Wapalestina wakijaribu kuzima moto baada ya ndege za Israeli kuushambulia mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza. |
Mashambulizi ya ndege za Israeli magharibi mwa Ukanda wa Gaza yamepoteza maisha ya Mpalestina mmoja na kujeruhi wengine kadhaa, wakati huu ambapo utawala wa Tel Aviv umezidisha mashambulizi kwenye eneo hilo.
"Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 20 ameuawa na mwengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya ndege za Israeli katika kambi ya wakimbizi ya Shati magharibi mwa mji wa Gaza," msemaji wa wizara ya Afya ya Gaza Ashraf al-Qudra alisema.
Jeshi la Israeli limethibitisha kufanya shambulizi hilo.
Siku ya Jumapili, ndege za Israeli zilifanya mashambulizi matatu katika maeneo mbalimbali katika mji wa kusini wa Khan Younis na jirani na mji wa Rafah kusini mwa Gaza.
Mapema Aprili, kwa mara ya kwanza utawala wa Tel Aviv ulifanya mashambulizi ya ndege kwenye ukanda wa Gaza tangu kufikiwa kwa makubaliano ya kukomesha mapigano ya siku nane kwenye maeneo ya Palestina Novemba 2012.
Katika mapiganao hayo yaliyoanza Novemba 14 mpaka 21, kiasi cha Wapalestina 177 waliuawa na wengine wapatao 1200 wakajeruhiwa.
0 comments:
Post a Comment