![]() |
Rais wa Tunisia ememteua waziri wa mambo ya ndani Ali Larayedh (pichani) kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo leo Februari 22, 2013. |
Rais wa Tunisia Moncef Marzouki amemteua Waziri wa mambo ya Ndani Ali Larayedh kuwa waziri mkuu mpya kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Hamadi Jebali mapema wiki hii.
Sasa Larayedh atakuwa na siku 15 za kuunda serikali mpya na kuwasilisha mpango yake mbele ya mkuu wa nchi, alisema Mancer na kuongeza kuwa Marzouki amemtaka kufanya hivyo "haraka iwezekanavyo kwa sababu nchi haiwezi tena kuendelea kusubiri."
Chama tawala Ennahda - ambacho kimeahidi kujenga serikali jumuishi - kilimpendekeza Larayedh baada ya Baraza lake la Shura kumchagua wakati wa usiku. Na kikiwa na wabunge 89 hakikupata ugumu wa kupata kura 109 zinazotakiwa kumpigia kura.
Waziri huyo mwenye umri wa miaka 57, ambaye aliwahi kufungwa jela na kuteswa chini ya utawala wa Zine El Abidine Ben Ali, amekuwa waziri wa mambo ya ndani tangu kuangushwa utawala wa Ben Ali mwaka 2011 na anatazamwa kama mwansiasa mwenye kusikiliza.
Uteuzi huo umekuja siku kadhaa baada ya Jebali kutangaza kuwa amejiuzulu kufuatia kushindwa kuunda serekali mpya ya wataalamu iliyotarajiwa kuiokoa nchi kutokana na mgogoro wa kisiasa uliokuwa ukiinyemelea.
Mgogoro huo uliibuka kutokana na hasira za wananchi kufuatia kuuawa mwanasiasa wa mrengo wa kushoto na mkosoaji mkubwa wa serikali Chokri Belaid. Mauaji hayo yalisababisha maandamano makubwa nchi nzima, huku makao makuu ya chama tawala cha Ennahda yakishambuliwa katika miji kadhaa.
Makundi ya Upinzani ymekituhumu chama cha Ennahda kuhusika na mauaji hayo. Lakini, kiongozi wa chama hicho, Rashid al-Ghannushi alilaani kitendo hicho na kukanusha tuhuma hizo.
0 comments:
Post a Comment