WAZIRI Mkuu wa Libya, Minister Ali Zeidan, ameripotiwa
kutekwa na watu wenye silaha katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli, serikali ya
Libya imetengaza.
“Mkuu wa serikali ya mpito, Ali Zeidan, alipelekwa
sehemu isiyojulikana kwa sababu zisizojulikana” asubuhi ya leo, ilisema taarifa
hiyo ya serikali.
Karani mmoja wa hoteli, ambaye hakutaka kutaja jina lake
kwa sababu ya kutoruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari, alisema kuwa waasi
wenye silaha walimchukua Zeidan kutoka Hoteli ya Corinthian kwenda kwenye
msafara wa magari uliokuwa ukisubiri eneo hilo.
Tukio hilo linatokea siku moja baada ya Waziri Mkuu huyo
kutoa wito wa kukomesha uasi katika nchi hiyo.
Zeidan alikiambia kituo cha habari cha serikali kwamba Libya
ilikuwa ikitumika kusafirisha silaha katika ukanda wote wa eneo hilo.
Utekwaji huo umefanywa siku kadhaa baada ya vikosi vya
Marekani kufanya shambulizi la kushittukiza mjini Tripoli na kumkamata mtu
anayedaiwa kuwa kiongozi wa al-Qaeda nchini humo, Abu Anas al-Libi.
Al-Libi, mwenye umri wa miaka 49, anaripotiwa
kushikiliwa na kuhojiwa katika meli ya kivita ya Marekani, USS San Antonio,
ambayo imeweka nanga baharini.
Serikali ya Libya inalichukuliwa shambulizi hilo la
Marekani kama utekaji nyara wa raia wa Libya, na wamemhoji balozi wa Marekani
nchini humo kuhusu hatua hiyo.
Mnamo Oktoba 8, Zeidan aliwaambia waandishi wa habari
mjini Tripoli kuwa, uhusiano wetu na Marekani ni muhimu, na tunalizingatia
hilo, lakini pia tunawajali raia wetu, na hilo ndio jukumu letu.”
0 comments:
Post a Comment