Mufti Mkuu wa Uganda, Sheikh Ramadhan Mubaje |
Mufti nchini Uganda, Sheikh Shaaban Ramadhan Mubaje
amepiga marufuku aya za Qur’an kutumika kama muito wa simu.
Mufti Mubaje alitoa Fat’wa hiyo wilayani Nakiso katika
mazishi ya aliyekuwa Sheikh anayehusika na Waislamu walio magerezani, Ibrahim
Ddumba.
Alisema moja ya sheria, kanuni na taratibu za QUr’an ni
kwa anayesikia aya zake zikisomwa anapaswa kusikiliza kwa utulivu wa hali ya
juu.
Kwa mujibu wa Sheikh Mubaje, hilo halifanyiki wakati wa
aya za Qur’an zinaposomwa katika muito wa simu.
“Qur’an inapotumika kama muito mwenye simu huacha
kusikiliza ama kwa kupokea au kukata jambo ambalo ni kinyume na mafundisho,”
alisema.
Sheikh Mubaje alisema ni vyema Waislamu wakaepuka
kutumia aya za Qur’an kama miito kwenye simu zao ili kutoingia kwenye makosa
hayo.
Kutokana na sense ya watu na makazi ya mwaka 2002,
asilimia 30.1 ya wananchi wa Uganda ni Waislamu.
Hata hivyo hakuna matumizi ya sheria za Kiislamu kwa
kuwa hakuna mahakama za Kiislamu zinazotambulika kisheria.
Ibara ya 129 ya katiba ya Uganda inaruhusu uanzishwaji
wa mahakama za kadhi lakini kutokana na mazingira mahakama hizo hazina nguvu
kisheria.
0 comments:
Post a Comment