Mwana jinakolojia (elimu ya uzazi) kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia, Denis Mukwege, amepokea tuzo ya mwaka huu wa 2013 ya
Kazi Za Kiraia, katika kutambua kazi ya utoaji huduma za kiutu katika eneo la
Mashariki mwa nchi hiyo lenye migogoro ya vita na machafuko.
Mukwege, ambaye aliwania Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka
huu, alipata tuzo hiyo jana Jumanne aliyotunukiwa kwa kazi yake ya kuwahudumia
wanawake waliobakwa na waathirika wa vitendo hivyo mashariki mwa Kongo ambapo
hospitali yake inayojulikana kama Panzi Hospital, imekuwa msitari wa mbele
katika kuwahudumia maelfu ya akina mama Kikongo wanaokumbwa na zahma hiyo
thakili.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Jeshi la Kongo na makundi
mbalimbali yenye silaha, kama vile M23, wanahusika na vitendo vya kuwabaka
raia.
"Nilipokutana na wanawake hawa maisha yangu
yalibadilika kabisa,” anasema Mukwege. “Taaluma yangu kama daktari ilinifanya
niwe shuhuda wa moja kwa moja wa unyama dhidi ya binadamu ambao ni vigumu
kuuelewe kikamilifu. Hii ni kwa sababu dhuluma za kingono zinawalenga watu
ambao ni rasilimali yetu ya juu kabisa: mama zetu, wake zetu na mabinti zetu.”
Mukwege anasema yumkini ubakaji ndio “uhalifu mkongwe
zaidi na usiolaaniwa sana".
"Hakuna kitu kisichowezekana kuhusu hili tatizo,”
anasema. “Tunaweza kuleta mabadiliko chanya nchini Kongo.”
Makundi kadhaa yenye silaha, ikiwemo M23, wanaendesha
harakati zao za uasi mashariki mwa Kongo na wanapigania kuidhibiti nchi hiyo
kubwa yenye maliasili za madini, kama vile dhahabu, urani, coltan, ambayo
hutumika katika utengenezaji wa vifaa vingi vya elektroniki, ikiwemo simu za
mkononi.
Tangu mwezi Mei 2012, takriban watu milioni 3
wameyekimbia makazi yao katika eneo la mashariki mwa Kongo. Takriban watu milioni
2.5 ni wakimbizi wa ndani, huku zaidi ya watu 460,000 wamekimbilia katika nchi
za Rwanda na Uganda.
Kongo imekuwa ikikabiliwa na matatizo matatizo kwa
miongo kadhaa, kama vile umaskini uliokithiri, miondombinu mibovu, na vita
katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo ambavyo viliibuka tangu mwaka 1998 na
kugharimu maisha ya zaidi ya watu milioni 5.5.
0 comments:
Post a Comment