JE WAUJUA: MSTARI WENYE KUELEZEA MAISHA YAKO “LIFE LINE” KATIKA KIGANJA CHAKO? SOMA HAPA UUJUE SASA.

Leo tutauzungumzia mstari muhimu sana na kila binadamu anao:Mstari wa maisha. Mstari huu unaeleza kwa uwazi kabisa hali ya kiafya uliyonayo kama mzima, mgonjwa, utaishi muda gani duniani n.k. 
Ni rahisi sana kuutambua mstari huu ambao kwa kawaida upo chini ya dole gumba na umekizunguka kidole hicho kwa kama nchi moja hivi toka kila upande kilikoanzia, na ndio mstari mkuu kiganjani ambao huwezi kumsoma mtu mistari mingine bila kuuhusisha huu ambao ni mstari mama na kwa kawaida huwa unasomeka wazi sana mida yote ukionyesha umri mkubwa kabisa wa maisha ya mwanamke umsomaye kufikia hata miaka 70 huku mara nyingi ukitishia maisha ya wanaume kuwa hawaishi zaidi ya miaka 60 – 65 tu! 
Msiogope ndugu zangu kwa kuwa huu ndio ukweli wenyewe na hata mimi nimeukuta tu unaendelea duniani.
Kwa kawaida mstari huu huanzia chini ya kidole cha shahada na kuzunguka kupitia katikati ya kiganja chako huku mstari huo ukikitenga kidole gumba na kuishia chini kwenye kifundo cha mkono na kiganja chako.
Alama zilizopo katika mstari huo huonyesha wazi mambo kama matukio katika maisha yako, kutokea kwa safari au kuhama mji kabisa, kifo, ajali, maradhi makubwa yaliyokukuta na yatakayokukuta, historia ya maisha yako kwa ujumla inasomeka katika mstari huu kwa urahisi kabisa, 
Alama hizo huweza kuwa kisiwa, duara, vistari kukatiza mstari huo na alama nyinginezo nyingi tu ambazo hukujulisha matukio ya ghafla yaliyokukuta na yatayokukuta mbeleni na kukuacha na king’ora akilini kwa kuwa utakuwa ukijua nini kitatokea karibuni. 
Mstari wa maisha uliopo kiganjani mwako kama ni mrefu na unasomeka bila shida yoyote humaanisha kuwa wewe ni mtu mwenye afya njema na mwenye maono ya wazi kuliko wengine. Lakini pia hudhihirisha kuwa wewe ni mwenye maisha marefu na yenye tija duniani.      
Kama mstari huo kiganjani umenyooka haijalishi kama ni mfupi au mrefu basi ujijue kuwa wewe ni mtu mwenye kuheshimiwa na jamii inayokuzunguka. Kuchimbika au kuzama ndani kwa mstari huo humaanisha kuwa kuna vikwazo katika mafanikio yako labda tu uwe na bidii sana katika kazi zako ndipo utakapoona mafanikio yanakuja jioni sana au siku za mwisho kabisa katika jitihada zako za kuyasaka maisha mazuri na utajiri ikiwezekana.      
Mstari usioonekana vema kiganjani humaanisha matatizo ambayo hukukwaza katika jitihada zako kufanikisha maazimio yako mara kwa mara. Kwa mwanamke kuwa na mstari wa maisha uliopindapinda humaanisha ubishi na dalili za jeuri ambazo humuathiri sana mwenye mstari huo na humuwia vigumu kupata kazi au hata kuolewa na baadaye kumharibia maisha yake kisaikolojia akiamini hana kosa ila tu hapendwi kumbe tatizo ni huo mstari wa maisha kupindapinda kiganjani.       
Kama mstari huo wa maisha kiganjani umepindapinda basi hii ni ishara kuwa maisha yako yatakuwa matamu sana ujanani lakini mambo yataharibika kidogokidogo na kujikuta uzeeni ukipata taabu na kusimulia tu kuwa ujanani uliionja pepo na sasa haipo. Wengi tumezoea kuwasikia wazee wakilalamikia hali hii. Lakini katika maisha kuna mengi. Kuna kupanda na kushuka pia hivyo wakati mwingine mstari huu huonyesha kuwa inawezekana baada ya dhiki zako basi itafuata faraja!         
Ukiona mstari huo unaanza katika hali isiyoeleweka hapo kiganjani basi utambue kuwa wewe ni mtu wa mambo mengi na unaweza ukabadilika ukafanya kitu tofauti na walivyokuzoea watu na mwisho wake ni kukushangaa kwa vile hakuna ajuaye kuwa wewe ni “multi task person” na huna pingamizi unapoamua jambo lako.      
Kama mstari huo wa life line kwako unaanzia kwenye mlima wa mwezi yaani fundo la nyama la dole gumba na kujichimba ukitembea na kuishia basi jijue utahama mji au nchi kabisa siku moja. Kazini au nyumbani kwako utapata vikwazo sana toka kwa marafiki, wafanyakazi wenzio, mwenza wa ndoa na hata wanafamilia yako.      
Kama mstari huo wa maisha hapo kiganjani kwako umegusana na mstari wa riziki (Head line) basi jijue hutadumu katika mahusiano wala ndoa kwa kuwa shughuli zako zitaingilia mahusiano yako na kujikuta ukichagua shughuli zako na kuvunja uhusiano mara kwa mara. Ukiona mstari huo hauonekani vizuri basi mambo ni mabaya zaidi na unatakiwa uje nikusaidie kujifukiza na maandiko yenye alama za furaha katika mahusiano na kukupa baadhi ya kinga kulingana na tatizo litakaloonekana kiganjani hapo kwani historia inaonyesha wengi walipatwa na maradhi ya moyo na wengine waliishia kujinyonga kwa kukata tamaa kumbe ni vitu vya kawaida kabisa.      
Kama wewe mstari huo umeanzia kwenye kifundo cha kiganja ukawa unapanda tu  juu basi ujue wazazi wako bado wanayaendesha maisha yako na wewe bado unawategemea na upo karibu nao sana, na itakubidi siku ikifika uingie hasara isiyosahaulika kwa ajili yao.      
Ukiona mstari huo hapo kiganjani una sura kama nyoka umeelekea juu toka kifundoni basi ujue maisha yako si mazuri na inakubidi uombe msaada wa ndugu na marafiki wakusaidie kimaisha tu huku ukinitembelea tuone tunamalizaje tatizo hili.      
Mstari uliokatika katika hauna shaka! Huu huonyesha kuwa wewe ni mvivu na mara nyingi huwa unakata sana tamaa na pengine kuwakatisha tamaa ulionao kwa muda huo. na unafanya tu kazi ili maisha yaende kwa kudra tu. Unahitaji ushauri wa kitaalamu ikiwemo kuhudhuria kliniki inayotoa tiba za kukuokoa usiangamie.      
Mstari wa maisha kama unagusa ule wa mahusiano yaani Heart line basi ujijue kuwa wewe una akili kidogo sana na ndio maana huna cha kujivunia duniani na mbaya zaidi kama mstari huo wa maisha hausomeki au hauna mwelekeo sahihi basi ujue kuwa mambo yako hayatakuendea vema kwa vile una mahusiano na watu wengi sana hivyo hata hujui nani ushirikiane naye kukuletea maendeleo binafsi.      
Ukiona mstari huo umeanzia kwenye mlima wa nyama za dole gumba ujue wewe ni mtu mwenye bahati sana duniani na wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wapo macho kuhakikisha ukikwama wao wapo kukusaidia. 
Kama una mistari miwili ya maisha na kila mmoja upo kivyake vyake basi ujijue kuwa wewe ni msanii. Sio msanii mwongomwongo, bali unaweza kufanya kitu kwa akili yako na kikavuta hisia za jamii inayokuzunguka yote! Mwanamke mwenye mistari hii miwili basi huyo ana nafasi kubwa ya kuolewa na mwenye pesa nyingi au mtu maarufu sana katika jamii inayomzunguka japo kuna ya kumwambia ayafanye kabla kulinda mahusiano yake.      
Kama mstari wako wa maisha upo wazi kabisa na una mistari miwili badala ya mmoja basi hii ni dalili njema kwako kwa kuwa inasema kuwa wewe una bahati sana ya kupata kazi na biashara, lakini kama mstari huo unauona umezama sana ndani ya kiganja basi elewa kuwa una matatizo na shida nyingi sana zinazokufanya usifurahie maisha yako hivyo ni bora ukapata ushauri wa kinajimu uweze kuondokana na hayo matatizo na mikosi ya mara kwa mara.      
Kama msitari wako wa maisha unaanzia katika mstari wa riziki (Head Line unaelekea juu basi ujijue kuwa wewe ni mtu mjanja sana na akili zako watu watazitumia kuanzisha biashara ambayo italeta mafanikio makubwa kwa wengi. Usisahau kuwa kama una mstari wa aina hii basi katika ujana wako kuna jambo kubwa sana utalifanya utasifika sana na jamii haitakusahau kamwe!      
Ukiona mstari wako wa maisha unaanzia kifundoni mwa kiganja halafu unapotelea juu badala ya kukizunguka kidole gumba basi ujijue kuwa wewe ni mtu anayejiamini sana na huwa unayasaka mambo makubwa tu hapa duniani wewe hushughuliki na vitu vidogovidogo.      
Kwa kumalizia tu leo, kama unaona kuwa mstari wako wa maisha unaanzia katika mstari wa mahusiano na unapotelea kwenye vidole juu basi ujijue utasulubika sana ujanani lakini wewe ndie utakaye kuwa na maisha mazuri kushinda yeyote anayekuzunguka kwa kuwa utakapofikia miaka 50 kila kitu kitaanza upya yakiwemo maisha yenye raha mpaka uingie kaburini (sweet death)
Ndugu msomaji. Naona leo hukutegemea kukuletea habari ya mstari wa maisha kwa kuwa nilikuahidi kukuletea mstari wa riziki (Head line) lakini kwa sababu zilizo mbele yangu nilijikuta nikikuletea mstari wa maisha ambao tungeuzungumzia siku nyingine. Lakini nina uhakika japo umenielewa na kuna ya kufanya umeyaona pia. Kama hujaona kitu na una shaka na kitu kiganjani kwako basi karibu sana tutaelekezana.
Share on Google Plus

About www.habarika24.blogspots.com

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment