WAZIRI ANASURIKA KUUAWA
WAZIRI wa Uvuvi nchini Kenya, Amason King amenusurika katika jaribio la kumuua mashariki mwa mji wa pwani wa Mombasa. Hata hivyo, habari zinasema kuwa, wauaji waliwaua raia watatu na mlinzi wa waziri huyo, na kuwajeruhi watu wengine kadhaa. Tukio hilo lilitokea jana Alhamisi wakati wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2013 katika eneo la kaskazini mashariki la Mtwapa huko Mombasa. Waziri huyo alisema kuwa, “Kijana mmoja alitokea kusikojulikana ndani umati wa watu na kunyakua kipaza sauti. Alianza kutuonesha mapanga. Alifuatiwa na watu wanne ambao nao pia walikuwa na mapanga.” Mnamo Septemba 30, kwa uchache Polisi wawili wa Kenya waliuawa katika shambulizi lililotokea jirani na mpaka wa Somalia. Siku hiyo hiyo, mtoto mmoja alipoteza maisha yake katika shambulizi la bomu katika kanisa moja mjini Nairobi. Habari zinasema kuwa mashambulizi ya hivi karibuni nchini Kenya huwenda yana uhusiano na uingiliaji na uvamizi wa kijeshi uliofanywa na Kenya katika nchi ya jirani ya Somalia. Mnamo Oktoba mwaka jana, Kenya iliwapeleka askari kwenye mpaka wake na Somalia kuwatafuta wapiganaji wa Al-Shabab, ambao nchi hiyo inawatuhumu kuhusika na utekaji wa raia kadhaa wa kigeni katika eneo la Kenya.
0 comments:
Post a Comment