Serikali ya Madagascar imepiga marufuku kutembea nyakati
za usiku katika kisiwa cha Nosy Be kilichopo kaskazini magharibi mwa nchi hiyo,
baada ya wananchi wenye hasira kuwauwa
watu watatu wakiwemo raia wawili
kutoka nchi za Ulaya.
Wizara ya Usalama wa Taifa ya Madagascar imetanGhaza
kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya raia wawili kutoka Ufaransa na Italia
wakishirikiana na mwenyeji Mbukini kupigwa na kisha kuchomwa moto hadi kufa baada ya kutuhumiwa kuwa walimuuwa
mtoto wa miaka minane kwa shabaha ya kuchukua baadhi ya viungo vyake.
Kiongozi mwandamizi wa wizara hiyo amesema kuwa, awali
watuhumiwa hao walikiri kutenda jinai hiyo ya kumuua mtoto huyo baada ya
kupigwa na wananchi waliokuwa na hasira.
CHANZO: IRIB
0 comments:
Post a Comment