MRIPUKO MKUBWA WAITIKISA DAMASCUS


File photo shows Syrian men inspecting the scene of a car bomb explosion in Jaramana district in the capital, Damascus.



Bomu lililotegwa kwenye gari limeripuka katika mji mkuu wa Syria, Damascus na kuua watu kadhaa.



Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa bomu hilo liliripuka jirani na Wizara ya Mambo ya ndani katika wilaya ya kati ya al-Marjeh leo Jumanne. 


Jana Jumatatu, mabomu mawili yaliripuka katika kitongoji cha al-Mazzeh mjini humo. Shambulizi hilo lilikuwa limeulenga msafara wa Waziri Mkuu Wael Nader al-Halqi. 

Waziri Mkuu huyo alinusurika katika shambulizi hilo lakini walinzi wake watatu na dereva wake walipoteza maisha.


Mripuko kama huo ulimuua Mohammad Abdul-Wahab Hassan,afisa mwandamizi katika Wizara wa Umeme wa nchi hiyo mnamo Aprili 24.



Mnamo Aprili 23, watu wenye silaha walifanya shambulizi jingine la bomu mjini Damascus, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa. Mripuko huo ulisababisha uharibifu wa mali na magari kadhaa.


Siku moja kabla, mripuko wa bomu uliutikisa mji wa al-Mleiha jirani na Damascus, na kuwajeruhi watu wengi. Mashambulizi hayo yanaelezwa kuvilenga vituo vya ukaguzi vya jeshi la Syria.



Syria imekuwa katika mzozo mkubwa tangu Machi 2011, na watu wengi, wakiwemo maafisa wa kijeshi, wamepoteza maisha. 

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment