Ukanda wa Gaza huko Palestina unakabiliwa na mashambulizi makali na jeshi la utawala katili wa Israel huku viongozi wa utawala huo wakisisitiza kuwa mashambulizi mapya dhidi ya watu wa eneo hilo yatakuwa makali zaidi na kuenea katika eneo lote la Gaza.
Ndege za utawala wa Kizayuni wa Israel zilianza mashambulizi makali dhidi ya Ukanda wa Gaza Jumatano iliyopita na hadi sasa zimeua shahidi Wapalestina wasiopungua 19.
Mwishoni mwa mwaka 2008 Israel ilifanya mashambulizi makali ya anga, nchi kavu na baharini dhidi ya watu wa Gaza na kusababisha maafa makubwa. Wakati huo wanasiasa wa chama cha Kadima wa Israel walitumia mashambulizi hayo kama chombo cha kujipatia jina na kujipigia debe katika uchaguzi wa bunge.
Maafa makubwa ya vita hivyo vya siku 22 yalimlazimisha Waziri Mkuu wa wakati huo wa Israel Ehud Olmet kubanduka madarakani na walimwengu wakamtambua kama mtenda jinai za kivita. Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa Waziri Mkuu wa sasa wa Israel Benjamin Netanyahu pia anafuata njia hiyo hiyo na anataka kushinda uchaguzi ujao wa bunge kwa gharama ya damu za wananchi wa Gaza. Hususan ikitiliwa maanani kwamba uchaguzi wa bunge la Israel umepangwa kufanyika mwezi Januari mwakani.
Tokea mwanzoni mwa mashambulizi ya Gaza ilionekana wazi kuwa Netanyahu anataka kutumia vita vya sasa katika propaganda za uchaguzi wa bunge. Mashambulizi ya sasa ya Gaza yanakamilisha yake ya siku 22 na kama ilivyodaiwa kwenye mashambulizi ya kabla yale, nafanyika kwa lengo eti la kulipiza kisasi dhidi ya Brigedia ya Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Hamas na yameanza kwa kumuua kigaidi kamanda wake Ahmad Jaabari.
Inaonekana kuwa malengo mengine ya mashambulizi ya sasa ni pamoja na kuzipotosha na kuzishughulisha fikra za ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel na matatizo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya ndani na pia kuzuia juhudi za Palestina za kutaka kutambuliwa rasmi kama nchi huru katika Umoja wa Mataifa.
Hitilafu zilizopo kati ya wanasiasa wa utawala ghasibu wa Israel zimepamba moto sana kwa kadiri kwamba duru za kisiasa zinazitaja kuwa ni vita vikubwa vya kuwania madaraka ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu dola hilo bandia liundwe.
Katika upande mwingine mashambulizi ya sasa ya Israel katika Ukanda wa Gaza ni mtihani mkubwa kwa Umoja wa Mataifa, serikali zilizochukua madaraka za Kiarabu kupitia njia ya mapinduzi ya wananchi na ulimwengu mzima wa kiarabu kwa ujumla. Kwani hapana shaka kuwa macho ya walimwengu hususan watu wa Mashariki ya Kati yanasubiri kuona jibu la pande hizo mbele ya mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wa Gaza.
Tangu mwaka 2006 wakati Hamas iliposhinda uchaguzi mkuu wa Palestina na kushika madaraka, eneo la Gaza limekuwa likikabiliwa na njama za aina mbalimbali na mashambulizi ya Israel yanayoungwa mkono na nchi za Magharibi hususan Marekani. Eneo hilo limezingirwa kutoka pande zote za anga, nchi kavu na baharini. Hata hivyo watu wa Gaza wameendelea kuwa ngangari na nembo ya ushujaa na kusimama kidete.

0 comments:
Post a Comment