Boti moja iliyokuwa imewabeba mahujaji wa Kanisa
Katoliki imepinduka katika Mto Amazon nchini Brazil na kupoteza maisha ya watu
wasiopungua 12 na wengine 6 wakiwa hawajulikani walipo.
Tukio hilo lilitokea kwenye ukingo wa Mto
Amazon jirani na mji wa Macapa, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Amapa, nchini
humo.
Polisi walishindwa kufafanua kilichosababisha boti hiyo
kupinduka, lakini uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini kama chombo hicho
kilikuwa kimebeba uzito unaozidi kiwango ambao ni watu 40.
Miongini mwa waliofariki ni pamoja na nahodha wa boti
hiyo, Reginaldo Reis Nobre, kwa mujibu wa maafisa wa polisi.
Maafisa hao wamesema kuwa watu wa uokozi walikuwa
wakitafuta manusura wengine, ambao walikuwa sehemu ya kundi lililokuwa
likishiriki katika sherehe maarufu za kidini nchini humo.
Katika maeneo mengine, barabara za ndani ya miji ya
Brazil zimeendelea kushikilia rekodi ya kuwa miongoni mwa barabara hatari zaidi
duniani.
Ajali za barabarani nchini Brazil hupoteza maisha ya
zaidi ya watu 35,000 kila mwaka.
0 comments:
Post a Comment