Ndege moja ya Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish
Airlines) iliyokuwa ikitokea Istanbul kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro
ililazimika kukatisha safari na kurudi Istanbul baada ya kuzuka mapigano kati
ya mke na mume kwenye ndege.
Ndege hiyo iliyoondoka Istanbul saa 1: 30 kwa majira ya
nchini Uturuki, ilipofika kwenye anga ya Cairo, abiria wawili raia wa Slovenia Anton
Cestnik na mkewe Knavdiya Cesnit walianza kubishana na kuzozana. Cestnik aliwashambulia
abiri wengine huku akiharibu skrini iliyokuwa upande wa nyuma wa siti.
Abiria wengine waliwataarifu wafanyakazi wa ndege kuhusu
tukio hilol ambapo waliingilia kati lakini hawakuweza kumtuliza bwana huyo
mwenye umri wa miaka 54. Rubani aliamua kurudi Istanbul huku wafanyakazi wa
ndege wakiendelea kushughulika na abiria huyo wakamfunga pingu na kumpeleka
eneo la nyuma ya ndege. Cestnik alikata pingu hizo za plastiki na kuendelea
kuwashambulia abiria wengine.
Baada ya kutua katika uwanja wa Atatürk mjini Istanbul, Cestnik
na mkewe walikabidhiwa mikononi mwa polisi ambapo abiria wengine 149 walianza
safari kuelekea Dar es Salaam baada ya kuchelewa kwa muda wa saa 7. Katika maelezo
yake mbele ya polisi, Cestnik alisema kuwa ana tatizo la hofu.
Katika taarifa yake, Shirika la Ndege la Utruki
lilithibitisha kutoka kwa tukio hilo lakini halikufafanua zaidi. Kwa mujibu wa
sheria za usafiri wa anga, wanandoa hao walirejeshwa kwenye kituo chao cha
awali mjini Munich nchini Ujerumani, huku shirika hilo likimtoza faini Cestnik kwa
hasara ambayo shirika hilo liliipata kutokana na tukio hilo.
CHANZO: Sabah Daily
0 comments:
Post a Comment