Mvua kubwa na nzito imesababisha mafuriko nchini Ugiriki na kaskazini mwa Italia ikiambatana na mikondo ya maji yenye uwezo wa kusomba magari. mwanamke mmoja amefariki dunia kwa mshtuko baada ya kukwama katika gari yake iliyokuwa imezungukwa na mikondo ya maji.
mjini Athens mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 amefariki kwa shambulio lamoyo lililosababishwa na mshituko baada ya kukwama ndani ya gari iliyokuwa ikisukumwa na maji. Mwanamke mwingine aliokolewa kutoka kwenye gari pindi mikondo mikubwa ya maji ilipokuwa ikiyasukuma magari.
Mamlaka zililazimika kufunga barabara katika maeneo yenye mabonde ya Athens na vituo viwili vya stesheni kwa sababu za kiusalama kutokana na maji yenye tope zito kuanza kusomba magari, pikipiki hata magari yaliyoegeshwa kando kando ya barabara.
Mafuriko hayo yalisababisha kukatika umeme mara kwa mara wakati wa usiku.

Mvua ya jana Ijumaa ndiyo mvua kubwa zaidi kunyesha katika kipindi cha miaka 50 mpaka 60, ilisema idara ya hali ya hiwa ya Ugiriki. Katika maeneo mengine ya mji, zaidi ya mm100 zilinyesha wakati wa mvua hiyo iliyodumu kwa muda wa saa tano, kiwango ambacho ni zaidi ya wastani wa unyeshaji wa mwezi mzima.
![]() |
| Mfanyakazi wa Manispaa akifanya kazi kwenye barabara iliyoathiriwa na mafuriko katikati mwa mji wa Athens Februari 22, 2013. |
Huko Catania, kwenye kisiwa cha Sicily nchini Italia, shule zilifungwa na safari za ndege zilielekezwa kutua katika uwanja wa Palermo kutokana na mafuriko.
Mamia ya askari wa zima moto na wafanyakazi wa idara ya uokozi walitumika ili kuwasaidia wale walionasa katika mafuriko. Mtu mmoja anaripotiwa kujeruhiwa na mwingine kupotea baada ya kubebwa na maji.
Imeripotiwa kuwa kiasi cha lita 50 kwa kila mita moja ya mraba kilinyesha ndani ya nusu saa katika kisiwa cha Sicily jana Ijumaa.

0 comments:
Post a Comment