Kuna tambi za aina mbalimbali,
zenye ladha na maumbo tofauti. Upishi wake nao unatofautiana kutokana na
aina ya tambi. Unaweza kuandaa tambi kama chakula kikuu, kama salad, au kama
kitafunwa, kutokana tu na aina ya tambi utakayochagua na jinsi utakavyoiandaa.
MAHITAJI
- Tambi paketi 1 -zenye umbo la spring
- Jibini kavu kikombe 1: Sugua kwa sugulio la
karoti (shred)
- pilipili hoho za kijani 3 kubwa- kata vipande
vinene kwa urefu
- Pilipili hoho nyekundu Moj: kata vipande vinene
kwa urefu kisha gawanya kila kipande mara mbili
- Giligiliani kavu kijiko 1 cha chakula : saga
mbegu kavu za giligiliani
NJIA
1.
Chemsha maji
mengi hadi yatokote (lita mbili). Ongeza tambi, acha zichemke hadi ziive .
- Usiache ziwe rojo hazitapendeza
2.
Katika kikaango au
sufuria zito weka pilipili hoho za rangi zote, kisha weka jikoni katika moto
mdogo, geuza kila mara hadi zote zipate joto na kuanza kusinyaa kisha weka
pembeni
- Usiongeze kitu chochote kwenye pilipili
hoho
3.
Tambi zikiiva
chuja maji yote kisha weka tambi kwenye bakuli la chuma au sufuria pana
- Chuja maji mara tu tambi
zikiiva, usiache zipoe wala kupoteza joto
4.
Katika bakuli la
tambi ongeza pilipili hoho. Nyunyuzia chumvi na unga wa giligiliani kisha
nyunyuzia jibini na changanya vizuri.
Saladi yako iko tayari kwa
kula. Unaweza kula salad hii na vyakula vingine au ukaifanya sehem kuu ya
mlo wako. Ni vyema kujua kwamba saladi si lazima ziwe mboga za majani peke
yake, yaweza kua mchanganyiko wa mboga za majani na vyakula vingine kama ilivyo
salad hii.
(Kwa hisani ya: Tolly Kitchen)
0 comments:
Post a Comment