![]() |
| Mashambuli yaliyofanywa leo na Wazayuni kwenye mji wa Gaza. |
Leo Wapalestina wengine watano wamekufa katika wimbi la mashambulizi ya angani dhidi ya Ukanda wa Gaza. .
"Wavamizi wa Kiisrael wametekeleza zaidi ya mashambulizi 20 ya anga na kuyashambulia makao makuu ya polisi na usalama katika Ukanda wa Gaza. Mpaka sasa watu sita wameuawa, akiwemo kamanda Ahmad Jabari," msemaji wa wizara ya mambo ya ndani, Islam Shahwan alisema.
Ifuatayo ni radiamali kutoka maeneo mbalimbali duniani kuhusu mauaji hayo na mashambulizi ya anga yanayoendelea.
| Misri |
Katika maelezo yake, Amr, aliionya Israel dhidi ya "ongezeko lolote la mashambulizi na taathira zake mbaya zinazoweza kuathiri uthabiti wa eneo hilo".
Wakati huo huo, chama cha Rais Mohamed Morsi cha Muslim Brotherhood, kimewataka Waarabu kuisusia Israel, huku chama cha Freedom and Justice Party (FJP) kikionya kwamba huwenda Misri isivumilie tena kuona Wapalestina wakishambuliwa.
Chama hicho cha FJP mashambulizi ya anga yaliyomuua Jabari mjini Gaza yalihitaji "hatua ya haraka ya Waarabu na Jumuia ya Kimataifa ili kusitisha ukatili huo".
Israel "haina budi kuzingatia mabadiliko yaliyotokea katika nchi za eneo la Arabia na hususan Misri," kilisema. Misri "haitakubali Wapalestina kuandamwa na dhulma za Israel, kama zamani".
Morsi, muungaji mkono mkubwa wa Wapalestina kabla ya ushindi wake wa mwezi Juni, alikuwa akitarajiwa kuondoa mzingiro uliowekewa Ukanda wa Gaza ambayo inapakana na Misri, lakini serikali yake imeshindwa kutekeleza ahadi zake.
Chama cha Brotherhood, ambacho kina mafungamano ya karibu na harakati ya Hamas, kimeitisha "ususiaji wa kiuchumi" na kuwahamasisha wananchi "ili kuunga mkono chaguo hilo la ususiaji na upinzani".
| Umoja wa Mataifa |
"Katibu Mkuu ametaka kusitishwa mara moja mapigano," msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema huku akiongeza kuwa huo ndio msimamo wa Ban Ki-moo.
"Pande zote mbili zinapaswa kufanya kila kitu kuepusha hujuma zaidi na wanatakiwa kuheshimu wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa kuhakikisha kuwa raia wanalindwa nyakati zote," aliwaambia waandishi wa habari.
| Uingereza |
"Tunazitambua ripoti za kifo cha kamanda mwandamizi wa Hamas Ahmed Jabari," Ofisi ya Wizara ya Mambo ya ndani ilieleza katika ujumbe uliowekwa kwenye mtandao wa Twitter.
"Tunaendelea kuzitaka pande zote kujizuia ili kuepusha hatari ambayo haitakuwa na maslahi kwa yeyote."
Siku ya Jumanne Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza, William Hague, alionya kwenye Mkutano wa pamoja wa EU-Arab League mjini Cairo kuwa dunia iko "katika hatari iliyolala kuelekea kwenye mgogoro mkubwa" iwapo hapatakuwepo na maendeleo katika mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati.
| Marekani |
"Tunafuatilia hali hiyo kwa karibu. Tunasimama pamoja na washirika wetu wa Israel katika haki yao ya kujilinda dhidi ya ugaidi," alisema Luteni Kanali Stephen Warren.
Siku ya Jumatatu, mshauri wa Rais Barack Obama wa usalama wa kitaifa, Tom Donilon, alikutana na mwenzake wa Israel, Yaakov Amidror, katika ikulu ya White House katika wakati ambapo wakijipanga kujibu mashambulizi yaliyokuwa yakihanikiza kwenye mpaka na ardhi ya Palestina.
KABUGA KANYEGERI kwa msaada wa mashirika ya habari

0 comments:
Post a Comment