UTURUKI YALAANI MASHAMBULIZI DHIDI YA WAISLAMU WA SRI LANKA



Nchi ya Uturuki imelaani vikali  mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Waislamu wachache wa Sri Lanka ambayo yameibua wasiwasi miongoni mwa jamii za watu wachache juu ya kuenea kwa visa vya ghasia.

"Tunaamini kuwa hatua za dharura zitachukuliwa ili watu wa Sri Lanka waishi kwa amani tena baada ya matukio ya mwaka  2009 ambapo serikali ilifanikiwa kukomesha vitendo vya kigaidi," imesema taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo iliyotolewa leo.

Sehemu za ibada na maduka ya Waislamu katika maeneo mbalimbali ya Sri Lanka yalishambuliwa siku ya Jumamosi asubuhi baada ya ghasia dhidi ya Waislamu zilizofanywa Juni 15 na kuua Waislamu watatu kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Magenge ya wafuasi wa dini ya Kibuddha yaliushambulia msikiti kwenye kijiji cha Navanthurai katika wilaya ya  Jaffna na chumba cha kusalia katika Chuo Kikuu cha Jaffna, kwa mujibu wa wakazi na wanafunzi wa eneo hilo.

Maduka kadhaa ya Waislamu yalichomwa moto siku ya Jumamosi katika eneo la Panadura, kilometa 25 kusini mwa Colombo.

Ghasia za sasa zilishamili baada ya mkutano mkubwa uliofanywa na kundi la Mabudhha wenye msimamo mkali Juni 15 katika mji wa  Aluthgama. Baadae kundi hilo lilielekea katika maeneo yenye Waislamu wengi na kuzusha ghasia kubwa.

Tokea wakati huo Polisi nchini  Sri Lanka walipiga marufuku mikusanyiko yote inayochochea maneno ya chuki dhidi ya dini na imani nyingine, msemaji wa polisi SSP Ajith Rohana amesema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment