
China imekiri kuwepo kwa kile kinachoitwa kama "vijiji vya kansa" baada ya wananchi kuwa na wasiwasi kwa muda mrefu kuhusu athari ya uchafuzi wa mazingira kwenye afya zao.
Wizara ya mazingira ilitoa ripoti yake mpya kabisa jana Ijumaa iliyokuwa na kichwa cha habari "Ulinzi na udhibiti dhidi ya hatari zilizoletwa na kemikali kwenye mazingira katika kipindi cha miaka mitano (2011-2015)".
"Kemikali zenye sumu zimesababisha madhara kwenye mazingira yanayohusiana moja kwa moja na maji na uchafuzi wa hewa," ilisema ripoti hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kemikali hizo zinaweza kusababisha hatari ya muda mrefu kwenye afya ya binadamu na kusababisha moja kwa moja kile kinachoitwa "vijiji vya kansa".
"Kuna kadhia kubwa kabisa na za hatari za afya na matatizo ya kijamii kama kuibuka kwa vijiji vya kansa kwenye baadhi ya mikoa," ilisema.
Kwa kujibu wa wanaharakati, kiwango cha ugonjwa wa kansa kimeongezeka kwenye vijiji vilivyo jirani na viwanda na mito iliyochafuliwa.
Ghadhabu ya wananchi imekuwa ikiongezeka katika nchi hiyo juu ya uchafuzi wa hali ya hewa na uchafu unaotoka viwandani na vyombo vya habari vimekuwa vikitangaza sana kuhusu hali ya kile kinachoitwa kama "vijiji vya kansa".
Mwezi uliopita, mji wa Beijing na miji mingine, ilifunikwa na wingu la moshi mzito lililopita viwango vya zamani vinachokuliwa na shirika la afya duniani kwa ni sumu.
Mwezi Februari mwaka jana, vyombo vya habari vya serikali vilitangaza mipango ya kupunguza viwango vya uchafuzi wa hewa katika mji mkuu Beijing kwa asilimia 30 ifikapo mwaka 2020 kwa kuchukua hatua mbalimbali kama vile kuondosha magari makongwe, kuhamisha maeno ya viwanda na kupanda misitu mipya.
0 comments:
Post a Comment