Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili
leo Sudan Kusini. Kiongozi huyo anatarajiwa kukutana na Rais Salva Kiir, watu
walioyakimbia makazi, viongozi wa kijamii na wafanyakazi na walinda amani wa
Umoja wa Mataifa.
Aidha, anatarajiwa kutoa wito wa kukomeshwa mapigano
ambayo yamepoteza maisha ya watu wengi ambapo viongozi wamepuuza juhudi za kuleta amani licha ya onyo na tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa
kuhusu mauaji ya kimbari na ukosefu wa chakula.
0 comments:
Post a Comment