
Afisa mmoja wa Afya kutoka wilaya ya Nyando katika Kaunti ya Kisumu nchini Kenya jana alifikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kumbaka mgonjwa.
Bwana David Wakenga Okoth, afisa afya katika kituo cha Afya cha Annex Health Center katika wilaya ya Nyando anatuhumiwa kwa kumdhalilisha kijinsia mgonjwa katika kliniki hiyo tarehe 3 Februari mwaka huu.
Kwa mujibu wa mashahidi, Wakenga alitumia cheo chake kumbaka mgonjwa wake. Mahakama ilielezwa kwamba siku hiyo ya tukio, mgonjwa huyo alikwenda kituoni hapo kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake ambapo mtuhumiwa alimlazimisha kufanya naye mapenzi na kutishia kumuua iwapo angeripoti tukio hilo.
Mbele ya mahakama ya Nyando, David alikanusha mashitaka hayo na kuachiwa kwa dhamana.
CHANZO: THE KENYAN DAILY POST
0 comments:
Post a Comment