BUNGE la Ethiopia limemchagua Mulatu Teshome kuwa rais
mpya wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka sita, akichukua nafasi ya Girma
Wolde-Giorgis.
"Baada ya ufunguzi wa bunge jipya, kikao cha pamoja
cha Wabunge wa Shirikisho kilimchagua Balozi Dk. Mulatu Teshome kuwa Rais wa Ethiopia,"
ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya nje.
Mulatu alikuwa balozi wa Ethiopia nchini Uturuki mpaka
alipochaguliwa kwenye wadhifa huo mpya. Pia aliwahi kuwa balozi wa Ethiopia
nchini China na Japan, na pia aliwahi kuwa waziri wa kilimo.
"Ninahisi kupata heshima kubwa kuwa rais wan ne wa
Jamhuri ya Shirikisho la Ethiopia,” alisema Mulatu baada ya kula kiapo, na
kuahidi kutekeleza “mikati ya maendeleo ya nchi.”
Rais aliyemaliza muda wake, Girma Wolde-Giorgis,
aliingia madarakani mwaka 2001 na kuchaguliwa tena mwaka 2007.
Nchini Ethiopia, ofisi ya urais ni cheo cha heshima tu
na madaraka hasa yanakuwa mikononi mwa waziri mkuu.
0 comments:
Post a Comment