![]() |
Hamad Rashid-Mbunge Wa Wawi(CUF) |
Hamad Rashid mbunge wa wawi kwa tiketi ya chama cha wananchi(cuf) aangukia pua, ni baada ya mahamaka kuu kutupilia mbali dai lake la kuwa chama hicho kilifanya kikao cha baraza kuu ambacho kilizuiliwa na amri halali ya mahakama, Hamad Rashid ambaye anatoka kwenye jeraha la kupoteza mke wake mdogo siku mbili zilizopita leo ameumizwa tena mahakamani, taarifa za bwana Hamad Rashid kushidwa kesi hiyo zilisambazwa na naibu katibu mkuu wa cuf bara Mh Julius Mtatiro kama ifuatavyo
“TUMESHINDA KESI YA AWALI AMBAYO MHE. HAMAD RASHID NA WENZIE WALIKISHTAKI CHAMA.
Hukumu imemalizika muda so mrefu hapa mahakama kuu.
Hoja zote za akina Hamad Rashid zimetupiliwa mbali.
Mahakama imejiridhisha kwamba, amri ya mahakama kuu ya kusitisha kikao cha BARAZA KUU kilichowafukuza uanachama HR na wenzake wanne haikufikishwa kwa chama kwa hivyo kikao husika kilikuwa halali.
Hii ina maana kwamba OMBI la Hamad Rashid na mawakili wake kuwa WAJUMBE WOTE WA BARAZA KUU la CUF wafungwe jela kwa kukiuka amri ya mahakama limetupiliwa mbali.
Kesi ya msingi ambayo HR na wenzake waliifungua kupinga uhalali wa KAMATI YA MAADILI YA CHAMA itasikilizwa tarehe 28/01/2013 ambapo mawakili wa chama watapangiwa tarehe YA kuleta hoja za kutaka kesi ya msingi ifutwe kwa kuwa taratibu zote zilifuatwa na walifukuzwa kihalali na kwa kuzingatia katiba ya chama.
Chama chetu kimefurahishwa na uamuzi huu kwani unaonesha namna ambavyo hatukukurupuka.
Chama pia kinatoa pole kwa mhe. Hamad Rashid kwa kufiwa na mkewe mdogo jana, tutashiriki katika kutoa pole na mazishi pia. Tunaamini haya ya kimahakama yana nafasi yake na ya kibinadamu hayakwepeki.”

Kwa niaba ya Wa Zanzibar,Tunatowa mkono wa pole kwa Mhe Hamad rashid kwa kufiliwa na Mke wake mdogo.
ReplyDeleteKwa kuonesha kuwa tupo pamoja naye katika Msiba huo, Katibu Mkuu wa CUF ambaye pia ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad atashiriki katika Maziko hayo.
Mungu amlaze mahala pema peponi - Amin