Kwa uchache watu wanne wakiwemo maafisa wawili wa polisi
wameuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari katika mji mkuu wa
Kenya, Nairobi.
Polisi wamesema kuwa mlipuko huo umetokea nje ya kituo
cha polisi Pangani mjini humo.
Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi hiyo, imethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bomu hilo lilitegwa katika gari aina ya
saloon.
Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi
hilo. Lakini polisi wanasema kuwa mitaa hiyo iliwahi kushuhudia mashambulizi
kama hayo.
Katika miezi ya hivi karibuni Kenya imekumbwa na
mashambulizi kadhaa ya mabomu.
Mwezi Septemba mwaka jana, shambulizi kwenye jengo la
kibiashara la Westgate mjini Nairobi liliwaua watu wasiopungua 67.
0 comments:
Post a Comment