WAKAGUZI wa Umoja wa Mataifa wameanza zoezi la
kuziharibu ghala za silaha za kemikali za Syria.
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa amesma kuwa mpaka mwisho
wa siku ya leo shehena moja ya silaha na zana za kutengenezea silaha hizo zitakuwa
zimeharibiwa.
Wachunguzi hao wamepewa kazi na Umoja wa Mataifa
kuziharibu kabisa silaha za kemikali za Syria, kufuatia nchi hiyo kusaini mkataba
wa kuwa mwanachama wa umoja wa kuzuia ueneaji wa silaha hizo.
Aidha, programu ya kuziangamiza silaha hizo imekuja
kufuatia shutuma zilizotolewa dhidi ya serikali ya Damascus kuwa ilitumia
silaha hizo katika shambulizi moja karibu na mji wa Damascus lililofanyika
mwezi Agosti mwaka huu na kuua mamia ya wananchi.
Hata hivyo, serikali ya Damascus imekuwa ikikanusha
tuhuma hizo na kuwalaumu waasi kuwa ndio wahusika wakubwa.
Programu hiyo inatarajiwa kuendelea mpaka katikati ya mwaka ujao.
0 comments:
Post a Comment