
Akizungumza wakati alipokutana na wakimbizi katika kambi ya Yida karibu na eneo la mpaka wa nchi hiyo na Sudan, Guterres amesema mbali na kuwa kambi hiyo iko karibu na eneo la mapigano, kila kitu hapo lazima kiingizwe kwa kutumia ndege.
Ametaja hali aliyoiona katika kambi hiyo kuwa ni 'mgogoro wa wakimbizi waliosahaulika'. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa raia 60 elfu waishio katika kambi ya Yida kuhama na kuingia ndani zaidi ya Sudan Kusini.
Kambi ya Yida iko katika jimbo la Sudan Kusini la Unity State ambapo umbali wake kutoka mpaka na Sudan ni kilomita 12. Wakimbizi hao wamekimbia mapigano kati ya jeshi la Sudan na waasi katika jimbo la Kordofan Kusini.
0 comments:
Post a Comment