Leo tarehe 1/10/2013 ilisomwa tena kesi ya shekh ponda
katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa Morogoro.
Kama madai ya wakili wa Shekh Issa Ponda kwamba shitaka
la kwanza la kushtakiwa kwenda kinyume na masharti aliyopewa katika mahakama ya
kisutu basi shtaka hilo linapaswa kuendeshwa na mahakaam ya kisutu na sio
katika mahakama ya mkazi mkoani Morogoro.
Hivyo leo hii watu wengi walijaa mahakamani hapo ili
kujua hatma ya kesi kwamba itaamishiwa Kisutu au itabakishwa Mkoani Morogoro.
Kesi hiyo imeamuriwa kubaki mkoani Morogoro baada ya
mjadala mrefu wa kisheria kati ya wakili wa Shekh Ponda na upande wa
mashtaka.Kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 7 November mwaka huu ambapo
mahakama itaanza kusikiliza Mashahidi wa kesi hiyo.Sheikh Ponda Amerudiswa
Rumande.
0 comments:
Post a Comment