Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
kamishna wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Suleimani Kova amesema ugunduzi
huo ulibainika baada ya uchunguzi uliofanywa na madaktari wa hospitali ya taifa
Muhimbili wakishuhudiwa na polisi pamoja na baadhi na ndugu wa marehemu ambapo
ameelezea marehemu alikutwa na hati za dharura za kusafiria nchi za nje na kuwa
uchunguzi zaidi unafanyika kubaini mtandao mzima wa usafirishaji wa dawa hizo
uliomuhusisha marehemu.
Katika tukio lingine kamanda Kova amesema jeshi hilo
linamshikilia mtu mmoja aliyejifanya kuwa mtumishi wa wizara ya afya na ustawi
wa jamii aliyekamatwa katika hospitali ya taifa Muhimbili akiwa amevalia mavazi
ya kidaktari pamoja na nyara mbalimbali zenye nembo ya hospitali hiyo kwa lengo
la kuwaibia watu.
Kutokana na tukio la ugaidi nchini Kenya kamanda Kova
amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulizi maeneo yote yenye mkusanyiko wa
watu wengi na kutoa wito kwa jamii kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi la polisi
pindi watakapo baini mtu au kikundi cha watu wanaowatilia shaka.
CHANZO: ITV
0 comments:
Post a Comment