ASKARI watatu wa Kenya walipoteza maisha yao wakati
wakipambana kuwaokoa mateka katika shambulizi kwenye Jumba la Kibiashara la
Westgate mjini Nairobi.
Askari wengine 8 wapigania maisha yao hospitalini baada
ya kujeruhiwa kwenye operesheni hiyo.
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF), Jenerali
Julius Karangi alisema kuwa askari 11 walijeruhiwa na kupelekwa kwenye
hospitali ya jeshi kwa matibabu. “Kwa bahati mbaya watatu kati yao walipoteza
maisha.”
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi, Kanali Cyrus
Oguna inasema kuwa KDF walionesha ari kubwa katika juhudi za kutekeleza operesheni
ndani ya jengo la Westgate.
“Mazingira tata na hatari ya tukio hili yalihitaji
uangalifu na tahadhari ya hali ya juu kuhakikisha usalama wa mateka. KDF ilifanya
kazi hii kwa kiwango cha hali ya juu kabisa cha weledi.” Alisema Oguna katika
taarifa hiyo.
Mkuu wa vikosi vya ulinzi, Jenerali Karangi alizifariji
familia za askari waliouawa na kuwaelezea kuwa mashujaa walioitoa damu yao kwa
ajili ya ulinzi wa taifa.
“Tunapenda kuwathibitishia kuwa matukio kama hayo
hayarudisha nyuma ari ya KDF ya kuhakikisha kwamba amani na uthabiti
vinapatikana nchini Somalia na katika ukanda huu.” Iliongeza taarifa hiyo.
CHANZO: KTN KENYA
0 comments:
Post a Comment