UTAFITI: WATOTO MILIONI 30 WANAKOSA ELIMU AFRIKA

 

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yamesema kiasi cha watoto milioni 30 kusini mwa jangwa la Sahara hawaendi shule kwa sababu ya umaskini na mizozo ya kivita inayolikumba bara la Afrika.

Takwimu hizo mpya zimetolewa katika ripoti mbili zilizochapishwa jana Jumanne na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto (UNICEF) na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Kwa mujibu wa takwimu za UNESCO, kiasi cha watoto milioni 19 hawapati elimu ya msingi katika nchi za Magharibi na Katikati mwa bara la Afrika, huku kiasi cha watoto milioni 10 katika maeneo ya kusini na mashariki mwa Afrika wakikosa shule.


Ripoti hizo za UNICEF na UNESCO zinasema kuwa mgogoro wa kiuchumi duniani na mizozo ya vita barani Afrika vinafifiza juhudi za kuwarejesha watoto hao shuleni. Katika maeneo yenye vita mazingira yamekuwa hatari zaidi kwa watoto kufika shuleni.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment