NA KABUGA KANYEGERI
Harakati ya Kipalestina ya Hamas imesema kuwa inarusha makombora kuelekea Tel Aviv katika kujibu mashambulizi ya Israel ambayo yamegharimu maisha ya wakazi 13 wa Gaza siku ya Jumatano.
Mapema, kombora kutoka Palestina lilikipiga kiwanda kimoja katika mji wa kusini mwa Israel wa Ashkelon na kuwaua watu watatu.Wakati huo huo, Wapalestina wanafanya mazishi ya kiongozi wa Brigedi ya Izzeddin Qassam, Ahmed al-Jabari aliyeuawa katika shambulizi la Israel kwenye gari lake siku ya jumatano.
Wapalestina watatu waliuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Israel kwenye mji wa kusini wa Khan Yunis katika Ukanda wa Gaza leo Alhamisi, na kufanya idadi ya watu waliouawa kufikia 13 tokea Jumatatno.
Vile vile zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa.
Haya yanatokea baada ya baraza la mawaziri la Israel kumpa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na mawaziri wa vita na wa mambo ya nje mamlaka ya kupanua na kuzidisha hujuma za mashambulizi dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa mamlaka hayo mapya, viongozi wa Israeli hawahitaji ithibati na ruhusa ya baraza la usalama kwa hatua yoyote watakayoamua kuichukua dhidi ya eneo hilo la Pwani.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice ametetea hujuma za mashambulizi ya Israel dhidi ya ukanda wa pwani wa Palestina, ambao umekuwa chini ya mzingiro wa Wazayuni kwa miaka mitano.

0 comments:
Post a Comment