KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Shafii Yatera (40) ameuanza vibaya Mwaka 2013 baada ya kusherekea Mwaka Mpya akiwa Gereza Kuu la Karanga mjini Moshi.
Yatera alipandishwa kizimbani juzi mbele ya Hakimu mkazi, Sophia Masati, akikabiliwa na tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Msasani.
KADA huyo ndiye ambaye katika uchaguzi mkuu wa 2010 alichuana na mbunge wa sasa wa Jimbo la Mwanga ambaye pia ni waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushika nafasi ya pili.
Akisomewa mashtaka yake, Wakili wa serikali Kanda ya Moshi, Oscar Ngole alidai kuwa Novemba 1, 2012 MSHTAKIWA ALIMWINGILIA KIMWILI MWANAFUNZI HUYO WA KIDATO NNE KINYUME CHA SHERIA.
Wakili huyo alidai kuwa kitendo alichokifanya mtuhumiwa huyo ni kunyume cha kifungu 130 (2) (e) na 131 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, adhabu ya kosa hilo ni kifungo cha miaka 30 jela. Hata hivyo kada huyo wa Chadema ambaye ni mkazi wa Pasua, mjini Moshi alikanusha mashtaka hayo, lakini upande wa mashtaka ukaiomba mahaka kuzui dhamana kwa sababu za kiupelelezi.
Wakili Ngole alidai kuwa endapo mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana ataathiri uchunguzi wa kesi hiyo kwa kile kinachodaiwa amekuwa akishawishi mwanafunzi huyo kutokutoa ushirikiano kwa polisi.
Hakimu Masati anayeisikiliza kesi hiyo allikubali ombi hilo la upande wa mashtaka na kuamuru mshtakiwa apelekwe rumande katika Gereza Kuu la Karanga hadi Januari 14, 2013 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Source: Mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment