![]() |
| Watuhumiwa sita waliotiwa mbaroni kwa kumnajisi mke wa mtu katika basi la abiria nchini India |
Watu sita wametiwa mbaroni kwa kosa la kumnajisi abiria kwenye basi linalofanya safari za mikoani nchini India. Hayo yamesemwa leo na polisi ya India. Tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki chache tu baada ya genge la wanaume sita kumnajisi mwanachuo wa kike aliyekuwa na umri wa miaka ishirini ndani ya basi huko New Delhi na kusababisha kifo chake hivi karibuni.
Kifo cha mwanachuo huyo aliyekuwa akisomea taaluma ya udaktari kilisabbisha hasira kubwa za wananchi wa India hususan katika mji wa New Delhi na kuibua pia maandamano makubwa nchini humo. Mwanamke huyo mwingine aliyenajisiwa na kundi la watu kwenye basi la abiria, ametajwa kuwa ni mke wa mtu na alinajisiwa juzi Ijumaa. Alikutwa na maafa hayo wakati alipopanda basi akielekea kwa wakwe zake wanaoishi katika jimbo la Punjab.
Mwanamama huyo alitekwa nyara baada ya kupanda basi na kisha genge hilo la wahuni likampelekea hadi katika wilaya inayopakana na mji wa kidini wa madhehebu ya Makalasinga katika mji wa Amritsar. Hayo yamesemwa na polisi wa eneo hilo Raj Jeet Singh.
Singh ameongeza kuwa wanaume hao watano walijiunga na dereva na kondakta wa basi hilo ambao walimpeleka mwanamke huyo sehemu isiyojulikana, baadae wakamnajisi usiku kucha na kisha wakamtupa karibu na kijiji wanapoishi wakwe zake jana asubuhi. Polisi imesema kuwa wanaume sita kati ya saba waliohusika katika jinai hiyo wametiwa mbaroni kwa kosa la kumnajisi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29.
CHANZO: IRIB

0 comments:
Post a Comment