MJI WA GOMA WAANGUKIA MIKONONI MWA WAASI

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa na Polisi wa Kongo wakiwa wamesimama mjini Goma, jirani na mpaka wa Rwanda, muda mfupi kabla ya mji huo kuangukia mikononi mwa Waasi wa M23.

Waasi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameidhibiti Goma, ambao ni mji muhimu katika eneo lenye madini mengi la nchi hiyo, baada ya siku kadhaa za mapigano baina ya vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na kundi la waasi la M23. Hayo yameelezwa na msemaji wa waasi hao.

Waasi hao waliokuwa wamejizatiti kwa silaha nzito walitembea katikati ya mji huo wenye wakaazi milioni moja, bila kukabiliwa na upinzani wowote, huku walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwatazama na kusalimiwa na kikundi kidogo cha wakaazi.
  
"Mji wa Goma ulianguka kwenye majira ya saa 5:33 kwa saa za Kongo, licha ya mashambulizi ya helkopta na silaha nzito nzito zilizotumiwa na jeshi la Kongo (FARDC) mji huu umeangukia mikononi mwetu," msemaji wa waasi hao, Vianney Kazarama, aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu.

Waasi hao walifanikiwa zaidi baada ya kuushikilia uwanja wa ndege za jeshi mjini Goma.

"Uwanja wa ndege uko chini ya udhibiti wa M23 (Waasi)," afisa mmoja alisema kwa sharti la kutotajwa jina lake.

Mapema, Lambert Mende, msemaji wa serikali, alionya juu ya athari zitokanazo na waasi wa M23 kuudhibiti mji huo, huku akiilaumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao.

"Kama Goma ikianguka, kutazuka matatizo mengi sana. Kimsingi tunakataa kuzungumza nao  (M23). Kwa sababu tukifanya hivyo, tutakuwa tumeuondoa uhusika na uwajibikaji wa Randa."

Congo na Rwanda zimewahi kupigana mara mbili, vita ya karibu kabisa ikiwa ni ile iliyofikia tamati mwaka 2003 baada ya kudumu kwa takriban miaka sita.

Kundi la M23 linaongozwa na askari walioasi miezi nane iliyopita, wakidai kuwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikiuka makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2009 yaliyokusudia kuwajumuisha katika jeshi.

Hata hivyo, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaona kwamba Randa, ambayo imekuwa ikiingia mara kwa mara Kongo kwa muda wa miaka 18, iko nyuma ya uasi huu.

Kukamatwa kwa Goma kunaweza kumtikisa Rais Joseph Kabila, ambaye amekuwa akijitahidi kujaribu kuleta amani ya nchi yake.

Nchi hiyo kubwa ya Afrika ya Kati imekuwa katika vita vilivyoiyumbisha baina ya mwaka 1994 na 2003 ambavyo vimeuwa takriban watu milioni 5. Maeneo mengi ya Mashariki bado yanakabiliwa na migogoro mbalimbali inayosababishwa na uwepo wa makundi mbalimbali ya waasi, licha ya juhudi zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kujaribu kuwadhibiti.

Umoja wa Mataifa una wanajeshi wapatao 6,700  wa kulinda amani, wakiwemo askari 1400 waliopo Goma na maeneo ya jirani.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment