![]() |
| Kijana wa Kimisri akitupa moto kwenye jengo moja wakati wa vurugu zilizotokea mjini Cairo, Novemba 22, 2012. |
Wamisri wenye hasira wayachoma moto makao makuu ya chama cha Rais Mohamed Morsi katika miji mitatu wakipinga hatua ya rais huyo kufanya mabadiliko ya kikatiba yanayompa mamlaka yasiyokuwa na kikomo.
Ofisi za chama cha Freedom and Justice Party (FJP), tawi la kisiasa la Muslim Brotherhood, leo ijumaa zimechomwa moto katika miji ya Suez, Ismailiya na Port Said, kwa mujibu wa televisheni ya Serikali ya Misri.
Ofisi za FJP katika mji wa Mediterranean wa Alexandria nazo pia zilishambuliwa, jambo lililopelekea kutzuka kwa mapambano baina ya waandamani na wafuasi wa Mursi.
Morsi alitoa azimio jipya ambalo, hakuna chombo chochote cha kisheria kitakachoweza kulivunja Bunge ambalo kwa sasa linaandika katiba mpya.
Azimio hilo linamruhusu rais kuchukua "uamuzi au hatua yoyote ili kuyalinda mapinduzi." Vilevile kwa mujibu wa azimio hilo, uamuzi na sheria yoyote itakayotolewa na rais ndiyo "ya mwisho na haiwezi kukatiwa rufaa."
Uamuzi huo ulisababisha upinzani kuitisha maandamani ya nchi nzima ambao waliliita azimio hilo kama "mapinzfuzi dhidi ya sheria" na "pigo kubwa dhidi ya mapinduzi ambalo lingekuwa na taathira mbaya."
Mohamed ElBaradei, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na ambaye aliyewahi kuwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Nguvu za Nyukila Duniani, alisema kuwa Mursi "amenyakua mamlaka yote dola na kujichagua kuwa fir'auni mpya."

0 comments:
Post a Comment