RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA HOSPITALI KUBWA NA YA KISASA YA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI KIJIJINI MLOGANZILA.

    Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chung IL  wakikata utepe kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila maeneo ya Kwembe, Kilometa 24 kutoka jijini Dar es salaam, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo itakayokuwa kubwa kuliko zote nchini jana April 24,  2014.

    Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Korea nchini Mhe. Chungh IL wakiweka udongo kwa pamoja wakati wa kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila Kilometa 25 kutoka jijini Dar es salaam. 

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mkasi Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Mhe John Mnyika ili na yeye akate utepe na viongozi wengine kuashiria uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa  Hospitali kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili kijijini Mloganzila mkoa wa Pwani jana April 24,  2014.

PICHA NA IKULU.


Share on Google Plus

About www.habarika24.blogspots.com

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment