KESI YA LEMA-JAJI OTMAN CHANDE AJITOA KUISKILIZA

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman


Rufaa ya mbunge wa jimbo la arusha mjini, Godbless Lema ambayo awali ilikuwa na dosari sasa itasikilwa na jaji Bernard Luanda. 

Mabadiliko hayo yamekuja baada ya jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande kujitoa kusikiliza rufaa hiyo zikiwa zimebaki sita kusikizwa. Rufaa hiyo inatarajiwa kusikizwa December 4 Mahakama ya rufaa, Kanda ya daR es salaam baada ya kurekebiswa dosali za kisheria ambazo ziligundulika mwanzo.
   
Kabla Salum Massati,na Natalia Kimaro walikuwa wakiongozwa na jaji Othman chande katika kuisikiliza kesi hiyo .

Lakini kutokana na kujitoa jaji chande pengo hilo litazibwa na jaji Lunda alisema Method Kimomogoro wakili wa lema


“Kisheria hili ni swala la kawaida” alisema wakili wa lema

Lakini wakili wa Dk.Batrida Buliani amesema hajapata taarifa yoyote kuwa jaji mkuu amejitoa kwenye kesi hiyo na pia huo sio utaratibu wa mahakama wa kutoa taarifa.


Rufaa hii imekuja baada ya Lema kuvuliwa ubunge April 5, 2012 mahakama kuu kanda ya Arusha


Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment