Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Deshchytsia |
Kaimu Waziri wa
mambo ya nje wa Ukraine Andriy
Deshchytsia amesema kuwa nchi yake iko tayari kupambana na Urusi iwapo Urusi
itapeleka vikosi vyake nchini humo.
Shirika la habari la Associated Press limemnukuu waziri
huyo akisema kuwa wananchi na jeshi la Ukraine wako tayari kukabiliana na
Urusi, kuitetea ardhi na kuilinda nchi yao.
Kauli ya Waziri huyo ni radiamali dhidi ya mpango wa
Urusi kufanya mazoezi ya kijeshi kwenye mpaka wa Ukraine baada ya waandamanaji
wapatao 5 wanaoiunga mkono Urusi kuuawa mashariki mwa Ukraine.
Deshchytsia amesema kuwa mazoezi hayo yanazorotesha hali
ya mambo katika eneo hilo na kwamba sasa wako tayari kuikabili Urusi moja kwa
moja iwapo itaingia Ukraine.
Aidha, Deshchytsia aliitolea mwito Jumuiya ya Ulaya
kuiwekea Urusi vikwazo vipya.
Leo Ukraine imetangaza kuanzisha awamu ya pili ya
operesheni maalumu kuwaondosha wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi katika miji
ya mashariki mwa nchi hiyo.
Taarifa kutoka mjini Kiev zinasema kuwa awamu hiyo
imeanza katika mji wa Slavyansk, ambao
unashikiliwa na waandamanaji.
Awamu ya kwanza ilianza jana, ambapo vikosi vya nchi
hiyo viliingia katika mji huo na waandamanaji 5 wanaiounga mkono Urusi
waliuawa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov ameilaana
vikali operesheni hiyo na kuiita kuwa ni “jinai kubwa” akisema kuwa serikali ya
Ukraine imeanzisha vita dhidi ya wananchi wake yenyewe.
Mnamo Aprili 17, serikali ya mpito ya Ukraine pamoja na
Marekani, Urusi na Jumuiya ya Ulaya zilifikia makubaliano mjini Geneva Uswiss,
ambayo yalizitaka pande zote kutatua mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine,
ambapo waandamanaji wameendelea kuyakalia majengo katika miji na majiji kadhaa.
0 comments:
Post a Comment