Utafiti wa Kituo cha Habari cha Marekani CNN, umebaini kwamba Tanzania ni nchi ya sita barani Afrika kwa watu wake kunywa pombe chafu (mataputapu).
Utafiti huo wa Machi 23 mwaka huu, ulibaini kwamba Uganda inaongoza kwa kunywa pombe chafu maarufu kama Luwombo kwa asilimia 14.52 ikifuatiwa na Rwanda kwa asilimia 6.44.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Tanzania inashika nafasi ya tano kwa kuwa na asilimia 4.52, ikiwa nyuma ya Burundi yenye asilimia 5.07.
Ivory Coast imekuwa nyuma ya Tanzania kwa kuwa asilimia 3.55 huku Tanzania ikiipiku Burkina Faso iliyoambulia asilimia 3.77, kwa wa watu wake kunywa pombe chafu.
Ripoti ya utafiti huo ilisema asilimia kubwa katika nchi za Afrika, wanapenda kutumia pombe kali kwa lengo la kuondoa msongo wa mawazo.
Mtaalamu wa masuala ya afya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Figo, Dk Francis Fulia aliwataka wananchi waache kunywa pombe hizo kwa sababu zinatengenezwa katika mazingira ambayo si salama.
Alisema hali hiyo inahatarisha usalama wa afya zao.
“Watanzania waachane na matumizi ya pombe hizo kwa kuwa zinatengenezwa katika njia sizisokuwa salama, pia zinasababisha magonjwa mbalimbali kama figo, ini, moyo ,kupata upofu ama kupoteza maisha,” alisisitiza.
Dk Fulia pia alipinga juu matumizi ya pombe katika kuondoa msongo wa mawazo.
“Pombe haina uhusiano wowote katika kupunguza mawazo, inatumika katika kumsahaulisha mtu tatizo lake kwa kipindi kifupi” alisema.
Aliongeza kuwa njia salama ya kuepuka msongo wa mawazo ni kusuluhisha kwa kutafuta chanzo cha msongo huo au kupata ushauri nasaha kutoka katika vituo mbalimbali vya afya.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya wananchi kujitumbukiza katika unywaji pombe uliokithiri ikiwamo kunywa pombe aina ya virobo gongo na pombe nyingine.
chanzo:mwananchi
chanzo:mwananchi
0 comments:
Post a Comment