzia Mwezi Januari, 2013. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa asilimia 30 ya Watanzania wanaunganishiwa umeme ifikapo mwishoni mwa Mwaka 2014/15.
50. Mheshimiwa Spika, kufuatia punguzo hilo la gharama za kuunganisha umeme, maombi yameongezeka na kufikia wastani wa maombi 15,673 kwa mwezi ikilinganishwa na maombi 11,718 kwa mwezi kabla ya punguzo. Ongezeko  
hilo ni sawa na asilimia 33.8. Kutokana na ongezeko hilo, changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji wa vifaa kama nguzo na mita kwa wakati ili kukidhi mahitaji. Kati ya Mwezi Januari, 2013 hadi Machi 2013, wateja 35,405 wameunganishiwa umeme. Ili kuhakikisha wateja wanaunganishiwa umeme kwa wakati, vifaa muhimu vya kuunganishia wateja umeme vilivyoagizwa na TANESCO kuanzia Mwezi Januari, 2013 ni kama ifuatavyo: nyaya zenye urefu wa kilomita 22,880, nguzo 133,800, mita 265,000 na transfoma 2,100.
51. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu uagizaji wa nguzo za umeme kutoka nje ya nchi, hususan Afrika Kusini, Uganda na Zambia. Hata hivyo, ukweli ni kwamba bei ya nguzo zinazozalishwa na Kampuni za Tanzania ni ghali ikilinganishwa na bei ya nguzo kutoka nchi nyingine. Mfano, bei ya nguzo hapa nchini pamoja na usafiri ni kati ya Shilingi 224,000 hadi Shilingi 749,000 wakati nguzo za Afrika Kusini ni kati ya Dola 138 hadi 420, sawa na kati ya Shilingi 219,000 hadi Shilingi 672,000. Aidha, baadhi ya wasambazaji wa nguzo wa ndani wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea (business as usual). Niwasihi sana wabadilike ili wanapopata kazi, waheshimu mikataba.
52. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Serikali imekamilisha utayarishaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na ujenzi
wa miundombinu ya umeme katika Wilaya za Kilombero (Morogoro) na Mbozi (Mbeya). Kazi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Mfano wa Usambazaji Umeme kwa Gharama Nafuu (Low Cost Design Standards). Gharama za mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia “Sida Trust Fund” zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 10, sawa Shilingi bilioni 16, ambapo takriban wateja 20,000 wataunganishiwa umeme. Utekelezaji wa mradi huu unategemewa kupunguza gharama za usambazaji umeme katika maeneo hayo.

SEKTA NDOGO YA NISHATI JADIDIFU
Uendelezaji wa Nishati Jadidifu (Renewable Energies)
(i) Uendelezaji wa Umeme wa Jua
53. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, ufungaji wa mifumo ya umeme wa jua katika Shule za Sekondari na Zahanati uliendelea ambapo mifumo zaidi ya 150 ilifungwa katika Wilaya za Iramba, Kasulu, Kibondo, Mkuranga, Mpanda, Muleba, Nyang’wale, Nzega, Rufiji na Sumbawanga. Sehemu ya Mradi huo (off grid component) unagharimiwa na Serikali kwa jumla ya Shilingi bilioni 2, sawa na Dola za Marekani milioni 1.25 pamoja na ufadhili wa Benki ya Dunia chini ya Mradi wa Tanzania Energy Development and Access Expansion Project (TEDAP) kwa gharama ya Dola za Marekani
milioni 22.5, sawa na Shilingi bilioni 36. Mradi huo utakamilika Mwaka 2014/15.
54. Mheshimiwa Spika, mradi mwingine wa umeme wa jua umeanza kutekelezwa na Kampuni ya Solawazi katika Wilaya ya Kigoma. Mradi huo utakaogharimu Dola za Marekani milioni 12, sawa na Shilingi bilioni 19.20 kwa kuanzia utawezesha kufua umeme wa MW 3 utakaoingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Kampuni hiyo imeingia Mkataba wa kuuziana umeme na TANESCO Mwezi Januari, 2013 chini ya utaratibu wa Mikataba Maalum (Standardized Small Power Purchase Agreement and Tariff – SSPA/T).
(ii) Uendelezaji wa Vyanzo vya Nishati ya Upepo
55. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, Kampuni ya Geo-Wind Power (T) Ltd kupitia Wizara ya Fedha imepeleka maombi ya mkopo Benki ya Exim ya China. Mradi huo unamilikiwa kwa ubia kati ya Power Pool East Africa Ltd, TANESCO na NDC. Mgawanyo wa hisa utajulikana baada ya majadiliano kukamilika Mwezi Julai, 2013. Gharama za mradi wenye uwezo wa kufua MW 50 ni Dola za Marekani milioni 136, sawa na Shilingi bilioni 217.60. Aidha, TANESCO imekamilisha taratibu za kumpata Mtaalam Mshauri (Technical Advisor) kwa ajili ya mradi wa kufua MW 100 unaotekelezwa na Kampuni ya Wind East Africa Limited kwa gharama za Dola za
Marekani milioni 285, sawa na Shilingi bilioni 456. Kampuni hiyo inamilikiwa na M/S Six Telecoms (asilimia 40), M/S Aldwych (asilimia 40), na M/S IFC (asilimia 20). Kampuni hizo zimepatiwa leseni za muda (provisional licence) na EWURA kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Miradi hiyo miwili itatekelezwa katika eneo la Kititimo, Mkoani Singida.
(iii) Uendelezaji wa Umeme Utokanao na Maporomoko Madogo ya Maji
56. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za Serikali kuwezesha sekta binafsi, mradi wa kuzalisha umeme kutokana na maporomoko madogo ya maji ya Mwenga, Mkoani Iringa wa MW 4 umewezeshwa kwa kupatiwa ruzuku ya Dola za Marekani 500, sawa na Shilingi 800,000 kwa kila kaya itakayounganishiwa umeme. Hadi Mwezi Aprili 2013, jumla ya wateja 465 waliunganishiwa umeme kati ya wateja 2,600 wanaotarajiwa kuunganishiwa, hivyo kupata ruzuku ya Dola za Marekani 232,500 sawa na Shilingi milioni 372.
(iv) Uendelezaji wa Tungamotaka (Biomass)
57. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, uhamasishaji wa matumizi bora ya tungamotaka (mkaa wa kuni na biogas) ulifanyika, ambapo mtambo wenye uwezo wa kufua umeme wa kW 24 kwa kutumia biogas ulifungwa katika Kijiji cha Manyata, Wilaya ya Kongwa.30
58. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Kituo cha Uendelezaji wa Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) iliendelea na utekelezaji wa Mradi wa Biogas for Better Life African Initiatives chini ya mpango ujulikanao kama Tanzania Domestic Biogas Program, kwa ajili ya kujenga mitambo ya biogas kwa ngazi ya kaya kupitia ufadhili wa HIVOS ya Uholanzi. Kwa kipindi cha Mwezi Januari, 2012 mpaka Desemba, 2012 mitambo 2,409 ilijengwa katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Ruvuma, Shinyanga na Singida. Mitambo mingine 12 imejengwa Zanzibar. Lengo la mradi huu ni kujenga mitambo 12,000 nchini ifikapo Desemba, 2014. Vilevile, kupitia REA, mitambo mingine ya biogas inajengwa Masasi (Gereza la Namajani) na Songea Vijijini (Kambi ya JKT Mlale).
59. Mheshimiwa Spika, sambamba na uendelezaji wa biogas, mafunzo kwa ajili kuwajengea uwezo Watanzania katika matumizi ya teknolojia hiyo yalitolewa katika maeneo ya Bukombe, Kasulu na Songea. Jumla ya Watanzania walionufaika na mafunzo hayo katika Mwaka 2012/13 ni 2,400.
(v) Uendelezaji wa Jotoardhi (Geothermal)
60. Mheshimiwa Spika, Mwezi Januari, 2013 NDC kwa kushirikiana na Kampuni za “Geothermal Power Tanzania Limited” na “Interstate Mining
Company” za Tanzania zilianza kuchoronga visima vifupi na virefu vya utafiti katika maeneo ya Mbaka na Ziwa Ngozi – Mbeya kwa ajili ya uhakiki wa uwezo wa kufua umeme kutokana na jotoardhi. Serikali pia, kwa kushirikiana na Taasisi ya Jiolojia ya Ujerumani (BGR) imeainisha maeneo katika vijiji vya Uyole na Wasanga Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuchoronga visima vifupi vitatu vyenye kina cha mita 400 kila kimoja. Taarifa za tafiti hizo zitawezesha nchi kuangalia uwezekano wa kufua umeme kutokana na jotoardhi. Gharama za kuchoronga kisima kimoja ni kati ya Dola za Marekani 400,000, sawa na Shilingi milioni 640 hadi Dola za Marekani milioni 1, sawa na Shilingi bilioni 1.6.
Matumizi Bora ya Nishati
61. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wilaya 10 zilibainishwa kwa ajili ya kutekeleza mradi wa mfano wa matumizi bora ya nishati chini ya Mradi wa Low Carbon Energy Efficiency & Climate Change Mitigation. Wilaya hizo ni Geita, Kasulu, Kahama, Kwimba, Mbinga, Mbulu, Misenyi, Mpanda, Ngorongoro na Urambo. Lengo la mradi ni kuhamasisha matumizi endelevu ya nishati na kupunguza hewa ukaa (carbon dioxide). Mradi huu utagharimiwa na Serikali pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 16, sawa na Shilingi bilioni 25.60.

SEKTA NDOGO ZA GESI ASILIA NA MAFUTA
Kuongeza na Kuboresha Miundombinu ya Gesi Asilia
(i) Miundombinu ya Gesi Asilia iliyopo
62. Mheshimiwa Spika, kwa sasa, uwezo wa mitambo ya kusafisha gesi asilia iliyopo ni futi za ujazo milioni 70 kwa siku (mmscfd). Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya gesi asilia, ililazimu kuongezwa (re-rating) kwa uwezo wa mitambo hiyo na kufikia futi za ujazo milioni 103. Ikumbukwe kuwa, gesi asilia hivi sasa inasafirishwa na bomba lenye urefu wa kilomita 225 na kipenyo cha inchi 16 kutoka Songo Songo hadi Dar es Salaam ambapo asilimia 80 ya gesi hiyo hutumika kufua umeme na kiasi kinachobaki cha asilimia 20 hutumika kwenye baadhi ya viwanda na taasisi.
63. Mheshimiwa Spika, umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia unafikia wastani wa MW 330 ikilinganishwa na uwezo wa mitambo iliyopo yenye jumla ya MW 501. Uwezo huo haufikiwi kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu ya kutosha ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia. Ili kukidhi mahitaji ya umeme, Serikali imelazimika kutumia mafuta kufua umeme ambayo ni ghali ikilinganishwa na vyanzo vingine. Mafuta hayo yanaigharimu Serikali takriban Shilingi bilioni 5 kwa siku, sawa na
Dola za Marekani bilioni 1 kwa mwaka. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inajenga miundombinu mipya ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia.
(ii) Mradi wa Bomba la Kusafirisha Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam
64. Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam ulizinduliwa rasmi tarehe 08 Novemba, 2012 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Mradi huo unahusisha ujenzi wa Bomba lenye urefu wa kilomita 532 na kipenyo cha inchi 36. Pia, bomba hilo lina uwezo wa kusafirisha futi za ujazo za gesi asilia milioni 784 kwa siku. Mradi huo pia utahusisha mitambo miwili ya kusafisha gesi asilia katika maeneo ya Mnazi Bay -Madimba (Mtwara) na Kisiwa cha Songo Songo (Lindi). Mradi utagharimu Dola za Marekani milioni 1,225.3, sawa na Shilingi bilioni 1,960. Kazi za usanifu wa mradi na ulipaji fidia kwa wananchi wapatao 3,092 waliopisha maeneo ya mradi zimekamilika. Aidha, hatua za awali za ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi asilia zimeanza. Hadi sasa visima viwili vya maji vyenye uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 50 kwa saa kwa kila kimoja vimekamilika. Visima hivyo, ni kwa ajili ya mitambo ya kusafisha gesi asilia katika eneo la Madimba na kwa matumizi ya wananchi. Vifaa mbalimbali vya ujenzi wa 34
nyumba za wafanyakazi wa mradi vimewasili nchini mwishoni mwa Mwezi Aprili, 2013.
65. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa miundombinu hii utaleta manufaa makubwa kwa Taifa. Hadi sasa Mikoa ya Lindi na Mtwara imepata manufaa mbalimbali yatokanayo na miradi ya gesi asilia ikiwa ni pamoja: tozo ya asilimia 0.3 ya mauzo ya gesi asilia, huduma za jamii kama zahanati, shule, umeme, maji na ufadhili wa mafunzo katika vyuo vya ufundi (VETA) na Sekondari. Manufaa mengine yatakayopatikana ni pamoja na: ujenzi wa viwanda mbalimbali vikiwemo kiwanda cha Saruji cha Kampuni ya Dangote ambacho ujenzi wake umeanza, kiwanda cha mbolea, mtambo wa kufua umeme wa MW 400 kupitia Kampuni ya Symbion pamoja na ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme ya msongo wa kV 220 kutoka Mtwara hadi Songea. Aidha, Kampuni ya Schlumberger ya Houston, Marekani imejenga karakana kubwa Mtwara ambayo itakuwa inatengeneza vifaa vya uchimbaji, utafutaji na uendelezaji wa rasilimali za mafuta na gesi badala ya kupeleka nje ya nchi.
66. Mheshimiwa Spika, taratibu za kupata umiliki wa maeneo ya ujenzi wa viwanda (Industrial Park) vyenye kutumia gesi asilia zinaendelea katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Ujenzi wa viwanda hivyo utaongeza fursa za ajira kwa Watanzania pamoja na mapato kwa Serikali.
(iii) Usambazaji wa Gesi Asilia Jijini Dar es Salaam
67. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa bomba la gesi asilia lenye kipenyo cha inch 12 na urefu wa kilomita 6.3 kutoka Ubungo hadi Mikocheni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusambaza gesi asilia majumbani na viwandani umekamilika. Bomba hili linahudumia wateja wa viwanda waliokuwa wakipata gesi kwa njia ya gesi iliyoshindiliwa ya mitungi (Compressed Natural Gas – CNG) pamoja na nyumba 70 zilizopo eneo la Mikocheni. Mradi huu umegharimu Dola za Marekani milioni 3.13, sawa na Shilingi bilioni 5.
68. Mheshimiwa Spika, kwa kuwa miundombinu iliyopo sasa ya kuleta gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam haitoshelezi, uunganishwaji wa wateja wapya utaanza baada ya kukamilika kwa bomba la gesi asilia linalojengwa na Serikali kutoka Lindi na Mtwara hadi Dar es Salaam. Katika kuendeleza mradi huo, Serikali kupitia TPDC imemwajiri Mshauri atakayefanya kazi ya kusanifu michoro ya ujenzi ya mtandao wa kusambaza gesi asilia na vituo vya kujazia gesi hiyo kwenye magari katika Jiji la Dar es Salaam. Vilevile, Mshauri huyo atasimamia upatikanaji wa Mkandarasi atakayejenga mtandao huo. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 80, sawa na Dola za Marekani milioni 50.
Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia  
69. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Kampuni za utafutaji mafuta ziliendelea kutekeleza mipango kazi kama ilivyoainishwa kwenye mikataba yao. Katika kipindi hicho, Kampuni za BG/Ophir na Statoil/ExxonMobil zilifanikiwa kuchoronga visima vinne (Zafarani – 2, Lavani – 2, Tangawizi na Jodari North) kwenye kina kirefu cha maji baharini ili kutathmini kiasi cha gesi asilia kilichopo. Kisima cha Tangawizi kimegundulika kuwa na kiasi cha futi za ujazo kati ya trilioni 4 hadi 6 wakati kisima cha Jodari kimegundulika kuwa na futi za ujazo trilioni 4.1 badala ya futi za ujazo trilioni 3.4 zilizotangazwa awali. Aidha, kisima cha Zafarani – 2 kimegundulika kuwa na futi za ujazo trilioni 6, wakati kisima cha Lavarani – 2 kimegundulika kuwa na futi za ujazo trilioni 4.7. Hadi sasa kiasi cha gesi asilia kilichogundulika nchini ni takriban futi za ujazo trilioni 41.7.
Upitiaji wa Mikataba ya Utafutaji na Ugawanaji wa Mapato
70. Mheshimiwa Spika, kazi ya kudurusu mikataba ya utafutaji na ugawanaji wa mapato (Production Sharing Agreements – PSAs) ilikamilika mwishoni mwa Mwezi Novemba, 2012. Kukamilika kwa kazi hiyo kumeiwezesha Serikali kubaini maeneo yanayohitaji kuboreshwa katika mikataba hiyo. Pia, matokeo ya uchambuzi wa mikataba hiyo yatasaidia katika uandaaji wa sera, sheria na kanuni za usimamizi wa sekta ndogo za mafuta na gesi asilia itakayokidhi matakwa ya Watanzania.
Usimamizi wa Biashara ya Mafuta
71. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA iliendelea kusimamia usambazaji wa mafuta ili kuhakikisha kuwa yanapatikana wakati wote na maeneo yote nchini. Hadi Mwezi Aprili, 2013 kulikuwa na wafanyabiashara wakubwa (wholesalers) 88 na wafanyabiashara wa rejareja 867. Katika Mwaka 2012/13 hadi kufikia Aprili, 2013, kiasi cha lita za ujazo bilioni 2.30 za nishati ya mafuta ziliingizwa nchini kwa ajili ya soko la ndani yenye thamani ya takriban Dola za Marekani bilioni 1.68, sawa na Shilingi bilioni 2,688. Kiasi hiki ni sawa na ongezeko la lita milioni 303.41, sawa na asilimia 13.20 ikilinganishwa na mafuta yote yaliyoagizwa Mwaka 2011/12. Kati ya kiasi hicho cha mafuta, lita 1,405,711,203 zilikuwa dizeli, sawa na asilimia 61 ya mafuta yote yaliyoingizwa nchini; petroli lita 562,368,954, sawa na asilimia 24; na mafuta ya taa lita 230,708,012, sawa na asilimia 10. Bidhaa nyinginezo za mafuta ilikuwa ni asilimia 5 ya mafuta yote. Aidha, katika kipindi hicho lita za ujazo bilioni 1.36 za mafuta yaliagizwa na nchi jirani kupitia Bandari ya Dar es Salaam, hii ni sawa na asilimia 37.16 ya mafuta yote yaliyoagizwa Mwaka 2012/13.
72. Mheshimiwa Spika, uagizaji wa mafuta kwa pamoja umeendelea kufanyika chini ya Kampuni ya uratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (Petroleum Importation Coordinator - PIC). Aidha, Mwezi Novemba, 2012, Serikali kupitia Mamlaka
ya Bandari Tanzania (TPA) ilizindua boya jipya la kupakulia mafuta, Single Point Mooring (SPM). Kuzinduliwa kwa boya hilo kumeongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam wa kupokea meli za mafuta ya dizeli kutoka uzito wa tani 36,000 hadi tani 95,000 kwa wakati mmoja, sawa na ongezeko la asilimia 163.9.
73. Mheshimiwa Spika, Mwezi Novemba, 2012 Kampuni ya Addax Energy SA ya Uswisi iliyoshinda zabuni ya kuagiza mafuta kwa pamoja iliagiza mafuta kiasi cha tani laki 1 za dizeli. Hata hivyo, mafuta hayo yaligundulika kuwa chini ya viwango vinavyotakiwa kwa Tanzania. Mafuta hayo yalikuwa na thamani ya takribani Dola za Marekani milioni 96.7, sawa na Shilingi bilioni 154.72. Serikali kupitia Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) na Kampuni ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PIC) ilifanikiwa kuzuia mafuta hayo kuingia nchini. Kufuatia tukio hilo, Kampuni hiyo ililipa faini ya takribani Dola za Marekani milioni 1.24, sawa na Shilingi bilioni 1.98 na kufungiwa kushiriki katika shughuli za uagizaji mafuta nchini kwa kipindi cha miezi minne (4). Naamini hatua hii itakuwa ni fundisho kwa Kampuni yoyote isiyofuata taratibu na inayofikiria kuleta mafuta yasiyokidhi viwango nchini mwetu.
74. Mheshimiwa Spika, baada ya Serikali kuanza kutafuta mbia kwa ajili ya uanzishwaji wa Hifadhi ya Mafuta ya Taifa (National Strategic Petroleum Reserve), kampuni nyingi za nje na ndani ya nchi
zilionesha nia ya kushiriki. Ili kupata mshiriki kwa njia ya ushindani na atakayeleta tija kwa Taifa, Serikali ilitangaza zabuni Mwezi Machi, 2013 ambapo Kampuni 23 zilijitokeza kuomba kushirikiana na TPDC. Pamoja na Kampuni hizo kujitokeza, Kampuni zilizorudisha zabuni zilikuwa 10. Ufunguzi wa zabuni hii ulikuwa tarehe 29 Aprili, 2013 na Timu ya Uchambuzi inaendelea na kazi yake ili kupata Kampuni inayofaa kushirikiana na TPDC. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Wizara ya Fedha, EWURA, PIC, TPDC na TRA inaandaa kanuni za kusimamia mfumo huo kwa mujibu wa Sheria.
75. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia EWURA imeendelea kudhibiti ubora wa mafuta nchini. Katika kipindi cha Julai, 2012 hadi Machi, 2013, jumla ya vituo vya mafuta 146 kati ya vituo 900 vilivyopo nchini vimekaguliwa. Vituo 18 kati ya hivyo havikukidhi viwango vya ubora na vilichukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria. Hatua za kisheria zilizochukuliwa ni pamoja na kufungiwa kuendesha biashara hiyo kwa kipindi maalum na kutozwa faini.
76. Mheshimiwa Spika, EWURA pia imeendelea kupanga na kusimamia bei kikomo kwa bidhaa za mafuta kwa mujibu wa Sheria ya EWURA ya Mwaka 2001 na Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2008. Kutokana na udhibiti huo, jumla ya vituo 20 vya mafuta vilitozwa faini kwa kukiuka Taratibu za Upangaji Bei (Price Setting Rules, 2009). Vituo
16 kati ya hivyo vilikuwa vikiuza mafuta zaidi ya bei kikomo na vituo vinne (4) havikuwa na matangazo ya bei.
Bei za Mafuta
77. Mheshimiwa Spika, bei za mafuta katika Soko la Dunia kwa Mwaka 2012 zilikuwa zikipanda na kushuka. Kiwango cha juu cha bei kilikuwa katika Mwezi Machi, 2012 ambapo mafuta ya dizeli yaliuzwa kwa Dola za Marekani 1,010 kwa tani na mafuta ya taa na ndege yaliuzwa kwa Dola za Marekani 1,071 kwa tani. Aidha, kiwango cha juu cha bei ya mafuta ya petroli kilikuwa Dola za Marekani 1,150 kwa tani katika Mwezi Aprili, 2012. Kwa wastani, katika Mwaka 2012, bei za mafuta katika Soko la Dunia zilikuwa juu kwa asilimia 3.9 kwa mafuta ya petroli; asilimia 0.2 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 2.7 kwa mafuta ya taa na mafuta ya ndege ikilinganishwa na bei za Mwaka 2011.
78. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Serikali kupitia Wizara imeendelea kushiriki katika shughuli za uendeshaji wa Kampuni za “Puma Energy Limited” ambapo Serikali ina hisa asilimia 50; Tanzania - Zambia Pipeline Limited (TAZAMA) ambapo Serikali pia ina hisa asilimia 30; na Tanzania International Petroleum Reserve (TIPER) ambapo ina hisa asilimia 50. Kampuni hizo zinaendelea kufanya vizuri kifedha na Serikali inategemea kupata gawio wakati wowote kazi za uhakiki wa hesabu za fedha zitakapokamilika Julai, 2013.


KUANDAA SERA, SHERIA NA MIPANGO KWA AJILI YA KUSIMAMIA SEKTA YA NISHATI
79. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wizara yangu imekamilisha Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia. Maandalizi ya Rasimu hiyo yalishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo: Wizara na Taasisi za Serikali; Waheshimiwa Wabunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini; Kampuni za utafutaji wa mafuta na gesi asilia; Washirika wa Maendeleo; Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola; Wanataaluma wa Vyuo Vikuu nchini; Community Based Organization (CBOs); Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), vyombo vya habari na wananchi katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kigoma, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Rukwa na Tanga. Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia imewasilishwa katika ngazi husika za Serikali. Sambamba na Sera hiyo, Mkakati wa Utekelezaji wake (Natural Gas Implementation Strategy) uliandaliwa.
80. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Mpango Kabambe wa Uendelezaji wa Sekta ya Umeme (PSMP) ulipitiwa upya kwa kushirikisha wadau, hususan Wizara na Taasisi za Serikali, Washirika wa Maendeleo na Sekta Binafsi. Aidha, Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja - The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2013 ziliandaliwa na kutangazwa kupitia Tangazo la Serikali Na. 59072013 la tarehe 15 Machi, 2013.  
Mafanikio Yaliyopatikana katika Sekta ya Nishati
81. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza kazi zilizopangwa kwa Mwaka 2012/13, mafaniko yaliyopatikana katika Sekta ya Nishati ni pamoja na: kuongezeka kwa idadi ya Watanzania waliunganishiwa umeme kutoka asilimia 18.4 (Mwaka 2012) hadi asilimia 21 (Aprili, 2013) ambapo kwa upande wa vijijini idadi ya Watanzania waliounganishiwa umeme imefikia asilimia 7; kuzinduliwa na kuanza kutekelezwa kwa mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mnazi Bay (Mtwara) na Songo Songo (Lindi) hadi Dar es Salaam; kukamilika kwa ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mkuza wa bomba la gesi; kukamilika kwa Mradi wa Ujenzi wa Bomba dogo la Gesi Asilia kutoka Ubungo hadi Mikocheni Jijini Dar es Salaam; kukamilika kwa Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia; na kuondoa makali ya upungufu wa umeme nchini.
82. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine katika Sekta ya Nishati ni yafuatayo: kutekelezwa kwa ahadi ya kupunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wateja; kukamilika kwa Mradi wa Mwenga MW 4 (Iringa) wa ufuaji umeme kutokana na maporomoko madogo ya maji; kukamilika kwa upelekaji umeme katika Makao Makuu ya Wilaya za Namtumbo na Nkasi; kupatiwa mafunzo kwa wajasiriamali 178 kuhusu nishati jadidifu; kukamilika kwa ufungaji wa mifumo ya umeme wa jua katika maeneo mbalimbali
nchini; na kukamilika kwa shindano la Lighting Rural Tanzania 2012 ambapo jumla ya Shilingi bilioni 2.17, sawa na Dola za Marekani milioni 1.36 zilitolewa kwa miradi 15 iliyoshinda katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Kigoma, Manyara, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani na Shinyanga ambapo miradi 7 ipo katika Mkoa wa Dar es Salaam na mradi mmoja mmoja kwa kila mkoa.
Changamoto katika Sekta ya Nishati
83. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo, Wizara katika Mwaka 2012/13 imekabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo: kudhibiti upotevu wa umeme; kuwa na mbadala wa kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia majumbani; kufikisha umeme vijijini; kukidhi ongezeko la mahitaji ya nishati nchini, hususan umeme; kuongeza wigo wa rasilimali au vyanzo vya kuzalisha umeme; kukidhi matarajio ya wananchi kuhusu manufaa yatokanayo na gesi asilia; kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Nishati; mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameathiri ufuaji wa umeme kutokana na maji; na uzalishaji wa umeme wa uhakika na wa kutosheleza ambao kwa kiasi kikubwa umetegemea zaidi mafuta mazito na dizeli ambayo ni ghali.
84. Mheshimiwa Spika, utakumbuka kuwa mnamo Mwezi Desemba, 2012 kulifanyika maandamano ya wananchi wa Mtwara wakitaka kujua faida ya kugunduliwa gesi asilia katika Mikoa ya Kusini.  
Utashi wa wananchi ndio wa Serikali. Kama nilivyoelezea kwenye Hotuba yangu, manufaa yatokanayo na uvunaji wa gesi asilia ni mengi. Hivyo, Serikali makini na sikivu imesikia, imeelewa na sasa inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kuhusu manufaa hayo. Hata hivyo, ni muhimu ikaeleweka kuwa maandamano ya aina hiyo yanarudisha nyuma utekelezaji wa mipango ya Serikali inayolenga kuleta maendeleo ya wananchi na Taifa letu kwa ujumla. Hivyo, yakiendelea yanaweza kuwafukuza wawekezaji kwa kuhofia maisha yao, mali zao na mitaji yao. Umeme wa uhakika ni uchumi wa uhakika. Ndugu zetu wa Mtwara wasizuie ndugu zao wa Tanzania kupata umeme wa uhakika kwa uchumi wa uhakika.
SEKTA YA MADINI
Mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa
85. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wizara imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kukuza shughuli za utafutaji, uchimbaji na biashara ya madini nchini. Pia, Wizara iliimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini ili kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa. Kiwango cha ukuaji wa shughuli za kiuchumi za uchimbaji madini kilifikia asilimia 7.8 katika Mwaka 2012 ikilinganishwa na asilimia 2.2 Mwaka 2011. Aidha, mchango katika Pato la Taifa ulifikia asilimia 3.5 ikilinganishwa na asilimia
3.3 kwa Mwaka 2011 kwa bei ya Mwaka 2012.
86. Mheshimiwa Spika, thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi iliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.98, sawa na Shilingi bilioni 3,168.32 Mwaka 2011 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.30, sawa na Shilingi bilioni 3,684.05 Mwaka 2012. Ongezeko hili la asilimia 16.3, lilitokana na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la Dunia kutoka wastani wa Dola za Marekani 1,571.28 kwa wakia Mwaka 2011 hadi kufikia wastani wa Dola za Marekani 1,668.63 kwa wakia Mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi imeendelea kuchangiwa kwa kiwango kikubwa na madini ya dhahabu ambapo mchango wake kwa Mwaka 2012 ni takriban asilimia 94.
Utekelezaji wa Shughuli Zilizopangwa katika Mwaka 2012/13
87. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, maeneo yaliyopewa kipaumbele katika Sekta ya Madini ni kuboresha utoaji na usimamizi wa leseni za madini; kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini; kuhamasisha uongezaji thamani madini; kuimarisha soko la madini ya vito; kuimarisha usalama, afya na utunzaji wa mazingira migodini; kukamilisha maandalizi ya kudurusu Sheria ya Baruti; kuwezesha utekelezaji wa shughuli za Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI); kuongeza fungamanisho la Sekta ya Madini na sekta nyingine za uchumi;  
ujenzi na uboreshaji wa ofisi za madini; na kuziwezesha Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Kuboresha Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini
88. Mheshimiwa Spika, katika hatua za kuboresha utoaji na usimamizi wa leseni, Mfumo wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini uliendelea kuimarishwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha ofisi za madini za Kanda zilizoko mikoani katika Mkongo wa Mawasiliano wa Taifa. Maboresho ya mfumo huo yamewezesha leseni 4,996 kutolewa na maombi 21,390 kukataliwa katika kipindi cha Julai, 2012 hadi mwishoni mwa Mwezi Aprili, 2013, na hivyo kufanya maombi yaliyoshughulikiwa kufikia 26,386. Aidha, maombi ya zamani yaliyokuwepo (backlogs) ilipofika tarehe 01 Julai, 2012 yalikuwa ni 28,333 na maombi mapya yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2013 ni 9,889 na hivyo kufanya maombi yaliyobaki kufikia 11,836 ikilinganishwa na maombi 28,333 yaliyokuwepo mwisho wa Mwaka 2011/12.
89. Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiweka juhudi za kutoa leseni kwa wachimbaji wadogo ambapo hadi sasa kuna jumla ya leseni hai za wachimbaji wadogo 17,040. Hata hivyo, leseni 8,570 zinazomilikiwa na wachimbaji hao hazijalipiwa ada ya mwaka ya jumla ya Shilingi bilioni 2.66 tangu Mwaka 2010 hadi 2012.
Kwa ujumla deni la ada za mwaka wanalodaiwa wachimbaji wadogo limefikia Shilingi bilioni 4.17 hadi kufikia Aprili, 2013. Aidha, mrabaha uliolipwa na wachimbaji wadogo katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2010 hadi 2012 ni Shilingi bilioni 2.11, kiwango ambacho ni kidogo sana kwa kuwa wengi wao hawawasilishi takwimu na wanaowasilisha hawaoneshi takwimu sahihi kwa nia ya kukwepa kulipa mrabaha na kodi nyingine za Serikali. Nitoe agizo kwa wachimbaji wadogo wote kuhakikisha kwamba wanalipa madeni ya ada ya mwaka ya leseni zao na wanawasilisha taarifa sahihi za uzalishaji na mauzo ya madini kwa ajili ya malipo ya mrabaha. Watakaoshindwa kutekeleza agizo hili, Wizara yangu haitasita kufuta leseni zao.
90. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoahidi katika Hotuba yangu ya Mwaka 2012/13, kwamba tutafuta leseni za madini ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi kwa muda mrefu. Nachukua fursa hii kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba hadi Mwezi Aprili, 2013 jumla ya leseni 160 za utafutaji, moja (1) ya uchimbaji wa kati na 268 za uchimbaji mdogo zimefutwa. Maeneo ya leseni hizo yatatolewa kwa waombaji wapya, hususan wachimbaji wadogo kwa mujibu wa Sheria. Zoezi hili ni endelevu ili kuhakikisha kuwa leseni zote zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
91. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa kuna usalama wa nyaraka muhimu za leseni za madini, Mfumo wa Data Recovery System (back up) ulianzishwa. Mfumo huu utatumika endapo patatokea hitilafu katika mfumo mama (main system) uliopo Makao Makuu ya Wizara.
Kuendeleza Uchimbaji Mdogo wa Madini
92. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza uchimbaji mdogo kwa Mwaka 2012/13, Wizara yangu iliahidi kutenga jumla ya maeneo 10 yenye ukubwa wa hekta 105,163 kwa ajili ya uchimbaji mdogo. Maeneo yaliyotengwa rasmi hadi sasa ni 16 yenye jumla ya hekta 265,396, ikiwa ni asilimia 160 ya lengo, zinazoweza kutolewa leseni takribani 26,539 za uchimbaji mdogo zenye ukubwa wa hekta 10 kila moja. Maeneo hayo na Wilaya husika ni Kakonko (Nyamwironge – Nyamtukuza); Kibaha (Kwamfipa na Viziwaziwa); Misungwi (Mihama); Mkuranga (Langweni-Mwanadilatu na Vianzi-Mindevu); Morogoro (Dete – Mwalazi); Mpwapwa (Winza); Mvomero (Melela); Same (Makanya); Simanjiro (Mwajanga); Singida (Mpambaa); Tarime (Nyakunguru na Nyamwaga); Tunduru (Mbesa); na Uvinza (Ilagala). Leseni za uchimbaji mdogo zinaendelea kutolewa kwenye maeneo hayo kwa mujibu wa Sheria. Aidha, taratibu za kisheria zinatarajia kukamilishwa kabla ya Julai, 2013 za kuwezesha kutengwa maeneo mengine ya Ibaga (Mkalama), Isenyela (Chunya), Kapalamsenga (Mpanda) na Songwe (Mbeya Vijijini).
93. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012/13, Serikali ilitenga jumla ya Shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya kutoa mikopo ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata vifaa na mitaji kwa ajili ya kufanya kazi zao kwa ufanisi. Ili kuhakikisha mikopo hiyo inanufaisha walengwa na inarejeshwa kwa wakati na wakopaji, Wizara iliamua kutoa mikopo hiyo kupitia mfumo wa kibenki. Hivyo, zabuni ya kupata benki itakayosimamia kazi hiyo ilitangazwa Mwezi Februari, 2013 na mshindi amepatikana ambaye ni Benki ya TIB. Taratibu za kuhamisha fedha hizo na utoaji wa mikopo zitakamilishwa kabla ya Julai, 2013.
94. Mheshimiwa Spika, jukumu la kuwaendeleza wachimbaji wadogo limekabidhiwa kwa STAMICO. Katika kutekeleza jukumu hili, Mpango Kazi na Programu ya Mafunzo kwa wachimbaji wadogo iliandaliwa na kuanza kutekelezwa ambapo mafunzo katika baadhi ya maeneo nchini yalitolewa. Mafunzo hayo yalishirikisha Wakufunzi kutoka Wizara ya Nishati na Madini; Wakala wa Jiolojia; Wakala wa Ukaguzi wa Madini; SIDO; Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; na Chuo cha Madini Dodoma. Jumla ya washiriki 797 walihudhuria mafunzo yaliyoendeshwa katika maeneo ya Geita (Geita na Rwamgasa), Kigoma (Ilagala), Lindi (Ruangwa), Shinyanga (Shinyanga Mjini na Kahama) na Singida (Londoni). Pia, mafunzo hayo yalishirikisha Viongozi wa Serikali na watoa huduma katika maeneo ya uchimbaji. Mafunzo hayo yalilenga kutoa elimu ya nadharia na kwa  
vitendo juu ya utafutaji wa madini, uchimbaji, uchenjuaji, elimu ya biashara, ujasiriamali na utunzaji wa mazingira pamoja na masuala mtambuka.
95. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendesha mkutano wa pili wa kitaifa tarehe 6 hadi 7 Desemba, 2012 hapa Dodoma. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa wachimbaji wadogo kutoka mikoa yote nchini na ulilenga kusikiliza changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini na kuweka mikakati ya kuitatua, pamoja na kuimarisha vyama vyao vya kimkoa (REMAs) na kitaifa. Jumla ya wachimbaji wadogo 185 waliowawakilisha wenzao kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara walihudhuria. Kupitia maazimio ya mkutano huo, REMAs zimeundwa katika mikoa yote, Viongozi wa mpito wa kitaifa wamechaguliwa; Mpango Kazi wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo ulijadiliwa na kupitishwa; na takwimu na taarifa muhimu za wachimbaji wadogo zilikusanywa kote nchini kwa lengo la kuwatambua, kubainisha changamoto zinazowakabili na kujenga kanzidata (database).
96. Mheshimiwa Spika, pamoja na ukuaji wa kasi wa sekta ndogo ya uchimbaji madini, wachimbaji wadogo wengi hawatunzi kumbukumbu za mapato na matumizi na hawalipi kodi na mrabaha stahiki. Hali hii imekuwa ikiikosesha Serikali kiasi kikubwa cha mapato. Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa wachimbaji wadogo wanatunza kumbukumbu sahihi za
uchimbaji na mauzo ya madini, pamoja na kulipa kodi na mrabaha stahiki. Aidha, taarifa hizo zitawasaidia wakati wa kuwapa mikopo ili kuboresha shughuli zao.
97. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Madini imeendelea kukumbwa na migogoro ya mipaka ya leseni za madini. Migogoro hiyo imekuwa ikihusisha wachimbaji wadogo wenyewe kwa wenyewe na kati yao na wachimbaji wakubwa. Wizara imeendelea kusuluhisha migogoro ya aina hiyo kwa mujibu wa Sheria. Pia, uimarishaji wa Mfumo wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni umesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya mipaka ya leseni za madini kwani leseni zinatolewa kwa kuzingatia kanuni ya aliyewahi kuomba kupatiwa leseni kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010. Wizara yangu imeendelea kuwachukulia hatua watumishi wote wanaosababisha migogoro ya aina hiyo kwa uzembe, kukiuka Sheria na taratibu zilizopo au kupokea rushwa. Changamoto kubwa inayoikabili Sekta kwa sasa ni uvamizi unaofanywa na wachimbaji wadogo kwenye maeneo yenye leseni za utafiti mkubwa wa madini. Nitumie fursa hii kuwataka wachimbaji wadogo kuacha tabia hiyo kwani ni ukiukaji wa Sheria za nchi.
98. Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi za Wizara yangu kutatua migogoro katika Sekta ya Madini, baadhi ya Wakuu wa Wilaya, Mikoa na Halmashauri wamekuwa wakijihusisha  
na usuluhishi wa migogoro katika maeneo ya utafutaji na uchimbaji madini, pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali yanayohusu usitishwaji ama kuhalalisha uchimbaji unaovunja Sheria wa madini. Hali hii imekuwa ikileta migongano ya kiutendaji na kukuza migogoro husika. Nitoe wito kwa viongozi hao kuepuka utoaji wa maamuzi yanayohusu Sekta ya Madini bila kushirikisha mamlaka husika.
Kuhamasisha Uongezaji Thamani Madini
99. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara yangu iliendeleza ushirikiano na wadau wa madini ili kuboresha mbinu bora za uchenjuaji na uongezaji thamani madini. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Aprili, 2013 jumla ya leseni 32 za uchenjuaji madini ya dhababu zilitolewa ikiwa ni maendeleo ya awali katika kuhawilisha teknolojia (technology transfer) ya uchenjuaji madini ya dhahabu kwa wachimbaji wadogo. Aidha, katika kujenga uwezo wa kuchenjua madini ya shaba hapa nchini, Serikali ilitoa leseni mbili (2) za kuyeyusha madini ghafi ya shaba. Leseni hizo zilitolewa kwa Kampuni ya Danformation (T) Limited ya Jijini Dar es Salaam na TPM (T) Limited ya Mpanda Mjini. Viwanda hivyo vina uwezo wa kuyeyusha jumla ya tani 48,000 za shaba ghafi kwa mwaka. Maboresho zaidi ya teknolojia yanafanywa na viwanda hivi ili viweze kuchenjua shaba zaidi za madaraja ya chini ya kiwango cha asilimia 18.
100. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendea kuimarisha shughuli za uongezaji thamani madini ya vito nchini ambapo madini ya vito yaliyokatwa Mwaka 2012/13 ni Karati 751,415 kati ya tani 1,545 za vito ghafi iliyozalishwa. Hivi sasa, kuna vituo 183 vya ukataji vito hapa nchini, mashine 107 za ukataji vito na wataalamu wa ukataji wapatao 105.
101. Mheshimiwa Spika, katika kuweka mkazo suala la uongezaji thamani wa madini, hususan madini ya vito, Wizara ilianzisha Kituo cha Uongezaji wa Thamani Madini cha Arusha (Arusha Gemmological Centre) Mwaka 2009 kwa lengo la kufundisha wachimbaji wadogo namna ya kuongeza thamani madini yao. Katika Mwaka 2012/13, Kampuni ya OGM Consultants ya Dar es Salaam ilisaini Mkataba wa kusanifu na kusimamia ukarabati wa Kituo hicho. Aidha, tarehe 01 Aprili, 2013 Mshauri alipatikana kwa ajili ya kuandaa Mpango Kazi wa Kituo, Mitaala ya Kufundishia, Mahitaji na Sifa za Wakufunzi wanaohitajika ili kuanzisha na kutimiza masharti ya kusajili Kituo. Pia, Kampuni ya Wagtech Projects Limited ya Uingereza imesaini Mkataba wa kuleta mashine za ukataji, usanifu na utengenezaji wa mapambo ya vito katika Kituo hicho. Kazi hiyo itakamilika Mwaka 2014/15 na itagharimu Dola za Marekani milioni 2 sawa na Shilingi bilioni 3.2.
Kuimarisha Soko la Madini ya Vito
102. Mheshimiwa Spika, Serikali ilianzisha Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Usonara yaliyofanyika kwa mara ya kwanza Mwezi Aprili, 2012 mjini Arusha. Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika tena Mwezi Oktoba, 2013. Aidha, maandalizi yanaendelea ili kuhakikisha kuwa maonesho hayo yanapanuka zaidi na kufanyika kila mwaka ili kuifanya Tanzania kuwa kituo cha vito Barani Afrika. Lengo ni kukuza biashara na soko la madini ya vito hapa nchini.
103. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Kitengo cha TANSORT imeendelea kusimamia biashara ya madini ya almasi na vito hapa nchini kwa kutambua, kuchambua na kuthamini madini hayo. Katika kipindi cha Mwaka 2012/13, jumla ya Karati 125,940 za almasi zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 31.70, sawa na Shilingi bilioni 50.72 zilichambuliwa na Karati 751,415 za madini ya vito yaliyokatwa na tani 5,392 za madini ghafi ya vito yenye jumla ya Dola za Marekani milioni 28.72, sawa na Shilingi bilioni 45.95 zilithaminishwa na kuuzwa nje ya nchi. Jumla ya mrabaha uliolipwa Serikalini ni Shilingi bilioni 4.19, sawa na Dola za Marekani milioni 2.62.
Kuimarisha Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira Migodini
104. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Ilani ya Chama Tawala ya Mwaka 2010 – 2015 Ibara ya 56 (e) kuhusu kuimarisha ukaguzi wa migodi katika masuala ya usalama, afya na utunzaji wa mazingira migodini, Wizara iliendelea kufuatilia kwa karibu utendaji wa shughuli za migodi na utafutaji wa madini nchini. Katika kipindi cha Mwaka 2012/13 migodi 6 mikubwa ya dhahabu, migodi ya kati 15, migodi midogo 1,120 na maeneo 229 ya utafiti wa madini yalikaguliwa ambapo taarifa za ukaguzi huo zilitumika kurekebisha masuala ya kiusalama, mazingira na utendaji kwa ujumla. Aidha, katika kipindi hicho, Serikali ilikamilisha ujenzi wa mtaro katika eneo la D’souza lililopo Kitalu B Mirerani ili kuepusha maafa ya mafuriko kwa wachimbaji wadogo katika eneo hilo kama yaliyotokea miaka ya 1998 na 2008.
105. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa utunzaji wa mazingira migodini, uchambuzi na upitishaji wa Mipango ya Ufungaji wa Migodi (Mine Closure Plans) ulifanyika kwa migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi, North Mara na Tulawaka. Migodi yote hiyo pamoja na Mgodi wa Golden Pride ambao Mpango wake wa kufunga mgodi ulichambuliwa na kupitishwa hapo awali, itaingia katika hatua ya kusaini mikataba ya kuweka hati fungani (rehabilitation bond) ya
ukarabati wa mazingira. Aidha, uchambuzi wa mipango ya ufungaji wa migodi ya Geita (dhahabu), Mwadui (almasi) na TanzaniteOne (tanzanite) utakamilika ifikapo Julai, 2013. Kulingana na taarifa za Mipango ya Ufungaji wa Migodi hiyo, gharama za ukarabati wa mazingira ni: Bulyanhulu (Dola za Marekani milioni 35.86, sawa na Shilingi bilioni 57.38), Buzwagi (Dola za Marekani milioni 46.92, sawa na Shilingi bilioni 75.07), Golden Pride (Dola za Marekani milioni 9.56, sawa na Shilingi bilioni 15.30), North Mara (Dola za Marekani milioni 67.46, sawa na Shilingi bilioni 107.94) na Tulawaka (Dola za Marekani milioni 19.98, sawa na Shilingi bilioni 31.97). Aidha, gharama za awali za ufungaji migodi ambayo mipango yake haijaidhinishwa na Serikali ni Geita (Dola za Marekani milioni 63.36, sawa na Shilingi bilioni 101.38), Mwadui (Dola za Marekani milioni 26.49, sawa na Shilingi bilioni 42.38), na TanzaniteOne (Dola za Marekani milioni 0.13, sawa na Shilingi bilioni 0.21).
106. Mheshimiwa Spika, Migodi ya Golden Pride (Nzega) na Tulawaka (Biharamulo) inatarajiwa kufungwa rasmi ifikapo mwishoni mwa Mwaka 2013 na maeneo yake kukabidhiwa Serikalini. Kwa mujibu wa Sheria, mgodi unapofungwa eneo la mgodi husika hurejeshwa Serikalini ili lipangiwe matumizi mengine kadri itakavyoonekana inafaa. Hivyo, Serikali imeamua eneo la Mgodi wa Tulawaka lichukuliwe na STAMICO ili iendeleze uchimbaji kwa kiwango cha kati kwa kuwa bado 57
yapo mashapo ambayo yanaweza kuchimbwa kwa faida. Vilevile, eneo la Mgodi wa Golden Pride, Nzega litakabidhiwa Chuo cha Madini Dodoma ili litumike kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa mafundi mchundo (technicians).
Usimamizi wa Shughuli za Baruti
107. Mheshimiwa Spika, shughuli za uchimbaji madini huendana na matumizi ya baruti. Pamoja na kwamba baruti ni zana muhimu katika uchimbaji, matumizi yake yanahitaji udhibiti madhubuti ili kuhakikisha kuwa hayaleti madhara kwa watumiaji na jamii kwa ujumla. Ili kutimiza azma hiyo, Wizara iliendelea na maandalizi ya Sheria mpya ya Baruti na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwaka 2013.
108. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha usimamizi wa matumizi ya baruti, Wizara ilitoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini wapatao 409 katika Mikoa ya Lindi, Shinyanga na Singida. Mafunzo hayo yalihusu utaratibu wa kisheria wa upatikanaji, usafirishaji, utunzaji na utumiaji salama wa baruti. Lengo ni kuwajengea uwezo watumiaji wa baruti katika shughuli za uchimbaji wa madini nchini.
Utekelezaji wa Majukumu ya Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative - TEITI
109. Mheshimiwa Spika, nafurahi kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa, utekelezaji wa vigezo vitano vilivyokuwa vimesalia kuwezesha Tanzania kupata uanachama kamili wa EITI ifikapo tarehe 15 Februari, 2013 ulikamilika. Bodi ya EITI iliitangaza Tanzania kuwa mwanachama kamili wa EITI (EITI Compliant) tarehe 12 Desemba, 2012. Hatua hii ya uanachama kamili inaonesha kuwa Tanzania sasa inao mfumo thabiti wa utoaji wa taarifa za malipo na mapato kutoka katika kampuni zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini, gesi asilia na mafuta, ambao unawezesha wananchi kufahamu na kujadili mchango wa Sekta za Nishati na Madini katika Pato la Taifa. Tangazo la Bodi ya EITI lilitolewa miezi miwili kabla ya muda tuliokuwa tumejiwekea kutokana na utendaji mzuri wa Wizara na Sekretarieti ya TEITI nchini.
110. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka 2012/13, Rasimu ya Sheria itakayosimamia shughuli za TEITI katika ngazi ya Taifa imekamilika. Rasimu hiyo imezingatia maoni ya wajumbe wa Kamati Tekelezi na wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia na sekta binafsi. Aidha, Rasimu hiyo imewasilishwa kwa nchi wanachama ambazo tayari zina Sheria ya EITI kwa ajili ya kupata maoni ya nchi hizo tukikusudia kuboresha Rasimu yetu. Ni
matarajio yetu kuwa uandaaji wa Sheria hiyo utakamilika Mwaka 2014/15.
111. Mheshimiwa Spika, kuhusu kuhamasisha wachimbaji wadogo katika utoaji wa takwimu ili kubaini mchango wao kwenye sekta ndogo ya uchimbaji madini, Sekretariati ilitoa elimu juu ya Mpango wa EITI kwa viongozi wa Vyama vya Wachimbaji Wadogo vya Mikoa (Regional Miners Associations) waliokutana Dodoma tarehe 6 - 7 Desemba, 2012. Katika kikao hicho viongozi hao walichagua Mwakilishi wa wachimbaji wadogo kwenye Kamati Tekelezi ya TEITI kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Mwaka 2013 hadi 2015.
112. Mheshimiwa Spika, ili kujenga uwezo wa uendeshaji wa TEITI, wajumbe wa Kamati Tekelezi na watumishi wa Sekretariati wameendelea kupatiwa mafunzo na kushiriki katika makongamano yenye lengo la kubadilishana uzoefu kutoka nchi wanachama wa EITI. Mwezi Septemba, 2012 wajumbe wawili (2) wa Kamati Tekelezi na watatu (3) wa Sekretarieti walishiriki warsha juu ya mchango wa EITI katika usimamizi wa rasilimali za madini, gesi asilia, mafuta na misitu iliyofanyika Accra, Ghana. Aidha, Sekretarieti imeshiriki katika programu ya revenue forecasting kwa kutumia models kwa ajili ya kukadiria mapato ya Serikali kutoka Sekta ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta. Programu hii iliendeshwa na Mshauri M/S Econ – Poyry kwa ufadhili wa Serikali ya Kifalme ya Norway na ililenga kujenga uwezo wa Wizara na 60
Taasisi zinazohusika na usimamizi wa mapato ya Serikali, hususan Wizara ya Fedha, BOT, NBS, TEITI, TMAA, TPDC na TRA.
Kuongeza Fungamanisho la Sekta ya Madini na Sekta nyingine za Uchumi
113. Mheshimiwa Spika, kama nilivyobainisha katika hotuba yangu ya Mwaka 2012/13, kuwa njia mojawapo ya kuongeza fungamanisho la Sekta hii na sekta nyingine za jamii na uchumi ni kuhakikisha kwamba Kampuni zinazojishughulisha na madini zinatumia huduma na bidhaa za ndani kadri inavyowezekana. Katika kutekeleza azma hiyo, kanzidata ya mahitaji ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotakiwa migodini iliandaliwa, ambapo takwimu za Kampuni 13 za madini zilionesha kuwa huduma na bidhaa zinazotakiwa ni pamoja na catering and food services; logistics and clearing; jasi; pozzolana; makaa ya mawe; chokaa; huduma za maabara; huduma za kisheria; huduma za kihandisi; ukandarasi; na usafirishaji. Serikali itaendelea kuhamasisha na kuwasaidia Watanzania kujenga uwezo wa kutoa huduma hizo migodini.
114. Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa migodi mikubwa ya dhahabu nchini, kwa Mwaka 2012 ilinunua bidhaa na huduma za ndani zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 520.67, sawa na Shilingi bilioni 833.07. Kiasi hiki ni ongezeko la asilimia 61
37.2 ikilinganishwa na ununuzi uliyofanyika Mwaka 2011 wa Dola za Marekani milioni 379.57, sawa na Shilingi bilioni 607.31. Ununuzi wa bidhaa na huduma nje ya nchi kwa Mwaka 2012 ulikuwa Dola za Marekani milioni 829.35, sawa na Shilingi bilioni 1,326.96. Hivyo, ununuzi wa bidhaa na huduma za ndani kwa Mwaka 2012 ulikuwa ni asilimia 38.6 ya ununuzi wote wa ndani na nje.
Ujenzi na Uboreshaji wa Ofisi za Madini
115. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka 2012/13, Wizara ilikamilisha ukarabati wa Ofisi za Madini za Arusha na Shinyanga. Ukarabati huo umegharimu jumla ya Shilingi milioni 274.66 (Arusha Shilingi milioni 193.21 na Shinyanga Shilingi milioni 81.45). Maandalizi ya ujenzi wa ofisi za Dodoma, Mpanda na Mtwara yamekamilika na ujenzi unatarajiwa kuanza Mwaka 2013/14. Lengo la mradi huu ni kuboresha mazingira ya utoaji huduma kwa wananchi katika ofisi za madini mikoani.
116. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na juhudi za kutafuta fedha na kiwanja cha kujenga Ofisi za TMAA na TANSORT ili jengo hilo litumike pia kama kituo cha kimataifa cha biashara ya madini nchini. Kwa kuzingatia unyeti wa biashara hiyo, inabidi jengo hilo lijengwe kwenye eneo la kibiashara (strategic business area). Hivyo, ujenzi wake utaanza kutekelezwa mara kiwanja na fedha vitakapopatikana.
Elimu kwa Umma Kuhusu Uchimbaji wa Madini ya Urani
117. Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea na jukumu la kutoa elimu kwa kupitia vyombo vya habari na ziara za mafunzo kuhusu faida na changamoto za uchimbaji wa madini ya urani, ili kuondoa hofu kwa umma juu ya madhara ya utafutaji na uchimbaji wa madini hayo. Napenda kutumia nafasi hii kusisitiza kuwa kitaalamu, urani ikiwa katika hali ya muunganiko na oksijeni (Triuranium Octoxide - U3O8) kama ilivyo ardhini ama baada ya kuchimbwa na kuchenjuliwa haina madhara kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Uchimbaji wa madini ya urani unatarajiwa kuanza katika eneo la Mkuju Wilayani Namtumbo. Serikali itakuwa na hisa kwenye mgodi huu. Nawaomba wananchi waondoe hofu kuhusu madhara tarajiwa ya utekelezaji wa mradi huo kwa kuwa Serikali yao ipo makini na itazingatia taratibu zote za kitaifa na kimataifa za kuchimba, kutunza, kusafirisha na kuendeleza madini hayo.
118. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Mkuju unaomilikiwa na Kampuni ya Mantra Tanzania Ltd iliyosajiliwa na Msajili wa Kampuni chini ya Sheria za Tanzania uliuzwa Mwezi Desemba 2010 kwa Kampuni ya ARMZ ya Urusi baada ya kununua hisa za Kampuni mama iitwayo Mantra Resources ya Australia kupitia soko la hisa la Australia kwa bei ya jumla ya Dola za Marekani milioni 1,043.80, sawa na Shilingi
bilioni 1,670.08. Kufuatia hatua hiyo Serikali kupitia TRA iliwapatia madai wahusika ya Dola za Marekani milioni 205.80 ambapo Dola za Marekani milioni 196 zilitakiwa kulipwa kama Capital Gain Tax na Dola za Marekani milioni 9.8 ni Ushuru wa Stempu. Hata hivyo, Kampuni hiyo ilipinga madai hayo na shauri hilo lilifikishwa Mahakama ya Kodi.
119. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko kuwa Serikali imetoa leseni ya uchimbaji kwa Mradi wa Mto Mkuju bila kushirikisha baadhi ya wadau na kuwa malipo stahiki hayajalipwa. Napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa umiliki na uendeshaji wa uchimbaji mkubwa wa madini unakamilika kwa mhusika kupata leseni ya uchimbaji. Aidha, leseni ya uchimbaji hutolewa baada ya mwombaji kupatiwa Hati ya Mazingira kutoka kwa mamlaka husika. Hivyo, taratibu za kisheria zimezingatiwa katika kutoa leseni hiyo. Kutolewa kwa leseni hakukufuta kesi iliyokuwepo Mahakamani.
Kuanzishwa kwa Migodi Mipya
120. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na juhudi zake za kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Madini. Kutokana na juhudi hizo, mgodi mpya wa dhahabu wa New Luika ulifunguliwa Wilayani Chunya na kuanza uzalishaji Mwezi Septemba, 2012. Gharama za awali za uwekezaji za mradi huo ni Dola za Marekani milioni 136, sawa na Shilingi bilioni 217.60. Hadi 64
kufikia Mwezi Aprili, 2013 mgodi huo ulikuwa umezalisha wakia 26,636.6 za dhahabu, sawa na kilogramu 755.15 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 31.49 sawa na Shilingi bilioni 50.38 na kuipatia Serikali Dola za Marekani milioni 1.26, sawa na Shilingi bilioni 2.02 kutokana na mrabaha.
121. Mheshimiwa Spika, Kampuni ya RECB Limited inamiliki leseni Na. ML 237/2006, ML 238/2006 na ML 239/2006 kwa ajili ya kuchimba madini ya niobium kwenye mradi wa Pandahill huko Songwe (Mbeya Vijijini). Wamiliki wa mradi huo wanakamilisha taratibu za kuanza ujenzi wa mgodi. Gharama za awali za mradi ni takriban Dola za Marekani milioni 60, sawa na Shilingi bilioni 96. Miradi mingine ya madini ambayo inakaribia kuanzishwa ni pamoja na Mradi wa Kabanga Nickel ulioko Kabanga, Wilayani Ngara unaomilikiwa na Kabanga Nickel Company Limited ya Tanzania; Mradi wa Magambazi Wilayani Kilindi, Mkoani Tanga wa kuchimba madini ya dhahabu, unamilikiwa na Kampuni ya Canaco Resources (T) Limited ya Canada; Mradi wa Nickel wa Ntaka uliopo Wilayani Nachingwea unaomilikiwa na Kampuni ya Ngwena (T) Limited, Kampuni tanzu ya IMX Resources ya Australia; na Mradi wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo Wilayani Sengerema unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold ya Uingereza ambao upo katika hatua za mwisho za upembuzi yakinifu.
122. Mheshimiwa Spika, shughuli za upembuzi yakinifu kwa ajili ya Mradi wa Nickel wa Kabanga uliopo Wilayani Ngara zimekamilika. Majadiliano ya awali kuhusu Mkataba wa uendelezaji wa mradi huo yameanza kati ya Serikali na Kabanga Nickel Company Limited. Ujenzi wa mradi huo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 1.2, sawa na Shilingi bilioni 1,920. Aidha, shughuli za tathmini ya mazingira na fidia kwa wananchi watakaopisha mradi zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Mwaka 2014/15.
Taasisi na Mashirika yaliyo katika Sekta ya Madini
123. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza majukumu yake mengine kupitia Taasisi na Mashirika yaliyo chini yake katika Sekta ya Madini kama ifuatavyo:
Wakala wa Jiolojia Tanzania – GST
124. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) ulikamilisha kukusanya takwimu za jiofizikia kwa kutumia ndege na kutathmini upatikanaji wa madini katika Wilaya za Babati, Bagamoyo, Bahi, Chamwino, Dodoma, Hanang, Handeni, Igunga, Iramba, Kilindi, Kiteto, Kondoa, Manyoni, Mpwapwa, Mvomero, Simanjiro na Singida Vijijini. Kazi hiyo imegharimu takriban Dola za Marekani milioni 13.67, sawa na Shilingi bilioni 21.87. 66
Aidha, GST imekamilisha utafiti wa kijiosayansi kutathmini upatikanaji wa madini katika maeneo ya Wilaya za Chunya, Lindi, Liwale, Manyoni, Mbarali, Nachingwea na Ruangwa, pamoja na kuchora ramani za jiolojia za maeneo hayo. Hatua hii itasaidia kuelewa maeneo yote muhimu kwa ajili ya uwekezaji na kuwawezesha wachimbaji, hususan wachimbaji wadogo nchini kupata maeneo ya kuchimba. Baadhi ya madini yaliyogunduliwa kuwepo kwenye maeneo hayo ni pamoja na Platinum Group Metals (PGM), shaba, graphite, dhahabu na almasi.
125. Mheshimiwa Spika, GST imeanzisha vituo vitatu vipya vya kisasa vya kupimia matetemeko ya ardhi vyenye uwezo wa kunakili taarifa za matukio ya matetemeko moja kwa moja kwenye kompyuta mara tukio linapotokea. Vituo hivi viko Arusha, Dodoma na Mbeya. Wastani wa kiwango cha matetemeko kama ilivyonakiliwa kwenye vituo hivyo (average seismic data reading) ni kuanzia 4.1 hadi 4.8 kwa kipimo cha Richter ikimaanisha kwamba nchi yetu kwa sasa haiko kwenye hatari ya matetemeko ya ardhi (earth quakes). Aidha, ujenzi wa ghala la kuhifadhia sampuli za miamba (core shed) huko Dodoma ulikamilika katika Mwaka 2012/13 na umegharimu Shilingi milioni 417.60, sawa na Dola za Marekani 261,000.
126. Mheshimiwa Spika, kazi za geological mapping; geochemical survey; na ground geophysical survey zilianza katika maeneo yenye Quarter
Degree Sheet (QDS) 12 na kujumuisha taarifa za remote sensing katika QDS mbalimbali. Aidha, katika kipindi cha Mwaka 2012/13, Wakala umefanikiwa kubadilisha ramani za jiolojia, QDS 42 kutoka kwenye mfumo wa karatasi na kwenda kwenye mfumo wa digitali kwa gharama ya Shilingi milioni 33.60, sawa na Dola za Marekani 21,000.
Chuo cha Madini - MRI
127. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2012/13, Chuo cha Madini – Dodoma kiliendelea kutoa mafunzo katika ngazi ya cheti na stashahada kwa jumla ya wanafunzi 351 katika fani ya jiolojia na utafutaji madini, uhandisi migodi na uhandisi uchenjuaji madini. Mnamo Mwezi Juni, 2013 jumla ya wanafunzi 49 wanatarajiwa kuhitimu katika fani za jiolojia na utafutaji madini (28), uhandisi migodi (10) na uhandisi uchenjuaji madini (11).
128. Mheshimiwa Spika, Chuo pia kiliandaa Mitaala ya ngazi za stashahada katika fani mpya za uhandisi na usimamizi wa mazingira migodini na jiolojia ya mafuta na gesi asilia. Mitaala hiyo iliwasilishwa NACTE na kupata uhalali na ithibati (accreditation). Baada ya hatua hiyo, Chuo kilianza kutoa mafunzo katika ngazi ya Cheti na Stashahada katika fani za uhandisi na usimamizi wa mazingira migodini kwa wanafunzi 35, jiolojia ya mafuta na gesi asilia kwa wanafunzi 65. Wizara ya Nishati na Madini
inafadhili wanafunzi 15 katika fani ya uhandisi na usimamizi wa mazingira na wanafunzi 15 katika fani ya jiolojia ya mafuta na gesi asilia.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania – TMAA
129. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2012/13, Wakala wa Ukaguzi wa Madini ulitekeleza majukumu yake na kuwezesha kupatikana kwa mafanikio mbalimbali. Katika kipindi hicho, TMAA kwa kushirikiana na TRA ilifanya ukaguzi wa hesabu za fedha kwa wamiliki wa migodi mikubwa, ya kati na kwa wanunuzi wa madini (mineral dealers). Kutokana na ukaguzi huo, katika kipindi cha Julai 2012 hadi Machi 2013, Mgodi wa Golden Pride uliopo Nzega unaomilikiwa na Kampuni ya Resolute Tanzania Limited umelipa kiasi cha Shilingi bilioni 19.8 kama kodi ya mapato (Corporate Tax). Hivyo, jumla ya kodi ya mapato iliyolipwa na mgodi huo hadi sasa (tangu uanzishwe Mwaka 2009) ni Shilingi bilioni 90.9. Mgodi wa Dhahabu wa Geita uliopo Geita unaomilikiwa na Kampuni ya AngloGold Ashanti Limited umelipa jumla ya Shilingi bilioni 108.1 kama kodi ya mapato. Hivyo, jumla ya kodi ya mapato iliyolipwa na mgodi huo kuanzia Mwaka 2009 hadi Mwezi Machi, 2013 ni Shilingi bilioni 299.4. Vilevile, Mgodi wa Tulawaka unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold umelipa kodi ya mapato mara moja tu ya jumla ya Shilingi bilioni 77.4 kwa Mwaka  
2012. Migodi mikubwa iliyolipa kodi ya mapato Mwaka 2011/12 ni Golden Pride iliyolipa jumla ya Shilingi bilioni 37.18, sawa na Dola za Marekani milioni 23.24 na Mgodi wa Geita uliolipa jumla ya Shilingi bilioni 188.10, sawa na Dola za Marekani milioni 117.55.
130. Mheshimiwa Spika, Migodi ya Bulyanhulu (Kahama), Buzwagi (Kahama), El Hillal Minerals (Mwadui), North Mara (Tarime) na Williamson Diamond (Mwadui), haijaanza kulipa kodi ya mapato (corporate tax) kwa kuwa bado haijaanza kupata faida. Wizara inafuatilia kwa makini uwekezaji kwenye migodi hii ili ianze kulipa kodi ya mapato haraka iwezekanavyo. Malipo ya kodi nyinginezo yaliyofanywa na migodi mikubwa kwa Mwaka 2012 ni kodi ya zuio – Withholding Tax (jumla ya Shilingi bilioni 67.64), Pay As You Earn - PAYE (jumla ya Shilingi bilioni 87.45), Skills Development Levy (jumla ya Shilingi bilioni 19.32), Service Levy (jumla ya Shilingi bilioni 4 (kama ilivyofafanuliwa katika aya ya 135), kodi na tozo nyinginezo (jumla ya Shilingi bilioni 42.8) na mrabaha (jumla ya Shilingi bilioni 107)- kama ilivyofafanuliwa katika aya ya 142.
131. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TMAA imeimarisha ukaguzi wa madini ya ujenzi kwa kutumia hati za mauzo ya madini katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Ukaguzi huo umewezesha kiasi cha Shilingi milioni 838.9 kulipwa kama mrabaha katika kipindi cha kuanzia

Julai, 2012 hadi Aprili, 2013 ikilinganishwa na wastani wa Shilingi milioni tatu (3) zilizokuwa zikikusanywa kwa mwaka katika mikoa hiyo kabla ya utaratibu huu kuanza. Utaratibu huu umeanza kutumika pia katika Mikoa ya Arusha, Katavi, Kigoma, Mwanza na Rukwa ambapo jumla ya Shilingi milioni 722 zimekusanywa kama mrabaha katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Aprili, 2013.
132. Mheshimiwa Spika, ili kujua kiasi na thamani halisi ya madini yaliyozalishwa na kuuzwa na migodi mikubwa nchini, Wakala ulifanya ukaguzi na uhakiki wa madini katika migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, Golden Pride, Mwadui, New Luika, North Mara, TanzaniteOne na Tulawaka. Ukaguzi huo ulifanyika kwa kuweka wakaguzi kwenye migodi hiyo yote muda wote wa uzalishaji na umewezesha kukusanywa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 61.04, sawa na Shilingi bilioni 97.66 kama mrabaha kutoka kwenye migodi hiyo katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Aprili, 2013.
133. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi wa biashara ya madini nchini, Serikali kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) imeanzisha Madawati Maalum ya kukagua madini yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia Viwanja vya Ndege vya Kimataifa vya Mwalimu Julius Nyerere (Dar es Salaam), Kilimanjaro na Mwanza. Madawati hayo yamesaidia katika kubaini na hatimaye kuwakamata watu wasio  
waaminifu wanaosafirisha madini nje ya nchi kinyume cha Sheria. Kwa kipindi cha kuanzia Oktoba, 2012 hadi Aprili, 2013, madini yenye thamani ya takriban Shilingi bilioni 13.12, sawa na Dola za Marekani milioni 8.13 yalikamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha Sheria. Wahusika wamechukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.
134. Mheshimiwa Spika, Wakala kwa kushirikiana na NEMC umeendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa shughuli za ukarabati na utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi mikubwa, ya kati na midogo. Wahusika wamekuwa wakipewa maelekezo yenye lengo la kuboresha hali ya mazingira kwenye maeneo yao. Jumla ya migodi mikubwa 8, ya kati 12 na midogo 123 ilikaguliwa katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Aprili, 2013. Ukaguzi huo umesaidia kuimarika kwa shughuli za utunzaji wa mazingira katika maeneo ya migodi.
135. Mheshimiwa Spika, Halmashauri za Wilaya zinazohusika na migodi mikubwa nchini zimeendelea kulipwa ushuru wa huduma (Service Levy) kwa mujibu wa Sheria zilizopo. Mwaka 2012, Mgodi wa Bulyanhulu umelipa Dola za Marekani 200,000 kwa Halmashauri ya Kahama; Mgodi wa North Mara umelipa Dola za Marekani 200,000 kwa Halmashauri ya Tarime; Mgodi wa Tulawaka umelipa Dola za Marekani 200,000 kwa Halmashauri ya Biharamulo; Mgodi wa Buzwagi umelipa Dola za Marekani
200,000 kwa Halmashauri ya Kahama; Mgodi wa Geita umelipa Dola za Marekani 200,000 kwa Halmashauri ya Geita; Mgodi wa Golden Pride umelipa Dola za Marekani 1,462,374 kwa Halmashauri ya Nzega; Mgodi wa TanzaniteOne umelipa Dola za Marekani 16,432 kwa Halmashauri ya Simanjiro; na Mgodi wa Mwadui umelipa Dola za Marekani 30,300 kwa Halmashauri ya Kishapu. Jumla ya malipo yaliyofanywa na migodi hiyo kwa Halmashauri husika kuanzia Mwaka 2006 hadi 2012 ni Dola za Marekani 9,099,005 sawa na Shilingi bilioni 14.41.
136. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na majadiliano na Kampuni za Madini zenye MDAs ili zikubali kuondoa kipengele kinachowaruhusu kulipa Ushuru wa Huduma katika kiwango cha Dola za Marekani 200,000 badala ya kulipa kiasi cha asilimia 0.3 ya mapato halisi kama Sheria inavyotaka. Migodi hiyo ni ile ya Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, North Mara na Tulawaka. Aidha, Halmashauri za Wilaya zinatakiwa kudai malipo ya Ushuru wa Huduma kwa Kampuni zinazotoa huduma kwenye migodi. Kampuni hizo zinatakiwa kulipa ushuru huo kwa kiwango cha asilimia 0.3 ya mapato halisi.
Shirika la Madini la Taifa – STAMICO
137. Mheshimiwa Spika, Serikali iliamua kulihuisha Shirika la STAMICO ili litekeleze majukumu mahsusi katika Sekta ya Madini kwa maslahi ya  
Taifa. Napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa tumeendelea kulijenga upya Shirika hili ikiwa ni pamoja na kulipatia fedha, vifaa vya utafutaji madini na kuongeza idadi ya watumishi. Bodi ya STAMICO imeteuliwa rasmi tarehe 14 Aprili, 2013 na kuzinduliwa tarehe 11 Mei, 2013. Hadi Desemba, 2012 Shirika hilo lilikuwa na thamani (Book Value) ya Shilingi bilioni 5.47. Katika kipindi cha Julai, 2012 hadi Aprili, 2013; matumizi ya Shirika yalikuwa Shilingi bilioni 2.35. Vyanzo vya mapato ya Shirika yalikuwa ruzuku kutoka Serikalini Shilingi bilioni 1.02; malipo ya ubia (Shilingi bilioni 1.22); mabadiliko ya thamani ya Shilingi kwa fedha za kigeni (Shilingi milioni 53.40); huduma ya uchorongaji (Shilingi milioni 29.99); na kodi ya pango (Shilingi milioni 29.35).
138. Mheshimiwa Spika, STAMICO ina ubia na Kampuni ya TANZAM 2000 katika Mradi wa uendelezaji upya Mgodi wa Buckreef. Katika Mradi huu, STAMICO inamiliki hisa asilimia 45 na TANZAM 2000, inamiliki asilimia 55. Katika Mwaka 2012/13, kazi zilizofanyika katika mradi huu ni pamoja na uchorongaji miamba, uchunguzi wa sampuli za miamba katika maabara na resource modelling kwa ajili ya kutathmini mashapo. Hadi Mwezi Aprili, 2013 kiasi cha dhahabu kilichothibika kuwepo katika mradi wa Buckreef na maeneo ya jirani ya Bingwa na Tembo Mines ni wakia za dhahabu milioni 2.12.
139. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza azma ya Serikali ya kushiriki katika uwekezaji kwenye Sekta ya Madini, Mwezi Januari, 2013 STAMICO ilimpata mbia wa kuendeleza upya Mgodi wa Dhahabu wa Buhemba. Mbia aliyepatikana ni Kampuni ya Manjaro Resources ya Australia. Mgodi huo una mabaki ya uchimbaji wa zamani (tailings) yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 70, sawa na Shilingi bilioni 112. Aidha, eneo hilo linakadiriwa kuwa na mashapo ya dhahabu katika miamba kwa kiwango cha wakia 400,000. Kupitia STAMICO, Serikali itamiliki hisa asilimia 40 katika mgodi utakaoanzishwa na kupata gawio la asilimia 30 ya thamani ya dhahabu itakayozalishwa kutokana na mabaki ya uchimbaji wa zamani yaliyopo katika eneo hilo.
140. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 inayotaka madini ya vito kuchimbwa na Watanzania kwa umiliki wa hisa zisizopungua asilimia 50, Serikali ilifikia makubaliano kati yake na Kampuni ya TanzaniteOne inayochimba madini ya Tanzanite. Kutokana na makubaliano hayo, STAMICO kwa sasa ni mmiliki mwenza wa eneo la leseni ya Kitalu C, Mirerani kwa asilimia 50 kwa niaba ya Serikali.
141. Mheshimiwa Spika, kuhusu Mgodi wa Kiwira, napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa, mgodi huu umerudishwa rasmi Serikalini baada ya sehemu kubwa ya madai yaliyokuwepo  
kulipwa. Hivi sasa, Serikali kupitia STAMICO ipo huru kuuendeleza mgodi huo. Malipo yaliyofanyika ili kuurudisha Serikalini mgodi huo ni jumla ya Shilingi bilioni 40 zilizolipwa kwa wadai mbalimbali ikiwa ni pamoja na CRDB, PSPF na NSSF. Mgodi huo unatarajiwa kuanza tena uzalishaji wa makaa ya mawe ifikapo Mwaka 2015/16. Shughuli zitakazofanyika kabla ya kuanza uzalishaji ni kupanua mgodi wa chini; kujenga mgodi wa wazi (open - cast); kujenga mtambo wa kufua umeme wa MW 200; na kujenga njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 132 kutoka Kiwira hadi Mbeya. Shughuli hizo zinakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 450, sawa na Shilingi bilioni 720.
Mafanikio Yaliyopatikana katika Sekta ya Madini
142. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2012 hadi Aprili, 2013, Sekta ya Madini ilipata mafanikio yafuatayo: kulipwa Serikalini kwa kodi ya mapato (corporate tax) kutoka Kampuni za Geita Gold Mining Limited (Geita) - Shilingi bilioni 108.1, Resolute Tanzania Limited (Golden Pride) - Shilingi bilioni 19.8 na African Barrick Gold (Tulawaka) - Shilingi bilioni 77.4. Kulipwa kwa Shilingi milioni 838.9 kama mrabaha kutokana na uzalishaji wa madini ya ujenzi kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani; kukusanywa kwa jumla ya Dola za Marekani milioni 61.04, sawa na Shilingi bilioni 97.66 kama mrabaha kufuatia ukaguzi na uhakiki
wa madini yaliyozalishwa kwenye migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi, Geita, Golden Pride, New Luika, North Mara, Mwadui, TanzaniteOne na Tulawaka; kuanzishwa kwa madawati kwenye viwanja vya ndege vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza kwa ajili ya kudhibiti utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi, ambapo madini yenye thamani ya takriban Shilingi bilioni 13.12 yalikamatwa yakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha Sheria; STAMICO kupewa Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Kiwira na kupata mbia wa kuendeleza upya Mgodi wa dhahabu wa Buhemba; Tanzania kuwa mwanachama kamili wa EITI (EITI compliant); na Chuo cha Madini, Dodoma kuanzisha fani mpya katika ngazi ya stashahada za uhandisi na usimamizi wa mazingira migodini na jiolojia ya mafuta na gesi asilia.
143. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa miradi mipya ya Mkuju – urani (Ruvuma), Pandahill – niobium (Mbeya), Ntaka – nickel (Lindi) na Dutwa – nickel (Simiyu); kuanzishwa kwa vituo vitatu vya kisasa vya kupima matetemeko ya ardhi katika Mikoa ya Arusha, Dodoma na Mbeya; kukamilika kwa ujenzi wa ghala la kuhifadhi sampuli za miamba (core shed); kukamilika kwa kazi ya ukusanyaji wa takwimu za jiofizikia na tathmini ya upatikanaji wa madini katika Wilaya 17; kukamilika kwa utafiti wa kijiosayansi na uchoraji wa ramani wa kijiolojia kwa Wilaya za Chunya, Lindi, Liwale, Manyoni, Mbarali, Nachingwea na Ruangwa;
kutengwa kwa maeneo 16 yenye ukubwa wa hekta 265,396 kwa ajili ya uchimbaji mdogo wa madini; kukamilika kwa ujenzi wa mtaro wa D’souza katika eneo la Mirerani; kukamilika kwa ukarabati wa ofisi za madini Arusha na Shinyanga; na kuendelea kurasimisha (formalizing) wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuanzisha REMAs.
144. Mheshimiwa Spika, sambamba na mafanikio hayo ya kisekta, naomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa Wizara yangu imepata Hati Safi ya Hesabu za Mwaka 2011/12. Matokeo hayo yamepatikana baada ya Wizara kusimamia kikamilifu mapato na matumizi yake kwa kufuata taratibu, Sheria na kanuni zilizopo. Wizara itaendelea kuboresha zaidi utendaji wake ili kuhakikisha fedha za umma zinatumika kulingana na vipaumbele vilivyowekwa kwa manufaa ya Watanzania.
145. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka 2011/12, pamoja na Hati Safi ya Hesabu, Wizara pia imepata alama za jumla za asilimia 83 kwa kufuata taratibu za ununuzi ipasavyo na kuwa moja kati ya Wizara zenye ufanisi katika masuala yote ya ununuzi. Ufanisi huo ulibainishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) baada ya kufanyika ukaguzi. Mafanikio hayo ni dalili njema Kiwizara na Kitaifa kwa ujumla katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinatumika kwa uwazi na kwa manufaa ya Watanzania.
Changamoto Zinazokabili Sekta ya Madini
146. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha utekelezaji cha Mwaka 2012/13, Sekta ya Madini ilikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo; utengaji wa maeneo ya wachimbaji wadogo; ukuaji kwa kasi wa shughuli za uchimbaji usio rasmi; kuzuia uvamizi wa maeneo yenye leseni za utafutaji na uchimbaji madini unaofanywa na wachimbaji holela; kushamiri kwa biashara isiyo halali ya madini, hususan, madini ya dhahabu na vito; fungamanisho la Sekta ya Madini na sekta nyingine za uchumi; na usalama, afya na mazingira katika maeneo ya migodi.
Ajira na Maendeleo ya Rasilimali Watu
147. Mheshimiwa Spika, kufuatia ugunduzi mkubwa wa gesi asilia nchini, Wizara imeendelea kutekeleza Mpango wa Uendelezaji Rasilimali Watu wa Marshall Plan on Capacity Building and Development in Oil and Gas Industry 2012 - 2016 ili kuzalisha wataalamu Watanzania wa kutosha katika fani hizo. Mwaka 2012/13 kupitia mpango huo, Wizara kwa kushirikiana na TPDC imeweza kufadhili vijana wa Kitanzania 122 katika fani ya mafuta na gesi ambapo vijana 30 walipelekwa Chuo cha Madini Dodoma (MRI) kwenye mafunzo ya miaka mitatu (Full Technician Certificate); 10 Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM); 64 VETA Lindi na 50 VETA Mtwara (Certificates); na taratibu za kuwapeleka vijana 10 nchini Brazil na 20 China  
kusoma kozi katika ngazi za uzamili na uzamivu katika fani za gesi na mafuta zimekamilika. Aidha, Wizara imedhamini watumishi wanne (4), wawili (2) kutoka Wizara yangu na wawili (2) kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda katika masomo ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Aberdeen nchini Uingereza.
148. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka 2012/13, Wizara iliajiri watumishi 30 kwa kibali cha Mwaka 2011/12. Aidha, taasisi zilizo chini ya Wizara ziliajiri jumla ya watumishi 22. Kati ya hao TPDC (17) na REA (5).
149. Mheshimiwa Spika, katika kuongeza tija na motisha kwa watumishi, katika Mwaka 2012/13 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 56 na kuwathibitisha kazini watumishi 15. Aidha, Wizara iliwapeleka mafunzoni jumla ya watumishi 90 katika fani mbalimbali. Kati ya hao, 26 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na 64 mafunzo ya muda mfupi.
150. Mheshimiwa Spika, kuhusu masuala ya afya za watumishi, Wizara iliendelea kutekeleza Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa Mwaka 2006 ambapo watumishi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (VVU) na wenye UKIMWI wanapewa huduma ya lishe, chakula na madawa maalum.

C. MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2013/14
151. Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2013/14 umezingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/12 – 2015/16; Malengo ya Taifa ya MKUKUTA II; Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010 - 2015; Mpango Mkakati wa Wizara ya Nishati na Madini 2011/12 – 2015/16; Maagizo ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa kwa Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti; Mwongozo wa Utayarishaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2013/14; na ushauri uliotolewa na Bunge pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti.
152. Mheshimiwa Spika, pamoja na miongozo hiyo, Wizara pia imeandaa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2013/14, kwa kuzingatia Mpango Mpya wa Ufuatiliaji na Tathmini wa miradi mikubwa ya Kitaifa ulioanzishwa na Serikali. Mpango huo unalenga katika kupata matokeo makubwa sasa “Big Results Now”. Mpango huo unashirikisha sekta sita, ambapo Sekta ya Nishati ni miongoni mwa sekta hizo. Wizara yangu imejipanga na imedhamiria kwa dhati kuhakikisha kuwa inatekeleza miradi yote iliyobainishwa katika Mpango huo, kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea “business as usual” na badala yake kufanya kazi kwa ubora, ufanisi na ubunifu wa hali ya juu.  
153. Mheshimiwa Spika, kulingana na matokeo ya Maabara ya Nishati (Energy Lab), iliyofanyika kupitia Mpango huo, jumla ya miradi 28 ilibainishwa, ambapo saba (7) ni ya ufuaji umeme, saba (7) ni ya usafirishaji umeme na 14 ni ya usambazaji umeme. Kati ya hiyo, miradi mitatu (3) itatekelezwa kwa utaratibu wa Public Private Partnership (PPP), mmoja utatekelezwa na Kampuni binafsi ya Kilwa Energy na miradi iliyobaki itatatekelezwa na Serikali. Gharama za kutekeleza miradi hiyo yote zinakadiriwa kuwa Shilingi trilioni 7, ambapo Serikali itachangia Shilingi trilioni 4.85 kwa kipindi cha miaka mitatu 2013/14 – 2015/16 na kiasi kilichobaki kitatolewa na Sekta Binafsi pamoja na Washirika wa Maendeleo.
154. Mheshimiwa Spika, Mpango huu unalenga kuleta manufaa makubwa kwa Taifa letu ifikapo Mwaka 2015/16, hivyo, naamini kuwa Wizara itapata ushirikiano mkubwa katika kutekeleza miradi hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo: Waheshimiwa Wabunge, Washirika wa Maendeleo, Wawekezaji wa Ndani na Nje na Wananchi kwa ujumla.
155. Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2013/14, pamoja na masuala mengine, unalenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika; kuongeza wateja wanaotumia umeme hasa vijijini; kuongeza kasi ya kupeleka umeme Makao Makuu ya Wilaya; ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia;
kusimamia na kudhibiti biashara ya mafuta; kuvutia uwekezaji katika Sekta za Nishati na Madini; kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali; kujenga uwezo wa usimamizi na ufuatiliaji katika Sekta za Nishati na Madini ili kukuza uchumi na kuharakisha maendeleo ya Taifa letu, kama ilivyoainishwa ndani ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo Mwaka 2025.
Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali
156. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imepanga kukusanya jumla ya Shilingi bilioni 220 katika Mwaka 2013/14. Kiasi hiki ni asilimia 14 zaidi ya lengo lililowekwa kwa Mwaka 2012/13 la kukusanya Shilingi bilioni 193.01. Mipango ambayo itatumika kukusanya mapato hayo ya Serikali ni pamoja na: kuboresha na kusimamia mikataba ya utafutaji na uzalishaji katika Sekta za Nishati na Madini; kuboresha Mfumo wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini (Mining Cadastral Information Management System – MCIMS); kuwezeshwa kwa Ofisi za Madini za Kanda kukusanya maduhuli ipasavyo; kuendelea kuimarisha usimamizi wa wachimbaji wadogo, kuwapa wachimbaji wadogo huduma za ugani na elimu juu ya ulipaji kodi na ada mbalimbali ili kuongeza tija katika uzalishaji madini; kudhibiti utoroshaji wa madini na ukwepaji wa kulipa mrabaha; na kuimarisha usimamizi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kanuni zake.  
SEKTA YA NISHATI
157. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka 2013/14, kazi zilizopangwa kutekelezwa katika Sekta ya Nishati ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam; kuimarisha njia za kusafirisha na kusambaza umeme; kuongeza ufuaji umeme; kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia umeme majumbani na kwenye shughuli za kiuchumi; kupeleka umeme katika Makao Makuu ya Wilaya 13 na maeneo mengine vijijini; kuboresha usimamizi na udhibiti wa biashara ya mafuta; kuweka misingi ya kisheria ya kusimamia Sekta Ndogo ya Gesi Asilia; kuendeleza vyanzo vya nishati jadidifu; na kupitia na kurekebisha miundo ya Mashirika ya TANESCO na TPDC kwa lengo la kuyaboresha na kuongeza ufanisi.
158. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali imeamua kutekeleza miradi itakayoleta matokeo makubwa na kwa haraka. Kutokana na uamuzi huo, kiasi cha Shilingi bilioni 545.13 kati ya Shilingi bilioni 558.35, sawa na asilimia 98 ya Fedha za Ndani za Bajeti ya Maendeleo kwa Mwaka 2013/14 zimetengwa ili kutekeleza miradi itakayoleta matokeo makubwa na ya haraka (Big Results Now).
SEKTA NDOGO YA UMEME
Kuongeza Uzalishaji wa Umeme Nchini
Miradi ya Kinyerezi I (MW 150) na II (MW 240)
159. Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali ni kuhakikisha mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi asilia inakamilika sawia na Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Hivyo, Serikali kupitia TANESCO itawezesha utekelezaji wa mradi wa uzalishaji umeme wa Kinyerezi I (MW 150) na Kinyerezi II (MW 240) ambapo, kazi za usanifu wa eneo la mradi (site layout design) na shughuli za ujenzi zitaanza. Katika Mwaka 2013/14 jumla ya Shilingi bilioni 208, sawa na Dola za Marekani milioni 130 zimetengwa kwa ajili ya Mradi wa Kinyerezi I na Shilingi bilioni 109.9, sawa na Dola za Marekani milioni 68.69 zimetengwa kwa ajili ya Mradi wa Kinyerezi II. Serikali itakamilisha ujenzi wa mitambo, kituo cha kupoozea umeme (sub-station 220kV) na njia ya kusafirisha umeme (kV 220) kutoka eneo la mradi na kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa eneo la Kimara na njia nyingine (kV 132) kwenda kwenye kituo cha Gongo la Mboto kwa ajili ya matumizi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Mradi wa Kinyerezi III (MW 300) na Kinyerezi IV (MW 300)
160. Mheshimiwa Spika, mradi wa Kinyerezi III unahusisha ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa MW 300 kwa kutumia gesi asilia. Mradi huu utatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali kupitia TANESCO na sekta binafsi. Katika kipindi cha Mwaka 2013/14, Serikali itakamilisha majadiliano na kampuni ya ubia kwa ajili ya kutekeleza mradi huo. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Mwaka 2015/16. Mradi huu utagharimu takriban Dola za Marekani milioni 389, sawa na Shilingi bilioni 662.4.
161. Mheshimiwa Spika, mradi wa Kinyerezi IV unahusisha ujenzi wa mtambo wa kufua umeme wa MW 300 kwa kutumia gesi asilia na njia ya kusafirisha umeme ya kV 400 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kupitia Morogoro. Serikali itakamilisha majadiliano na Mbia kutoka sekta binafsi kwa ajili ya kutekeleza mradi huo unaotarajiwa kukamilika Mwaka 2015/16. Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 800, sawa na Shilingi bilioni 1,280.
(i) Mradi wa Somanga Fungu MW 320
162. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazofanyika katika mradi huo kwa Mwaka 2013/14 ni pamoja na kukamilisha Mkataba wa Utekelezaji, kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi na 86
kuanza ujenzi. Awamu ya kwanza ya mradi huo itaanza na ufuaji wa MW 230 kwa kutumia gesi asilia. Mradi utakamilika Mwaka 2015/16 na utagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 365, sawa na Shilingi bilioni 564.
(ii) Mradi wa Kuzalisha MW 400 Mkoani Mtwara
163. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya umeme katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, Serikali kupitia TANESCO imeingia mkataba na Kampuni ya Symbion Tanzania Limited kwa ajili ya kujenga mtambo wa kufua umeme wa MW 400 Mkoani Mtwara. Njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 400 kuanzia Mtwara hadi Songea itajengwa ikiwa ni sehemu ya mradi huo. Umeme utakaofuliwa utatumika katika mikoa ya kusini na ziada itaingizwa kwenye Gridi ya Taifa pamoja na kuuzwa Msumbiji na Malawi. Kutekelezwa kwa mradi huu, kutaongeza fursa za ajira kwa wakazi wa mikoa ya kusini kutokana na kuongezeka kwa uwekezaji kwenye sekta za viwanda na kilimo. Maandalizi ya Mradi yameanza kwa Kampuni ya Symbion kuanza kufanya upembuzi yakinifu na baadaye kuandaa gharama ya mradi husika.
(iii) Mradi wa Rusumo wa MW 80
164. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha upembuzi yakinifu kwenye eneo ambapo bwawa  
la kuzalisha umeme litajengwa; kuanzisha chombo cha kusimamia utekelezaji wa mradi (Special Purpose Vehicle - SPV); na kuingia mikataba ya kuuziana umeme kati ya SPV na mashirika ya umeme katika nchi husika. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya nchi tatu za Burundi, Rwanda na Tanzania ambapo mchango wa Tanzania ni Dola za Marekani milioni 28, sawa na Shilingi bilioni 44. Katika Mwaka 2013/14, Shilingi bilioni 22 sawa na Dola za Marekani milioni 13.75 zimetengwa ikiwa ni mchango wa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
(iv) Mradi wa Murongo/Kikagati MW 16
165. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali ya Tanzania na Uganda zitakamilisha mkataba wa ushirikiano (Bilateral Agreement) ili kuwezesha mradi huo kuanza kutekelezwa. Mradi huo unagharimu Dola za Marekani milioni 30.46, sawa na Shilingi bilioni 48.74. Mradi utatekelezwa na mwekezaji binafsi Trond Energy kutoka Norway na umepangwa kukamilika Mwaka 2015/16.
(v) Mradi wa Ufuaji na Usambazaji wa Umeme – Biharamulo, Mpanda na Ngara
166. Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa tathmini ya zabuni, ufungaji wa jenereta za kufua umeme wa MW 2.5 na usambazaji wa
umeme katika maeneo ya Biharamulo, Mpanda na Ngara utaanza Mwaka 2013/14. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uholanzi kwa gharama ya Euro milioni 33, sawa na Shilingi bilioni 66. Katika Mwaka 2013/14, Serikali imetenga Shilingi bilioni 2.1 kwa ajili ya utekelezaji na mradi utakamilika Mwaka 2014.
(vi) Ukarabati wa Mitambo katika Vituo vya Kufua Umeme
167. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha vituo vya kufua umeme nchini kwa Mwaka 2013/14, mitambo ya kituo cha kuzalisha umeme cha Hale kinachotumia nguvu za maji itakarabatiwa kwa ufadhili wa Serikali za Tanzania na Sweden. Mwaka 2013/14 kazi zilizopangwa kufanyika ni hizi zifuatazo: kumpata mshauri wa mradi, usanifu wa mradi na kuanza taratibu za kuwapata wazabuni mbalimbali wa mradi. Mradi huo umetengewa Shilingi bilioni 8.93 sawa na Dola za Marekani milioni 5.58 na unatarajiwa kukamilika Mwaka 2014/15.
Kuimarisha Njia za Kusafirisha na Kusambaza Umeme
168. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali itaendelea kuimarisha njia za kusafirisha na kusambaza umeme. Lengo ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 21 ya sasa
hadi kufikia asilimia 15 Mwaka 2015/16. Kazi hii itafanyika kupitia miradi mbalimbali ikiwemo:
(i) Uboreshaji wa Huduma za Umeme Jijini Dar es Salaam
169. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali kupitia TANESCO itaanza usanifu wa maeneo yatakayohusika na mradi, ununuzi wa vifaa, ujenzi na mafunzo kwa watumishi wa TANESCO watakaohusika na mradi huo. Jumla ya Shilingi bilioni 19.85 sawa na Dola za Marekani milioni 12.41 zitatolewa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Tanzania Energy Development and Access Expansion Project (TEDAP) na Serikali ya Finland ili kutekeleza mradi huo. Mradi huo utakamilika Mwaka 2014/15.
(ii) Mradi wa Makambako – Songea kV 220
170. Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa durusu ya kuongeza uwezo wa njia ya umeme kutoka kV 132 hadi kV 220, katika Mwaka 2013/14, Serikali kupitia TANESCO itafanya tathmini ya mali zilizoko ndani ya njia kuu ya kusafirisha umeme kwa mara ya pili; kulipa fidia; kusafisha njia kuu ya umeme yenye umbali wa kilometa 250 pamoja na viwanja vitakapojengwa vituo vya kupozea umeme eneo la Madaba na Songea; na kumpata mkandarasi wa mradi. Katika Mwaka 2013/14 jumla ya Shilingi bilioni 12.58, sawa na Dola za Marekani milioni 7.86 90
zimetengwa ambapo fedha za ndani ni Shilingi bilioni 2, sawa na Dola za Marekani milioni 1.25 na fedha za nje zitakazotolewa na Shirika la Maendeleo la Sweden ni Shilingi bilioni 10.58 sawa na Dola za Marekani milioni 6.61.
(iii) Mradi wa Iringa – Shinyanga kV 400
171. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazotekelezwa katika Mwaka 2013/14 ni pamoja na: ukamilishaji wa zabuni za kuwapata wakandarasi wa kujenga njia ya umeme msongo wa kV 400 katika vipande vitatu (3) vya Iringa – Dodoma, Dodoma – Singida na Singida – Shinyanga; maandalizi ya kuongeza uwezo wa vituo vya kupozea umeme katika Mikoa ya Dodoma, Iringa, Shinyanga na Singida; na kuhamisha miundombinu ya huduma za kijamii. Katika Mwaka 2013/14, Shilingi bilioni 5.44, sawa na Dola za Marekani milioni 3.4 zimetengwa kwa ajili ya kazi hizo, ambapo Shilingi milioni 440, sawa na Dola za Marekani 275,000 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 5, sawa na Dola za Marekani milioni 3.13 ni za nje. Mradi huo utakamilika Mwaka 2015/16.
(iv) Mradi wa North – West na North – East Grid kV 400
172. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali kupitia TANESCO itasanifu upya mradi huo kutoka kV 220 kwenda kV 400. Shilingi milioni 560, sawa na Dola za Marekani 350,000 zimetengwa kwa ajili ya kudurusu usanifu wa 91
mradi huo. Mradi umeombewa fedha kutoka Serikali ya China kama mradi wa kipaumbele. Ni mradi muhimu ambao utawezesha nchi yetu kuwa na Gridi kubwa yenye kusafirisha umeme mwingi. Mikoa ya Magharibi mwa nchi yetu itapata umeme mwingi na wa uhakika kupitia Gridi hii.
173. Mheshimiwa Spika, mradi wa North – East Grid unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya Dar es Salaam – Chalinze – Tanga – Same hadi Arusha katika msongo wa kV 400. Mradi wa North –West Gridi utakaohusisha ujenzi wa njia ya kV 400 kutoka Nyakanazi – Kigoma – Katavi – Rukwa hadi Mbeya. Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa njia kutoka Mbeya hadi Sumbawanga ambao utagharimu takriban Dola za Marekani milioni 136.25, sawa na Shilingi bilioni 218. Mradi wa North – East Gridi utagharimu Dola za Marekani milioni 770, sawa na Shilingi bilioni 1,232. Hata hivyo, baada ya msongo wa njia za umeme za miradi hiyo ya kubadilisha kutoka kV 220 hadi kV 400, Serikali inapanga kuhuisha Upembuzi Yakinifu uliopo sasa (updating Feasibility Study) ili kupata gharama halisi za miradi hiyo.
174. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali itaendelea na juhudi za kutafuta fedha ili kutekeleza miradi ya North – West na North – East Grid, ambayo ni miongoni mwa miradi ya Kitaifa ya kipaumbele iliyobainishwa kuleta matokeo makubwa na ya haraka (Big Results 92
Now). Miradi hiyo imepangwa kukamilika Mwaka 2015/16.
(v) Ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kutoka Mtwara - Songea na Mtwara – Lindi – Somanga Fungu (kV 220)
175. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha mikoa ya kusini kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, Serikali itasimamia ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme kutoka Mtwara hadi Songea na Mtwara hadi Somanga Fungu (Lindi). Hadi sasa, TANESCO wameingia makubaliano (MoU) na Kampuni ya M/S Symbion Power LLC. Miradi hii ikikamilika itaibua fursa mbali mbali za kiuchumi katika mikoa hiyo.
(vi) Mradi wa Singida – Arusha – Namanga kV 400
176. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, kazi zilizopangwa kufanyika katika mradi huu ni kumpata mshauri kwa ajili ya utekelezaji wa mradi. Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Benki ya Dunia. Mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme yenye urefu wa kilomita 414.4 katika msongo wa kV 400 kuanzia Singida kupitia Babati na Arusha hadi Namanga, pamoja na vituo viwili vya kupozea umeme. Aidha, mradi unahusisha upelekaji umeme katika vijiji vilivyo kando kando ya njia hiyo ya umeme. Gharama ya mradi ni Dola za Marekani milioni 242.09,  
sawa na Shilingi bilioni 387.34 na lengo ni kuukamilisha ifikapo Mwaka 2017. Mradi huu ni miongoni mwa miradi ya vipaumbele (Big Results Now).
(vii) Mradi wa Electricity V
177. Mheshimiwa Spika, Serikali imekusudia kuendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme nchini. Mradi wa Electricity V unakusudia kuongeza usambazaji umeme vijijini pamoja na upanuzi wa vituo vya kupozea umeme katika Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam. Serikali imepata mkopo toka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wa Dola za Marekani milioni 45, sawa na Shilingi bilioni 72. Mradi huu umegawanyika katika sehemu mbili kubwa, (i) ujenzi wa njia za usambazaji umeme vijijini katika Mikoa ya Geita, Mwanza na Simiyu. Wilaya zitakazofaidika na mradi huu ni Bukombe na Mbogwe (Geita), Busega (Simiyu), Kwimba, Magu, Misungwi na Sengerema (Mwanza). Mkandarasi wa ujenzi wa njia hizi ni M/S Eitel Networks TE AB kutoka Sweden na ataanza kazi Mwezi Juni, 2013. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 19.2, sawa na Shilingi bilioni 30.72.
178. Mheshimiwa Spika, eneo la pili linahusu upanuzi wa vituo vya kupozea umeme katika Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam. Kituo cha Sokoine cha Dara es Salaam kitajengwa upya na pia kituo cha Ilala kitawekewa transfoma mpya yenye uwezo wa 15 MVA. Aidha, katika Jiji la 94
Arusha kituo cha kupozea umeme cha Njiro kitawekewa transfoma mbili za kupozea umeme zenye ukubwa wa 50 MVA kila moja na zitawekwa kwenye msongo wa Kilovolti 132/33. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 7.3, sawa na Shilingi bilioni 11.68.
Kupeleka Umeme Makao Makuu ya Wilaya na Vijijini
179. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA itawezesha utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa kusambaza umeme vijijini. Mpango huo utajumuisha kupeleka umeme katika Makao Makuu ya Wilaya 13 za Buhigwe, Busega, Chemba, Itilima, Kakonko, Kalambo, Kyerwa, Mkalama, Mlele, Momba, Nanyumbu, Nyasa na Uvinza pamoja na maeneo mengine ya vijijini. Katika Mwaka 2013/14, Shilingi bilioni 150 sawa na Dola za Marekani milioni 93.75 zimetengwa ambapo fedha za ndani ni Shilingi bilioni 90, sawa na Dola za Marekani milioni 56.25 na fedha za nje ni Shilingi bilioni 60 sawa na Dola za Marekani milioni 37.5. Aidha, REA inategemea kupata Shilingi bilioni 36, sawa na Dola za Marekani milioni 22.5 kutokana na asilimia 3 ya tozo ya mauzo ya umeme na asilimia 0.4 ya TRA pre- destination inspection fee on imported petroleum products. Aidha, gharama za kutekeleza awamu ya pili ya Mpango Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini ni Shilingi bilioni 881, sawa na Dola za Marekani milioni 550.63.

180. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia REA pia itaanza kutekeleza mradi wa majaribio wa gharama nafuu za miundombinu ya kusambaza umeme (Low Cost Design Standards) katika Mikoa ya Mbeya na Morogoro utakaounganisha jumla ya wateja 15,000 wa awali na idadi ya wateja inategemewa kuongezeka na kufikia zaidi ya 20,000.
181. Mheshimiwa Spika, REA itaendelea kuwezesha utoaji wa mafunzo na usaidizi wa kitalaam kwa wajasiriamali wa nishati na waendelezaji wa vyanzo mbalimbali vya nishati bora. Aidha, Wakala utawezesha utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Global Village Energy Partnership Program (GVEP). Katika miradi hiyo, vyanzo sita vya kuzalisha umeme wa maporomoko madogo ya maji vitaendelezwa. Vyanzo hivyo ni Darakuta (Babati), Lingatunda (Songea Vijijini), Luswisi (Ileje), Macheke (Ludewa), Mwoga (Kasulu), na Nole-Ihalula (Njombe). Kwa ujumla vyanzo hivi vitakuwa na uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawati 9.1 na hivyo kuwezesha kuunganisha jumla ya wateja 27,600. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi hiyo ni Shilingi bilioni 2 sawa na Dola za Marekani milioni 1.25.
(viii) Mradi wa Tanzania Energy Development and Access Expansion Project (TEDAP) Unaofadhiliwa na Benki ya Dunia
182. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka 2013/14, Serikali kupitia mradi wa TEDAP off - grid itaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huu ikiwemo: kukagua mifumo ya umeme wa jua iliyofungwa; kuhamasisha matumizi ya nishati bora; kufunga mifumo ya umeme jua kwenye vituo vya huduma za jamii Sumbawanga na kuwezesha kuanza utekelezaji katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Ruvuma, Shinyanga na Tabora. Aidha, waendelezaji wa miradi midogo ya kufua umeme wataendelea kukamilisha miradi yao chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia na Global Environment Facility (GEF) kupitia ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu. Gharama ya sehemu hii ya mradi (off – grid) ni Dola za Marekani milioni 22.5, sawa na Shilingi bilioni 35.
183. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutekeleza mradi wa TEDAP (on-grid), ambapo itakamilisha ujenzi wa kituo cha KIA cha kupozea umeme wa kV 132/33 kwa kuongeza transfoma moja yenye uwezo wa MVA 20 na upanuzi wa kituo cha Kipawa kwa kuongeza transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 90 kila moja. Aidha, ujenzi wa njia za usafirishaji za msongo wa kV 132 kutoka Ubungo hadi Kurasini, Kurasini hadi Mbagala na Kipawa hadi Gongo la Mboto utaendelea,  
ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Gongo la Mboto kV 132/33, mbili zenye uwezo wa MVA 45. Gharama ya sehemu hii ya mradi (on – grid) ni Dola za Marekani milioni 89, sawa na Shilingi bilioni 142.4.

SEKTA NDOGO YA NISHATI JADIDIFU
(i) Usimamizi wa Bio-energy
184. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Wizara itawasilisha kwa wadau Rasimu ya Sheria ya Bio-energy ili kupata maoni. Aidha, Mshauri wa kuainisha maeneo maalum (agro-ecological zoning) ya uendelezaji wa maeneo ya mimea ya bio-energy atapatikana ifikapo Mwaka 2013/14. Serikali pia itajenga uwezo kwa Taasisi zake na Halmashauri za Wilaya, vyombo vya fedha, wakulima, Taasisi zisizo za Kiserikali ili kuweza kusimamia kikamilifu masuala ya bio-energy. Katika Mwaka 2013/14, Shilingi bilioni 1, sawa na Dola za Marekani 625,000 zitatolewa na NORAD (Norway) na Sida (Sweden) kwa ajili ya kazi hizo.
(ii) Usimamizi wa Tungamotaka (Biomass)
185. Mheshimiwa Spika, Serikali itaandaa Mkakati wa Nishati ya Tungamotaka (Biomass Energy Strategy) nchini ambao utatoa mwongozo wa upatikanaji, usimamizi na matumizi bora ya tungamotaka. Kazi hii inatekelezwa na mshauri, Kampuni ya CAMCO (T). Aidha, Serikali 98
itafanya tathmini ya miradi ya tungamotaka inayotekelezwa na taasisi na kampuni binafsi kama vile Katani Ltd (kW 300), Sao Hill (MW 15), Tanzania Planting Company - TPC (MW 20) na Tanzania Wattle Company – TANWAT (MW 2.5). Lengo la tathmini hiyo ni kubaini namna bora ya kuendeleza matumizi ya tungamotaka kama chanzo cha nishati. TANESCO inanunua umeme kiasi cha MW 12 kutoka Kampuni za TANWAT na TPC. Katika Mwaka 2013/14, Shilingi milioni 500, sawa na Dola za Marekani 312,500 zitatolewa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa ajili ya mradi huo.
Kuendeleza Vyanzo vya Nishati Jadidifu
(i) Mradi wa Low Carbon Efficient Sustainable Energy Access
186. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, kazi zilizopangwa kutekelezwa chini ya mradi huu ni pamoja na: kuandaa tathmini ya mahitaji na upatikanaji wa nishati jadidifu; kuanzisha miradi ya nishati jadidifu; na kujenga uelewa kwa Halmashauri za Wilaya 10 zilizochaguliwa kushiriki katika mradi huu ambazo ni Geita, Kahama, Kasulu, Kwimba, Mbinga, Mbulu, Misenyi, Mpanda, Ngorongoro na Urambo. Miradi hiyo ni ya nishati ya umeme utokanao na jua, upepo, maporomoko madogo ya maji na tungamotaka. Jumla ya Shilingi bilioni 1.6, sawa na Dola za Marekani milioni 1 zitatolewa na UNDP kwa Mwaka 2013/14 kwa ajili ya mradi huo.
(ii) Mradi wa Biogas
187. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Kituo cha uendelezaji wa Zana za Kilimo na Teknolojia za Vijijini (CAMARTEC) kilichopo Arusha itaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi wa biogas chini ya programu ya uendelezaji biogas ngazi ya kaya (Tanzania Domestic Biogas Programme). Mitambo 12,000 inatarajiwa kujengwa katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Pwani, Ruvuma, Singida na Tanga. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Uholanzi liitwalo HIVOS, na utakamilika Mwaka 2014/15. Gharama za mradi huu ni takribani Shilingi bilioni 30, sawa na Dola za Marekani 18.75.
(iii) Uendelezaji wa Jotoardhi (Geothermal) na Mpango wa Scaling up Renewable Energy (SREP)
188. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo wakiwemo AfDB, BGR, DFID, ICEIDA, IFC JICA, UNEP, USAID na WB wamekubaliana kushiriki katika kuendeleza joto ardhi hapa nchini. Katika Mwaka 2013/14, kazi zitakazotekelezwa ni pamoja na kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia, kijiokemia na kijiofizikia katika maeneo matano yaliyopo Kisaki (Morogoro), Luhoi (Pwani), Majimoto (Musoma), Ziwa Manyara (Manyara) na Ziwa Natron (Arusha).
Matumizi Bora ya Nishati (Energy Conservation and Efficiency)
189. Mheshimiwa Spika, matumizi bora ya nishati ni muhimu ili kupunguza upotevu wa nishati, kuokoa fedha na kulinda mazingira. Miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa kwa ajili ya matumizi bora ya nishati ni kubadili taa zinazotumia umeme mwingi (Incandescent Bulbs) na kuweka zinazotumia umeme kidogo (Compact Florescent Light - CFL). Kwa kuanzia, zoezi hili litahusisha mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza, ambapo jumla ya taa milioni 3.2 zitabadilishwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 24, sawa na Dola za Marekani milioni 15

SEKTA NDOGO ZA GESI ASILIA NA MAFUTA
Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mtwara – Dar es Salaam
190. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali kupitia TPDC itaendelea kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na: ujenzi wa mitambo miwili ya kusafisha gesi asilia katika maeneo ya Songo Songo (Lindi) na Mnazi Bay (Mtwara); ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Lindi na Mtwara hadi Dar es Salaam; ujenzi wa vituo vya kupokelea gesi asilia Somanga Fungu, Kinyerezi na Tegeta; ujenzi 101
wa ofisi na kambi za wafanyakazi wa mradi; na ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kusafishia gesi asilia. Katika Mwaka 2013/14, Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 63, sawa na Dola za Marekani milioni 39.4 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. Fedha hizo zitatumika kulipia sehemu ya mchango wa Serikali katika mkopo wa Bomba la Gesi Asilia.
191. Mheshimiwa Spika, Serikali pia itahakikisha kuwa Vijiji vilivyopo kandokando na mkuza wa Bomba la Gesi Asilia vinanufaika na mradi huo. Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali kupitia REA itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika vijiji hivyo kutoka Mtwara hadi Lindi. Kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na kupata Mshauri wa kufanya tathmini na kuvitambua vijiji vitakavyohusika; kutayarisha na kutangaza zabuni za ujenzi; na kuanza ujenzi wa miundombinu. Katika Mwaka 2013/14, kiasi cha Shilingi bilioni 20, sawa na Dola za Marekani milioni 12.5 kimetengwa kwa ajili ya kazi hizo.
Utafutaji wa Gesi Asilia na Mafuta
192. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDC itaendelea kusimamia shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini kulingana na mikataba ya makampuni iliyoingia na Serikali. Jumla ya visima 17
vinatarajiwa kuchimbwa katika kipindi cha Mwaka 2013/14. Visima hivyo vitachimbwa na Kampuni za Afren, BG, Dodsal, Dominion, Heritage, Hydro Tanz, Maurel & Prom, Ndovu Resource, Ophir, Pan African na Statoil. Wastani wa gharama za kuchimba kisima kimoja ni kati ya Dola za Marekani milioni 40 na milioni 100 sawa na Shilingi bilioni 64 na bilioni 160 sawia.
193. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza uwekezaji, Serikali ilipanga kutangaza na kunadi maeneo mapya ya utafutaji wa mafuta na gesi nchini Marekani Mwezi Septemba, 2012. Hata hivyo, ili kuhakikisha mikataba mipya yote inafuata Sera na Sheria husika, tuliamua kusitisha hadi tuwe na Sera na Sheria. Kwa Mwaka 2013/14, Serikali imeamua kwamba zabuni ya awamu ya nne ya kunadi maeneo mapya ya uwekezaji (Fourth Off-shore Licensing Round) katika kina kirefu cha bahari ifanyike hapa nchini tarehe 25 Oktoba, 2013 Jijini Dar es Salaam. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa zoezi la kunadi maeneo mapya ya uwekezaji katika utafutaji wa mafuta kufanyika nchini. Pamoja na faida nyinginezo, zoezi hili kufanyika nchini litakuwa ni fursa muhimu kwa sisi wenyewe kuitangaza nchi yetu.
Kusimamia na Kudhibiti Biashara ya Mafuta
194. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali kupitia EWURA, itaendelea kuimarisha udhibiti wa biashara ya mafuta hapa nchini.  
Katika kutekeleza jukumu hilo, EWURA itahakikisha kuwa: miundombinu inayohusiana na biashara ya mafuta inajengwa na kutunzwa kulingana na Sheria ya EWURA ya Mwaka 2001 na Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2008; mafuta yanaagizwa na kuuzwa nchini kwa kuzingatia mwenendo wa bei katika soko la Dunia; na kuhakikisha usawa wa mazingira ya ushindani (level playing field) katika biashara ya mafuta.
Sera, Mipango na Sheria katika Sekta ya Nishati
195. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali itakusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuboresha durusu ya Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2003. Vilevile, Serikali itakamilisha Sera ya Petroli ambayo itatoa miongozo kuhusu shughuli za utafutaji na uendelezaji wa Sekta ndogo za Mafuta na Gesi Asilia (Upstream Petroleum Policy).
196. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Sera ya Gesi Asilia utaanza katika Mwaka 2013/14, baada ya Serikali kutoa uamuzi. Aidha, Wizara itakamilisha Mpango Kabambe wa Matumizi ya Gesi Asilia nchini ifikapo Juni, 2014. Katika Mwaka 2013/14, Serikali pia itawasilisha Sheria ya Gesi Asilia katika Bunge lako Tukufu.
Taasisi, Mashirika na Kampuni katika Sekta ya Nishati
(i) Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
197. Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kupitia upya muundo wa TANESCO ili kuongeza ufanisi na kuongeza ushindani katika Sekta Ndogo ya Umeme kwa lengo la kuboresha huduma za umeme nchini. Wizara imepokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wananchi na inatarajia kupokea mapendekezo ya muundo kutoka Menejimenti na Bodi ya TANESCO ifikapo tarehe 31 Mei, 2013.
198. Mheshimiwa Spika, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetoa fedha (Grant) za kumpata Mshauri ambaye atatoa mapendekezo juu ya Muundo Mpya wa TANESCO unaofaa kufikiriwa na Serikali. Benki hiyo pia, imekubali kutoa fedha za kujenga uwezo wa watendaji wa Wizara, TANESCO na TPDC. Baada ya kupokea mapendekezo kutoka vyanzo mbalimbali, Wizara itaandaa Mwongozo (Road Map) wa namna bora ya kubadilisha muundo wa TANESCO na Sekta Ndogo ya Umeme. Mwongozo umepangwa kukamilika Mwezi Juni, 2014.
(ii) Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
199. Mheshimiwa Spika, kutokana na kuongezeka kwa shughuli za utafutaji mafuta na uendelezaji wa matumizi ya gesi asilia, Serikali inapitia upya muundo wa TPDC ili kuongeza ufanisi kwa kuanzisha kampuni tanzu za Shirika hilo. Kampuni tanzu zitahusika na shughuli za usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia, na mafuta nchini. Menejimenti na Bodi ya TPDC zimeagizwa kuwasilisha mapendekezo ya muundo mpya wa Shirika hilo ifikapo tarehe 30 Mei, 2013. Aidha, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetoa fedha (Grant) kumpata Mshauri ambaye atatoa mapendekezo juu ya Muundo Mpya wa TPDC unaofaa kufikiriwa na Serikali.
(iii) Ushiriki wa Serikali katika Kampuni za TIPER, Puma Energy Ltd na TAZAMA
200. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali kupitia Wizara itaendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uendeshaji wa Kampuni ambazo Serikali ina hisa za Puma Energy Limited (hisa za Serikali ni asilimia 50), Tanzania Zambia Pipeline Limited - TAZAMA (hisa za Serikali ni asilimia 30), na Tanzania International Petroleum Reserve - TIPER (hisa za Serikali ni asilimia 50).
SEKTA YA MADINI
201. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka 2013/14, kazi zilizopangwa kutekelezwa katika Sekta ya Madini ni pamoja na kuboresha utoaji na usimamizi wa leseni za madini; kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini; kuongeza idadi ya wachimbaji wadogo (ajira); kuendelea kuvutia wawekezaji wakubwa; kuimarisha makusanyo ya maduhuli yatokanayo na madini; kuimarisha usimamizi wa afya, usalama na utunzaji wa mazingira migodini; kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini; kuimarisha usimamizi wa biashara ya madini; kuwezesha Taasisi na Mashirika yaliyo chini ya Wizara; na kujenga ofisi za madini Dodoma, Mpanda na Mtwara.
Kuboresha Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini
202. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Wizara itaendelea kuboresha Mfumo wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni (MCIMS) ikiwa ni pamoja na kukamilisha maandalizi ya kuwawezesha waombaji kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao wa intaneti (online). Wizara pia itaendelea kushughulikia maombi ya leseni kwa wakati na itahakikisha kuwa maombi yote yaliyowasilishwa kabla ya tarehe 31 Desemba, 2012 yanashughulikiwa na kujibiwa ifikapo mwishoni mwa Mwezi Septemba, 2013. Aidha, Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kwa kufuta
leseni zote zinazokiuka matakwa ya Sheria hiyo ili kutoa nafasi kwa wawekezaji wengine wenye uwezo wa kuyaendeleza.
Kuendeleza Uchimbaji Mdogo wa Madini
203. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia STAMICO, GST, MRI, TMAA na kwa kushirikiana na SIDO, VETA na Chuo Kikuu ca Dar es Salaam (UDSM) itaendelea kutekeleza mpango wa mafunzo kwa nadharia na vitendo kwa wachimbaji wadogo. Katika Mwaka 2013/14, mikopo kwa wachimbaji wadogo itatolewa kupitia Benki ya TIB badala ya utaratibu wa awali wa kukopesha na kukodisha vifaa vya uchimbaji katika vituo maalum vilivyoanzishwa. Utaratibu huu utarahisisha ufuatiliaji wa marejesho ya mikopo na kuongeza idadi ya wakopaji. Vifaa vya uchimbaji vya kukodisha vitasimamiwa na STAMICO. Aidha, Wizara itaendelea kutenga maeneo ya uchimbaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Kuongeza Idadi ya Wachimbaji Wadogo (Ajira)
204. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kutenga maeneo kwa ajili ya uchimbaji mdogo. Maeneo 10 yanatarajiwa kutengwa katika sehemu mbalimbali nchini kwa ajili ya wachimbaji wadogo kwa Mwaka 2013/14. Aidha, Wizara itaendelea kutoa elimu ya ugani kwa wachimbaji wadogo ili kuwawezesha kufanya shughuli za utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji mbale (ore) kwa tija na ufanisi zaidi. Juhudi hizo zitaongeza ajira kwa Watanzania na kuinua kipato chao.108
Kuimarisha Makusanyo ya Maduhuli Yatokanayo na Madini
205. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na madini ambapo kwa Mwaka 2013/14 lengo ni kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 199.96, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.12 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 173.70 zilizopangwa kukusanywa kwa Mwaka 2012/13. Lengo hilo litafikiwa kwa kuimarisha ufuatiliaji wa maduhuli hayo kupitia Ofisi za Madini za Kanda. Pia, shughuli za ukaguzi kupitia TMAA zitachangia kwa kiasi kikubwa kufikiwa kwa lengo hilo. Nitoe agizo kwa wamiliki wa leseni za madini kuacha mchezo wa kukwepa kulipa kodi na mrabaha stahiki. Wale watakaobainika, Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufuta leseni zao.
Kuimarisha Usimamizi wa Afya, Usalama na Utunzaji wa Mazingira Migodini
206. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kusimamia Sheria zinazohusu Afya, Usalama na Utunzaji wa Mazingira migodini kwa kuimarisha ukaguzi katika migodi mikubwa, ya kati na midogo. Aidha, Wizara itakamilisha hatua ya pili ya mipango ya ufungaji migodi (mine closure plans) ya Bulyanhulu, Buzwagi, Golden Pride, North Mara na Tulawaka kwa kuhakikisha kuwa migodi hiyo inaweka hatifungani (Rehabilitation Bond) kwa ajili ya ukarabati wa mazingira. Vilevile, Wizara itakamilisha mipango ya ufungaji migodi  
kwa migodi ya Geita Gold Mine, TanzaniteOne na Williamson Diamonds Limited. Aidha, Serikali itasimamia taratibu za eneo la Mgodi wa Golden Pride, Nzega kukabidhiwa kwa Chuo cha Madini, Dodoma na Mgodi wa Tulawaka, Biharamulo kukabidhiwa kwa STAMICO pindi migodi hiyo itakapofungwa rasmi.
Kuendelea Kuvutia Wawekezaji Wakubwa
207. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali itaendelea kuvutia mitaji na teknolojia inayohitajika kuendeleza Sekta ya Madini. Kazi hii itafanyika kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika Sekta ya Madini, kushiriki kwenye warsha na maonesho ya ndani na nje ya nchi yanayokutanisha wawekezaji katika Sekta ya Madini, kutoa taarifa za kijiolojia kupitia GST zinazohitajika katika shughuli za utafutaji wa madini, kutoa leseni za madini kwa wakati kwa waombaji watakaotimiza masharti ya kisheria.
Kuhamasisha Shughuli za Uongezaji Thamani Madini
208. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka 2013/14, Wizara itaendelea kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani madini nchini na kutoa leseni za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini ya metali ikiwemo shaba. Aidha, Wizara itakamilisha Sheria ya Uongezaji Thamani Madini ili kukuza na kusimamia
vyema shughuli za uongezaji thamani kwa lengo la kuongeza mapato na ajira kwa Watanzania.
209. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Wizara itaendelea kukiimarisha Kituo cha Usanifu wa Vito cha Arusha kwa kukamilisha ukarabati wa majengo yake; kukipatia mashine za ukataji, usanifu na utengenezaji mapambo ya vito; kuandaa Mpango Kazi wa Kituo na mitaala ya kufundishia pamoja na kupatikana Wakufunzi wenye sifa stahiki.
Kuimarisha Usimamizi wa Biashara ya Madini
210. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi wa biashara ya madini nchini, Serikali kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) itaendelea kuimarisha madawati maalum ya kukagua madini yanayosafirishwa nje ya nchi kupitia Viwanja vya Ndege vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza. Nitoe wito kwa watendaji wote wa Serikali katika viwanja hivyo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa TMAA katika kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na utoroshaji wa madini. Pia, niwasihi wale wote wanaojihusisha au kufikiria kutorosha madini, kuacha mara moja kufanya hivyo kwani wakipatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria bila huruma.
211. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Serikali itaendelea kuboresha Kitengo cha Utambuzi na Ukadiriaji Thamani Almasi na  
Madini ya Vito (TANSORT), ili kiweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya ushauri wa masoko, ukataji na ukadiriaji thamani madini ya vito kwa wachimbaji wadogo na wa kati; kutoa huduma za kijemolojia (Gemmological Services) kwa wachimbaji wadogo na wa kati; kusimamia mauzo ya almasi na madini ya vito ndani na nje ya nchi; na kuthaminisha almasi na madini ya vito kwa ajili ya kukokotoa mrabaha. Aidha, Serikali itaendelea kujenga uwezo wa Kitengo hiki ili kiweze kutoa huduma kwa Watanzania wengi zaidi; kutoa elimu ya kulinda na kukuza soko la ndani na nje la almasi na vito kwa lengo la kuchangia ukuaji wa uchimbaji almasi na vito nchini; na kuendeleza wachimbaji wadogo wa almasi na madini ya vito, hususan katika maeneo ya ukadiriaji thamani madini ya vito.
212. Mheshimiwa Spika, Kitengo cha TANSORT kitaendelea kutumia ofisi yake ndogo iliyoko Antwerp, Ubelgiji katika kusimamia mauzo ya almasi ya Mgodi wa Mwadui (WDL) ambayo hufanyika huko Antwerp. Kupitia ofisi hiyo, TANSORT pia itaendelea kufuatilia masoko ya almasi na vito duniani kwa lengo la kupata bei na mwenendo wa masoko hayo. Pia, Serikali itaendelea kutafuta fedha na kiwanja kwa ajili ya kujenga jengo la kudumu la ofisi za TMAA na TANSORT ili shughuli za biashara ya madini nchini zifanyike sehemu moja na iliyo salama.112
213. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Sera ya Madini ya Mwaka 2009 kuhusu kuimarisha soko la madini ya vito nchini, Wizara kwa kushirikiana na TAMIDA itaendelea kusimamia Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Usonara ya Arusha. Kwa Mwaka 2013/14, maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 hadi 31 Oktoba, 2013 huko Arusha. Kupitia maonesho hayo, Serikali inatarajia kukusanya mrabaha wa zaidi ya Shilingi milioni 330, sawa na Dola za Marekani 206,250 kutokana na mauzo ya almasi na vito. Maonesho hayo yatajikita katika uhamasishaji na uendelezaji wa mfumo wa masoko ya madini; na uhamasishaji na uwezeshaji katika uongezaji thamani madini ili kuongeza fursa za ajira nchini. Uendelezaji wa maonesho hayo ni hatua ya kuifanya Tanzania kuwa kituo cha biashara ya madini ya vito barani Afrika.
Kujenga Ofisi za Madini - Dodoma, Mpanda na Mtwara
214. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi ni kujenga na kuimarisha ofisi za Maafisa Madini Wakazi na Kanda kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wadau wa Sekta ya Madini. Katika Mwaka 2013/14, Wizara itaendelea na mpango wake wa ujenzi wa Ofisi za Dodoma, Mpanda na Mtwara. Ili kutekeleza mradi huu, jumla ya Shilingi bilioni 4, sawa na Dola za Marekani milioni 2.5 zimetengwa kwa Mwaka 2013/14.113
Usimamizi wa Matumizi ya Baruti
215. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kusimamia utunzaji na matumizi sahihi ya baruti nchini. Ili kutekeleza jukumu hilo, Wizara itatoa mafunzo juu utunzaji, matumizi sahihi na salama ya baruti. Kwa Mwaka 2013/14, mafunzo hayo yatatolewa katika Mikoa ya Arusha, Katavi, Mtwara na Mwanza ili kuendelea kuwajengea uwezo watumiaji wa baruti. Aidha, ukaguzi wa mara kwa mara wa maghala ya kuhifadhia baruti utaendelea kufanyika ili kudhibiti matumizi mabaya na hatarishi ya baruti. Katika kuhakikisha kuwa matumizi ya baruti yanasimamiwa ipasavyo, Wizara itakamilisha Sheria mpya ya baruti ifikapo mwishoni mwa Mwaka 2014. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kazi hiyo ni Shilingi milioni 300, sawa na Dola za Marekani 187,500.
Elimu kwa Umma kuhusu Sekta ya Madini
216. Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na malalamiko mengi yanayoelekezwa kwenye Sekta ya Madini, hususan, kuhusu mchango wa Sekta hii katika uchumi wa Taifa. Malalamiko hayo, pamoja na mambo mengine yametokana na umma kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu Sera na Sheria zinazosimamia Sekta ya Madini. Katika Mwaka 2013/14, Wizara itaendelea kutoa elimu kwa umma kupitia vipindi vya redio na televisheni za hapa nchini. Maandalizi ya vipindi vya televisheni yamekamilika na vipindi  
hivyo vitaendelea kurushwa kupitia vyombo vya habari vya ndani kuanzia mwanzoni mwa Mwaka 2013/14.
Taasisi na Mashirika katika Sekta ya Madini
Chuo cha Madini - MRI
217. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14 Chuo cha Madini kitaendelea kutoa mafunzo katika ngazi ya cheti na stashahada katika fani za jiolojia ya utafutaji madini; uhandisi migodi; uhandisi uchenjuaji madini; uhandisi na usimamizi wa mazingira migodini; na jiolojia na uhandisi wa mafuta na gesi asilia. Aidha, kufuatia ongezeko la wanafunzi lililotokana na kuanzishwa kwa mafunzo ya fani mpya za mazingira; na mafuta na gesi asilia, Serikali kwa kushirikiana na wahisani katika Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia itafadhili ujenzi wa madarasa unaokadiriwa kugharimu Shilingi milioni 513, sawa na Dola za Marekani 320,625. Katika kipindi hicho pia, Chuo kitakamilisha ujenzi wa madarasa mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 140 kila moja.
218. Mheshimiwa Spika, pamoja na ujenzi wa madarasa, Serikali imepanga kujenga mihadhara nane (8) yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban 800, ofisi nane (8) za wakufunzi na ukumbi wa mikutano ambapo michoro ya majengo hayo imekamilika. Kwa Mwaka 2013/14 kiasi cha Shilingi bilioni 1.22, sawa na Dola
za Marekani 762,500 kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo.
219. Mheshimiwa Spika, Serikali imedhamiria kukipandisha hadhi Chuo hicho katika kiwango cha “Polytechnic”. Hatua hiyo, itawezesha Chuo hicho kutoa mafunzo ya aina mbalimbali na kupanua wigo wa kujiendesha kibiashara. Aidha, Chuo kitafungua campus mpya huko Wilayani Nzega baada ya Mgodi wa Golden Pride kufungwa rasmi na Chuo hicho kukabidhiwa majengo na miundombinu ya mgodi huo.
Shirika la Madini la Taifa – STAMICO
220. Mheshimiwa Spika, katika kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo, katika Mwaka 2013/14 Shirika litaajiri wafanyakazi wapya 78, kuwajengea uwezo wafanyakazi wapya na kuongeza vitendea kazi vya utafutaji madini ambavyo ni pamoja na magnetometers, resistivity/IP equipment na Gamma rays spectrometers. Vifaa hivyo vinakadiriwa kugharimu jumla ya Dola za Marekani 450,000 sawa na Shilingi milioni 720.
221. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, STAMICO na mbia wake, TANZAM 2000 wataendeleza upembuzi yakinifu katika eneo la Mgodi wa Buckreef ambao unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa Mwaka 2015. 116
222. Mheshimiwa Spika, kufuatia STAMICO kupata mbia wa kuendeleza Mgodi wa Buhemba, Kampuni ya Manjaro Resources, taratibu za kuunda na kusajili Kampuni ya ubia baina yao zitafanyika katika kipindi cha Mwaka 2013/14. Katika kipindi hicho, mkataba rasmi wa ubia (Definitive Joint Venture Agreement) utakamilika. Kazi zitakazotekelezwa baada ya kuingia mkataba ni kufanya tathmini ya mabaki ya zamani ya mgodi; kujenga mtambo wa kuchenjua mabaki hayo; na kufanya utafiti wa dhahabu katika miamba ndani ya eneo la leseni.
223. Mheshimiwa Spika, kufuatia kukamilika kwa makubaliano ya STAMICO kuwa mmiliki mwenza kwa asilimia 50 na Kampuni ya TanzaniteOne kwenye leseni ya eneo la Kitalu C Mirerani, Shirika litaingia mkataba rasmi wa uchimbaji na TanzaniteOne Mining Limited. Mkataba huo utaainisha namna uchimbaji utakavyoendeshwa, menejimenti ya mgodi, mgawanyo wa mapato; na wajibu wa wanahisa. Lengo ni kukamilisha mkataba huo ifikapo tarehe 30 Julai, 2013.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)
224. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarisha ukaguzi wa shughuli za uzalishaji na biashara ya madini kwa migodi mikubwa, ya kati na midogo kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), ili kuhakikisha kuwa Taifa linanufaika ipasavyo na rasilimali yake ya  
madini. Wakala utaendelea kuimarisha ukaguzi wa hesabu za fedha na kodi za migodi mikubwa, ya kati na wafanyabiashara wa madini ili kuhakikisha wanalipa kodi na mrabaha stahiki. Pia, Wakala utakamilisha mchakato wa usajili wa Maabara yake katika Shirika la Viwango vya Kimataifa (ISO 17025) ili iweze kujiendesha kibiashara; na kujenga uwezo katika kubainisha maoteo ya mapato ya Serikali kutoka kwenye Sekta ya Madini kwa kutumia mfumo wa kisasa (revenue forecasting model) ili kuwa na takwimu za uhakika za mapato ya Serikali kutokana na Sekta ya Madini. Vilevile, Wakala utaendelea kuimarisha ukaguzi wa mazingira katika maeneo ya migodi mikubwa, ya kati na midogo. Fedha zilizotengwa kwa Wakala ni Shilingi bilioni 9.78.
Wakala wa Jiolojia Tanzania – GST
225. Mheshimiwa Spika, katika kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Madini, Serikali kupitia Wakala wa Jiolojia Tanzania itaendelea kukusanya taarifa za kijiosayansi na kuchora ramani. Kwa Mwaka 2013/14, Wakala utaendelea kufanya utafiti na kuchora ramani za kijiolojia, kijiokemia na kiojiofizikia. Utafiti huo utafanyika kwenye maeneo ya QDSs 267, 268, 269, 270/271 yaliyoko katika Wilaya za Kilwa, Liwale, Nachingwea na Ruangwa. Utafiti huo umelenga kubaini uwepo wa madini muhimu yakiwemo dhahabu, Platinum Group Metals (PGM) na shaba. Vilevile, Wakala utaendelea kuboresha mfumo wa kutunza

kumbukumbu za kijiosayansi na kukusanya taarifa za matetemeko ya ardhi katika vituo vilivyopo nchini. Fedha zilizotengwa kwa Wakala ni Shilingi bilioni 7.31.
226. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia GST itakamilisha kazi ya kutafuta madini ya kiteknolojia (technology metals) kwa kushirikiana na Taasisi ya BRGM ya Ufaransa. Mradi huu unakadiriwa kugharimu Euro milioni 3.054, sawa na Shilingi bilioni 6.48 na utakamilika mwishoni mwa Mwaka 2013/14. Utafiti huu utawezesha kutengeneza ramani mpya inayoonesha mahali yanapopatikana madini ya kiteknolojia. Kuhusu utafiti wa maeneo yenye jotoardhi, Wakala utaendelea na utafiti huo katika maeneo ya Ziwa Ngozi (Mbeya) na Kisaki (Morogoro). GST inafanya utafiti huo kwa kushirikiana na BGR ambayo ni Taasisi ya Jiolojia ya Ujerumani.
AJIRA NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU
227. Mheshimiwa Spika, Wizara inakabiliwa na uhaba mkubwa wa watumishi. Katika Mwaka 2013/14, Wizara inatarajia kuajiri jumla ya watumishi 589 wa kada mbalimbali. Kati ya hao watumishi 138 ni kwa ajili ya Wizara, TANESCO 233, TMAA 12, STAMICO 78, GST 53, MRI 32, TPDC 39 na REA 4. Jitihada mbalimbali zinafanyika kwa kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Sekretarieti ya ajira


ili kuweza kupata wataalam hao kwa wakati. Aidha, ili kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa Sekta za Nishati na Madini, Wizara imepanga kuwajengea uwezo jumla ya watumishi 150 kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu ndani na nje ya nchi, kipaumbele kitatolewa katika maeneo maalumu yakiwemo mafuta na gesi asilia, energy economics; oil and gas accounting and auditing; oil and gas legal regime and contract negotiations; energy management; geothermal; uranium; mineral economics; na diamond valuation and sorting. 
228. Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kutekeleza Mpango Kabambe wa Uendelezaji wa Rasilimali Watu (Marshall Plan on Capacity Building and Development in Oil and Gas Industry 2012-2016) ambao utawezesha Watanzania kati ya 50 hadi 100 kupata elimu katika ngazi ya stashahada, shahada, na shahada za uzamili na uzamivu kwenye fani za mafuta na gesi asilia.


D. USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
229. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua misaada na ushirikiano kutoka kwa washirika mbalimbali wa maendeleo kwa kipindi cha Mwaka 2012/13. Kwa niaba ya Serikali napenda kutoa shukrani kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China; Serikali za nchi za Brazil, Canada, Finland, Japan, Malaysia, Marekani, Norway, Oman, Qatar, Sweden, Trinidad & Tobago na 120
Ufaransa. Vilevile, natoa shukrani kwa Benki ya Exim ya China, Benki ya BADEA, Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (DBSA), Benki ya HSBC, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Umoja wa Ulaya (EU), pamoja na Taasisi na Mashirika ya AFD (Ufaransa), CIDA (Canada), ECDF (Korea Kusini), FINIDA (Finland), JICA (Japan), KfW (Ujerumani), MCC (Marekani), NORAD (Norway), OFID (Saudi Arabia), ORIO (Uholanzi) na Sida (Sweden), GEF, GVEP, IDA, IFC, UNDP, UNEP, UNIDO, UNICEF na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola.


E. SHUKRANI
230. Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Katibu Mkuu Bw. Eliakim C. Maswi kwa uchapakazi wake mahiri na ushirikiano mkubwa anaonipa. Aidha, nawashukuru Makamishna wote, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na watumishi wote wa Wizara kwa kutekeleza majukumu yao kwa bidii na maarifa.
231. Mheshimiwa Spika, napenda niwashukuru, Wenyeviti wote wa Bodi za Wakurugenzi, Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi Watendaji, Watendaji Wakuu, na Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kwa jinsi wanavyofanya kazi kwa kushirikiana na Wizara. Taasisi hizo zimefanya kazi kwa karibu sana na mimi, nawaomba muendelee kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na ueledi ili kuhakikisha Wizara yetu


inafikia malengo tuliyopewa na Serikali yetu ya kuwatumikia Wananchi wa Taifa hili ambao ndio waajiri wetu.
232. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa vyombo vya habari mbalimbali nchini kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa. Vyombo hivyo vimekuwa vikifuatilia na kutoa taarifa za shughuli zinazohusu Sekta za Nishati na Madini. Ushirikiano huu utaendelezwa na kuimarishwa zaidi kwa manufaa ya Taifa ili kuhakikisha kuwa umma unapata taarifa za kina na za uhakika. Aidha, Wizara yangu itaendeleza mawasiliano mbalimbali ili kuboresha utoaji wa elimu na taarifa kwa umma. Wizara pia itaendelea kutoa taarifa za shughuli zinazotekelezwa na Wizara kupitia vipindi vya Luninga, Redio, Tovuti (www.mem.go.tz) pamoja na majarida mbalimbali.
233. Mheshimiwa Spika, vilevile, natoa shukrani zangu za dhati kwa wananchi wanaoniletea taarifa mbalimbali kwa njia ya maongezi ya simu, ujumbe mfupi (sms) barua na barua pepe zikiwemo za hujuma za miundombinu ya umeme, rushwa na wizi ndani ya Wizara na Taasisi zake. Naomba wananchi waendelee kuniletea taarifa na ninawaahidi nitaendelea kuzifanyia kazi kwa uadilifu wa hali juu. Aidha, nawasihi wananchi kwa umoja wetu tuendelee kupambana na hujuma, wizi na rushwa katika Sekta za Nishati na Madini na kulinda miundombinu ya umeme.


234. Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa, naomba nimshukuru sana mke wangu Bertha Muhongo, wanangu Godfrey Chirangi, Dkt. Musuto Chirangi, Dkt. Bwire Chirangi na Rukonge Muhongo pamoja na familia yangu kwa ujumla kwa msaada mkubwa wanaonipa kutekeleza kazi zangu kwa ubora na ubunifu mkubwa.


E. HITIMISHO
235. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Mwaka 2013/14, inalenga: kuboresha upatikanaji wa umeme wa kutosha na wa uhakika; kuongeza watumiaji wa umeme vijijini na mijini; kuimarisha usimamizi wa Sekta za Nishati na Madini ili kuongeza mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa; kuongeza ajira; na kupunguza umaskini nchini.


MAKADIRIO YA MATUMIZI YA MAENDELEO
236. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka 2013/14, Wizara ya Nishati na Madini inaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 992,212,745,000 sawa na asilimia 90 ya Bajeti yote ya Wizara kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 558,345,745,000 sawa na asilimia 56 ni fedha za ndani na Shilingi 433,867,000,000 sawa na asilimia 44 ni fedha za nje.


MAKADIRIO YA MATUMIZI YA KAWAIDA KWA MWAKA 2013/14
237. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2013/14, Wizara ya Nishati na Madini inaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 110,216,384,000 sawa na asilimia 10 ya Bajeti yote kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo kati ya fedha hizo, Shilingi 14,607,640,000 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zake na Shilingi 95,608,744,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) ya Wizara na Taasisi zake.



MUHTASARI WA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA MWAKA 2013/14

A: BAJETI YA MAENDELEO
MAELEZO
KIASI
ASILIMIA
Fedha za Ndani
558,345,745,000
56.27
Fedha za Nje
433,867,000,000
43.73
Jumla ya Bajeti ya Maendeleo
992,212,745,000
100.00
B: BAJETI YA MATUMIZI YA KAWAIDA
Mishahara
14,607,640,000
13.25
Matumizi Mengineyo
95,608,744,000
86.75
Jumla Matumizi ya Kawaida
110,216,384,000
100.00
C: JUMLA YA BAJETI YOTE
Bajeti ya Maendeleo
992,212,745,000
90.00
Bajeti ya Matumizi ya Kawaida
110,216,384,000
10.00
JUMLA KUU
1,102,429,129,000
100.00



Pakua/Download Hotuba.pdf

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment