Zaidi ya Nusu ya Wafungwa wa Guantamano wagoma kula

Wafungwa wa Guantamano wagoma kula chakula




Afisa mmoja wa jeshi la Marekani amesema kuwa zaidi ya nusu ya wafungwa wanaoshikiliwa katika jela ya Guantanamo wako katika mgomo wa kula wakilalamikia mazingira ya jela hiyo na kufungwa kwao bila ya kushtakiwa au kupatikana na hatia kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.

 Luteni Kanali Samuel House wa jeshi la Marekani amesema kuwa wafungwa 84 kati ya jumla ya wafungwa 166 wanaoshikiliwa katika jela hiyo ya kutisha inayosimamiwa na Marekani wanakataa vyakula vyote na wameainishwa kama wafungwa walioko katika mgomo wa kula.

 House amesema wafungwa 16 katika 84 waliosusia chakula hivi sasa wanalishwa kwa nguvu kwa kutumia mipira ya kupitia puani huku watano wakiwa wamelazwa hospitalini.  Mfungwa Shaker Aamer ni miongoni mwa wafungwa wa Guantanamo waliogoma kula chakula ambaye amekuwa katika jela hiyo kwa miaka 11 sasa.

CHANZO: IRIB
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment