MWAKALEBELA AWATAKA WAJASILIAMALI IRINGA KUEPUKA MATAPELI KATIKA MIKOPO YA BENKI YA WANAWAKE TANZANIA

Mwakalebela katikati akitoa maelekezo kwa  wajasiliama mali wanaohitaji                                                          mikopo ya benki ya wanawake Tanzania.
     Wakina mama  wajasiliamali mjini Iringa  wakipewa maelekezo kutoka mkurugenzi   mtendaji  wa kampuni ya ujasiliamali nchini  ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela (kulia)  wakati wa  semina  hiyo  inayoendelea katika ukumbi wa maendeleo ya jamii                                               mjini Iringa.
                     Wajasiliama mali  wanaotarajiwa  kukopeshwa na benki ya                                         wanawake Tanzania  wakipewa mafunzo  leo.

  Baadhi ya  wajasiliamali wenye ulemavu  wanaoshiriki  semina ya ujasiliama mali chini ya ufadhili wa kampuni ya VANNEDRICK (T) Ltd kwa  ajili ya kukopeshwa fedha na Benki ya  wanawake  Tanzania (TBW) wakimsikiliza mkurugenzi   mtendaji  wa kampuni ya ujasiliamali nchini  ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela (katikati)  wakati wa  semina  hiyo  inayoendelea katika ukumbi wa maendeleo ya jamii mjini Iringa.
MKURUGENZI  mtendaji  wa kampuni ya ujasiliamali nchini  ya VANNEDRICK (T) Ltd Fredrick Mwakalebela  amewataka wajasiliamali mjini Iringa  kuepuka matapeli  wanaotaka  kuwatoza fedha ili kunufaika na mikopo ya benki ya  wanawake Tanzania (TBW).

Pia Mwakalebela  amepongeza  jitihada za  wanawake na  wajasiliama mali mjini Iringa  kujitokeza kwa wingi katika mafunzo ya ujasiliama mali kabla ya kukopeshwa na benki  hiyo hivi karibuni .

Akizungumza  jana wakati wa mwendelezo wa  semina  hiyo kwa wajasiliama mali katika  ukumbi wa maendeleo ya jamii Kitanzini mjini hapa ,Mwakalebela  alisema  kuwa  amefurahishwa na idadi kubwa ya  wanawake wapatao  zaidi ya 400 ambao  wamejitokea  kutaka  mikopo hiyo  japo  wapo  baadhi ya  watu  wanaweza  kutumia njia  hiyo kwa  ajili ya kujipatia fedha kijanja .

" Neema kama  hizi zinapojitokeza  wapo  baadhi ya  watu wasio na malengo mazuri ambao  wamekuwa  wakitaka  kujinufaisha kwa  kuwachangisha   fedha  wajasiliama mali  hao  ili kupata mikopo .....hivyo  wanawake  wote na wajasiliamali  wanapaswa  kuwa makini wasikubali  kutoa  pesa  yoyote kwa ajili ya mikopo ya TBW "

Mwakalebela  alisifu  utaratibu wa benki  hiyo ya wanawake Tanzania  kuwa haumtaki mwomboji wa mkopo  kuchangia  fedha  yoyote  zaidi ya  kufungua akaunti ya kikundi kwa kiasi cha Tsh 10,000 pekee kabla ya  kukopeshwa mkopo husika.

Hata  hivyo  Mwakalebela kama mdhamini mkuu wa mafunzo hayo  mkoani Iringa  alisema  kuwa amevutiwa  zaidi na mwitikio mkubwa wa  wajasiliama mali  kujitokeza  kushiriki mafunzo hayo tofauti na mikoa mingine ambayo benki  hiyo  imepata  kupita na kuwawezesha  wajasiliamali kama  hao.


Alisema kwa upande  wake  amepata  kuzunguka maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa hasa  yale ya pembezoni na kuwahamasisha  wajasiliamali kujitokeza   kujiunga na vikundi ili  kunufaika na  mikopo  hiyo kupitia benki hiyo ya  wanawake Tanzania.


Share on Google Plus

About www.habarika24.blogspots.com

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment