POLISI mkoani Mtwara inawashikilia watu 11 kwa tuhuma za
kupata mafunzo ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs za al-Shabaab.
Tukio hilo la aina yake limetokea katika mlima
Makolionga wilaya ya Nanyumbu mkoani hapa ambapo pia CDs zenye mafunzo
mbalimbali ya kijeshi 25 zimekamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Zelothe Stephen
ameuambia “mtandao wa Kusini Leo” kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wiki moja
iliyopita baada ya jeshi lake kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema: “CD
hizo zilikuwa zinatoa mafunzo ya Al-Shabaab ya kuchinja watu, Mauaji wa Osama
Bin Laden, Zindukeni Zanzibar, Kuandaa Majeshi, Mauaji ya Idd Amin na Mogadishu
Sniper,” alisema Stephen.
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi wa wilaya ya Nanyumbu
mkoani hapa na kwamba walikuwa wakiongoza na Mohamed Makande 39, mkazi wa
kijiji cha Sengenya ambaye pia anashikiliwa na jeshi hilo.
Aliwataja wengine waliokamatwa kuwani Hassan Omary (39)
mkazi wa kijiji cha Nanyulu, Rashid Ismail (27). Abdallah Y. Hamisi (32), Salum
Wadi (38), Fadhili Rajabu (20), Abbas Muhidini (32), Ismail Chande (18), Said
Mawazo, Issa Abeid (21), na Ramadhani Issa (26) wote wakazi wa kijiji cha
Likokona.
Kuhusu vitu watuhumiwa walivyokamatwa navyo, Kamanda
Zelothe alisema, “Tumekamata mapanga mawili, Deki ya DVD, Solar, Visu, Tochi,
Betri, Simu za kiganjani 5, Vyombo mbalimbali vya kulia chakula, Baiskeli tatu,
Vitabu mbalimbali wa dini ya Kiislam, Unga wa mahindi kilo 50, Mahidi kilo 150
na virago vya kulalia. Vingine ni mfuko wa kijani unaosadikiwa ni wa kijeshi
wenye nembo ya nanga ya meli yenye mistari kulia na kushoto na nyoka katikati.”
Alisema jeshi lake licha ya kuwafikisha watuhumiwa
mahakamani, linaendelea na uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na Polisi Makao
Makuu kwa lengo la kufanikisha kuunasa mtandao mzima.
0 comments:
Post a Comment