SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye hospitali hiyo ya rufaa.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.

Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.

Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda Mugheny na David Mkufya wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya kukagua hospitali ya Rufaa ya                                 Mkoa huo.
(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Share on Google Plus

About www.habarika24.blogspots.com

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment